Kuwa mwanasayansi wa kukariri darasani ni tofauti na mwanasayansi wa kuvumbua, unaweza kuniambia amewahi kuvumbua nini katika uanasayansi wake? Tuache hilo ni mengi sana mpaka sasa yamesemwa hapa jukwaani na ya msingi achia chuki binafsi lakini kafanyia kazi lipi la maana? Hebu nisaidie kwa kuwa unaonekana una uelewa wangalau wa kuridhisha, ni eneo gani unataka nikupe takwimu zake ili afanyie kazi? Isije ikawa ni mwanasayansi kwa sifa za kupewa dakika za mwisho tukakuta na yeye ni walewale viongozi watakaoendesha nchi kwa kuagiza hadi toothpick. La kwanza la kufanyia kazi kabisa ni kubadili mifumo ya kiutendaji kwa taasisi mbalimbali za umma, kama mahakama, jeshi la polisi, vyeo vingi visivyo na tija ambapo unamkuta mtu mmoja ana vyeo mbalimbali mpaka anajikuta yeye ndio mtunga sheria lakini ana maslahi binafsi na sekta husika mfano naitaja hapo chini
- Katibu mkuu wa wizara
- Katibu mkuu sijui kiongozi wa wizara
- waziri/naibu waziri wa wizara
- comissioner wa wizara
- sijui CEO wa wizara
Samahani kwa kutaka vyeo vyote hivyo japo sio kwa usahihi lakini unapata picha na wakati huo huo wenye vyeo hivyo unawakuta sijui ni wenyeviti wa bodi sijui ya utalii, viwanda nk. Cha ajabu unakuta kwenye wizara husika budget ikija unakuta 70% yake ni gharama za posho na mishahara lakini maendeleo ni 30% achia mbali miradi hiyo kufanyika chini ya kiwango. Niendelee ama utampelekea kwanza hayo? Tunangoja utekelezaji wangalau wa miezi 6 hii ya mwanzo.