Ikulu na Wizara ya Afya lugha gongana

Ikulu na Wizara ya Afya lugha gongana

Ushauri wa aina hii ndo unahitajika. Naamini umeipata na kuisoma sera na ilani ya CCM ambayo Mh Rais wa awamu ya tano ameahidi kuitekeleza. Najua imetaarishwa na wataalamu wa aina mbalimbali. Pia ilitolewa humu jamvini kwamba Dr Magufuli wakati akiendelea na kampeni aliteua jopo la wataalamu akawapa dondoo rejea kutengeza mikakati ya kutekeleza sera na ilani ya hiyo ya CCM. Kufanya hivyo ndiyo misingi ya kisayansi (ona/sikia, kachunguze, tafsiri/tafakuri, chukua hatua).

Kinachotokea na kuendelea humu jamvini ni ushabiki tu wa kushutumu, kulaumu au kutetea. Tusubiri maamuzi yake na hatua zitakazofuata, baada ya kuwa amepata takwimu. Wanaosema anakurupuka hawajui misingi ya uongozi, utawala na menejimenti.

TAFAKARI CHUKUA HATUA

Samahani naomba nikuulize, hivi wewe unaishi hapa nchini ama nje ya nchi, ni nani aliyewahi kukuambia sera na ilani ya ccm imewahi kuwa mbaya? Hiyo mikakati mizuri imebaki kuwa nadharia ndani ya nchi hii na tatizo kubwa ni uwepo wa haohao watunga sera wazuri. Unakuta hao wataalamu ndio mabingwa wa kutunga sera lakini ukiangalia hayo malipo yao hao wasimamia sera yanazidi hata matokeo ya hizo sera. Tatizo jingine unakuta rasilimali watu za utekelezaji wa hizo sera wengi wako kiundugu/ kujuana achia mbali watu wanaojipa vyeo maradufu ili kukidhi matumbo yao. Hili ni tatizo sugu na ndio maana unakuta sekta nyingi zimejaza watu incompetent kwa fani husika kiasi kupelekea huduma kutolewa kwa kiwango duni ama kuweka gharama za juu kuliko uhalisia. Nikijaribu kuangalia sioni Magufuli anafanya nini kuondokana na kichaka hiki, hali hii inanifanya nione wale wanaotaka tumsifie Magufuli ndani ya wiki moja hii kama wanatuona majuha. Aina yetu ya kukosoa wangalau inamfanya asilewe sifa mapema kwani tunajua wanaomsifia ndio hasa vikwazo vyake kwani hatua nyingi anazochukua wao ndio wahanga namba moja na wao ndio watakakwamishwa tubaki palepale kuwa soko holela la bidhaa substandard nk. Mpelekee hii Magufuli mwambie Tindo wa jf anataka aitolee hii macho kwani mimi ni mkulima ninayeumizwa sana na mtindo wa kuuza mazao kwa mtindo wa rumbesa, huku madalali hapo kariakoo wakiwa na vitambi vikubwa bila kujua shambani tunakutana na dhahama gani, wakati huohuo mamlaka husika zikabiki na sera na ilani nzuri ya mkulima bila utekelezaji.
 
Wee mcfm40 acha kulisha watu uongo huyo Kikwete alikuwa akiongea kwenye kamati kuu gani maana hadhi yake yeye ni Kamati kuu ya CCM ambayo hatujaona ikikutana.
Labda kaongea kwenye kamati kuu za huko Msoga ambazo si za hadhi yake.
 
Wanaodhani Kikwete anaweza kumtikisa Magufuli na serikali yake atakuwa anakosea sana. Kikwete kwa Magufuli ni sawa na mwanamasumbwi Maugo kwa Tyson.

Kwa taarifa tu Kikwete ni mwoga mno tena mno kinachomsaidia ni ule uchekbob na utoto wa mjini, na kwa hulka yake hawezi kujaribu kumkwamisha JPM ndani ya miaka miwili hii atakayokuwa m/kiti na akijaribu tu atapigwa daflao na CCM yake ambayo hatakuja aisahau milele.
 
Nani ana ule wimbo wa CCM ni ile ile aniwekee hapa niburudike
 
Juzi rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza Muhimbili na kumwondoa mkurugenzi na bodi ingawa bodi ilishamaliza muda wake na mkurugenz kahamishiwa wizarani tu wala hajafukuzwa.

Ikulu ikadai Magufuli alikasirishwa sana kukuta mashine za MRI hazifanyikazi ndio maana kaisimanisha bodi,
Lakini jana kupitia Azam Tv Katibu mkuu wizara ya Afya Bw.Mbando alisema mashine haikutengenezwa kwa sababu Magufuli alisema bali ilikuwa tu kwamba akivyotenbekea pale mchakato wa kuikarabati mashine ulishakamilika.

Alisema tatizo lililokuwepo ni kwamba Phillips wanaidai serikali zaidi ya bil 7 ndio maana waligoma kuitengeneza hiyo nashine.

Sasa mchakato wa kupunguza deni ndio ulikuwa unaendelea na zilishapatikana bil3 kutoka hazina walizolipwa juzi hao Phillips ndipo wakakubali kuja kuifanyia mashine ukarabati.

Na hili linaleta maana zaidi kwa sababu wizara haiwezi kutoa bil3 ghafla tu bila kuwa zilikuwa kwenye mchakato.

Kwa hiyo hapa ikulu ilifanya usanii wa hali ya juu kuwaaminisha watanzania kwamba kulikuwa na uzembe pale muhimbili wakati uzembe ulikuwa serikalini. Serikali ilishindwa kulipa deni kwa wakati.

Na inasemeka hili jambo halikumfurahisha Kikwete kwa sababu lilipeleka picha kwamba serkali yake ilikuwa goigoi.

Haya ndio madhara ya Maigizo na kulazimisha kupendwa! Ikulu kuweni makini! Mwongozeni rais vizuri!

Lumumba wakikusikia utakula matusi ya nguoni!.
Mara nyingi maamuzi ya papo kwa papo tena level ya Raisi -ni maumivi maana Mkuu wa nchi mara nyingi amezungukwa na wanasiasa ambao uongo ndiyo maisha yao korido za Magogoni!.
Raisi Makini atakwenda site kujionea mwenyewe ,kuwaita chobingo watendaji wa Taasisi husika hasa -mameneja au kwa Muhimbili Madokta wa Idara mbalimbali na kuzungumza nao face to face behind closed doors na kumalizia na Manejimenti ya kuu ya Taasisi (Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi)-baada ya hapo anasepa kwenye Magogoni-kitakachofuata ni vitendo!.

Wanaodhani Kikwete anaweza kumtikisa Magufuli na serikali yake atakuwa anakosea sana. Kikwete kwa Magufuli ni sawa na mwanamasumbwi Maugo kwa Tyson.

Kwa taarifa tu Kikwete ni mwoga mno tena mno kinachomsaidia ni ule uchekbob na utoto wa mjini, na kwa hulka yake hawezi kujaribu kumkwamisha JPM ndani ya miaka miwili hii atakayokuwa m/kiti na akijaribu tu atapigwa daflao na CCM yake ambayo hatakuja aisahau milele.

Subiri uone...
 
Kamati kuu ya ccm ilikaa jana baada ya JK kumkabidhi JPM ofisi. JPM alialikwa kuhudhuria maana yeye sio mjumbe wa CC
 
Lumumba wakikusikia utakula matusi ya nguoni!.
Mara nyingi maamuzi ya papo kwa papo tena level ya Raisi -ni maumivi maana Mkuu wa nchi mara nyingi amezungukwa na wanasiasa ambao uongo ndiyo maisha yao korido za Magogoni!.
Raisi Makini atakwenda site kujionea mwenyewe ,kuwaita chobingo watendaji wa Taasisi husika hasa -mameneja au kwa Muhimbili Madokta wa Idara mbalimbali na kuzungumza nao face to face behind closed doors na kumalizia na Manejimenti ya kuu ya Taasisi (Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi)-baada ya hapo anasepa kwenye Magogoni-kitakachofuata ni vitendo!.

Tatizo yale maigizo aliyofundishwa na ccm wakati wa kampeni anayaendeleza katika mambo yanayohitaji weledi!
 
Wengine wana "viwanda vya uongo" - Kikwete.

Huu ni ufataani tu hakuna zaidi.

Huu uzi umenikumbusha Yericko Nyerere.

Ngoja wakutafute ukawaeleze aliyokueleza haya ya kamati kuu ni nani:

"Kikwete amedaiwa kuiambia kamati kuu jana kwamba si lazima kudhalilisha uongozi uliopita ili kuonesha tu kwamba mtu anafanya kazi. Ndio maana sasa Magufuli amesitisha zile ziara za kushtukiza ili ajipange kwanza nini cha kuzungumza kuepuka kudhalilisha uongozi uliopita"

Hivi Yericko Nyerere yuko wapi?
 
Wengine wana "viwanda va uongo" - Kikwete.

Mbona huhitaji kuwa na digrii kujua kwamba Kikwete hafurahishwi na anachofanya Magufuli? Mbona body language yake inam'betray!
 
Last edited by a moderator:
FaizaFox wewe nyumba ndogo ya mzee nini? Mbona unapenda kumtetea sana?
 
Mbona huhitaji kuwa na digrii kujua kwamba Kikwete hafurahishwi na anachofanya Magufuli? Mbona body language yake inam'betray!

Unaongelea body language sasa hivi?

Hayo uliyoyatoa kikao cha CCM sasa basi?
 
Mkuu Mp Kalix2 chukua LIKE ya maandishi.
Kusema ukweli ili Tanzania ipige hatua katika nyanja ya utendaji kazi,ni vyema Raisi kwa sasa na PM atakayeteuliwa wawe ni watu wa kwenda site kwenye idara za serikali na mashirika ya umma na kukutana kwanza na management then na wawakilishi wa wafanyakazi behind closed door,then baada ya hapo kama ulivyoshauri wanarudi ofisini na kuanza kuyafanyia kazi yale waliyoyaona na kuelezwa na viongozi wa sehemu husika na wafanyakazi.
Mfano kwa pale MNH ilitakiwa akutane na madaktari,then akutane na management yote mwisho amalizie kwa kukutana na nurses,hapo angepata kujua matatizo hasa yapo upande gani na jinsi ya kuyatatua.
Naamini kwa approach hii tunayoizungumzia akiitumia,huko kwenye Halmashauri atagundua madudu mengi saana kwani kuna watu ofisi za umma wamefanya kama ofisi zao binafsi na wao ni Miungu watu kwa wafanyakazi na wananchi wanaotafuta huduma kwao.Na haya yapo pia kwenye mashirika ya umma na idar nyingine za serikali.
 
Unaongelea body language sasa hivi?

Hayo uliyoyatoa kikao cha CCM sasa basi?
Unamtishia nani we ajuza. Hakuna kikao cha cc ya kitafanyiks nisipate habari zake. Nina informer humo ndani!
 
Hivi katibu mkuu wizara ya afya lazima awe Mbando? Hawezi patikana katibu mkuu mwingine toka mikoa mingine atakayeendana na kuiva na kazi ya Magufuli bila longo longo zilizoficha hisia za kISIASA ZA U-KASKAZINI AU LOLOTE?

Hivi ilikuwa lazima aongee angesema No comment kwa mfano tatiz lingekuwa wapi? AU angesematunashukuru mheshimiwa raisi na wizara ya fedha kuwezesha matengenezo ingemsumbua nini?

Hawa ndio makatibu mizigo miezi miwili michakato,michakato Raisi ondoa huyo weka mwingine

Acha unazi wewe.. mkoa anakotoka unahusiana nini na utendaji wake?? Kwa nini kutoka kaskazini iwe dhambi? Kwa taarifa yako kaskazini ni Tanzania na wana mchango mkubwa sana kwa hii nchi ukiachilia siasa zenu za ubaguzi.
 
Unamtishia nani we ajuza. Hakuna kikao cha cc ya kitafanyiks nisipate habari zake. Nina informer humo ndani!

Sikutishi nnakutanabahisha tu, nilimtanabahisha Yericko Nyerere hakuelewa.

Natumai wewe utakuwa muelewa zaidi. Kumbuka tu kuna sheria mpya ambayo imeshaanza kutumika.
 
Last edited by a moderator:
........................................................[deleted]

Na inasemeka hili jambo halikumfurahisha Kikwete kwa sababu lilipeleka picha kwamba serkali yake ilikuwa goigoi.

Wakati yeye anasema amefanya juhudi kubwa kuiboresha Muhimbili. Na kwamba tatizo km la juzi linajulikana kwamba ni ukata na ufinyu wa bajeti ndio kikwazo.

Kikwete amedaiwa kuiambia kamati kuu jana kwamba si lazima kudhalilisha uongozi uliopita ili kuonesha tu kwamba mtu anafanya kazi. Ndio maana sasa Magufuli amesitisha zile ziara za kushtukiza ili ajipange kwanza nini cha kuzungumza kuepuka kudhalilisha uongozi uliopita.

Haya ndio madhara ya Maigizo na kulazimisha kupendwa! Ikulu kuweni makini! Mwongozeni rais vizuri!

Kuna maelezo yanakuwa ni kama komedi vile! Kama kweli hayo ndo maneno yaliyosemwa, kweli Kikwete anategemea kuendelea kusifiwa hata baada ya kuondoka ikulu? Kweli hadi anaondoka hajui ugoigoi wa utawala wake? AJABU kabisa!!!

Nahisi ni mazoea ya kupewa sifa kwa miaka mingi. sasa hiyo hali haipo na haitakuja tena. Naona hata kuitwa Dr kunapungua polepole! Baadaye itabakia majina yake halisi.
 
Magufuli ana kibarua kigumu. Atapata upinzani ndani na nje ya chama chake!
 
Back
Top Bottom