Ikulu na Wizara ya Afya lugha gongana

Ikulu na Wizara ya Afya lugha gongana

Wabongo ndiyo tupo hivihivi miaka yote,wapinzani wanaponda kila kitu(sio kukosoa) ccm nao wao wanatetea kila kitu. Halafu tunawapinzani lakini hawapendi kupigwa mambo yao hata pale wakoseapo.

Basi ndiyo hivyohivyo siasa za vyama ndiyo zimetawala na ndiyo zinazoendesha nchi.

Mie naamini vyama vingi wala si suruhu ya matatizo yetu watz, imekuwa sasa ni sehemu ya watu kutengenezea vipato huku wakifuja Kofi zetu kibao kupitia ruzuku
 
kwanza magufuli hajamdhalilisha mtu, wale wagonjwa pale chini wanahusikaje na deni la phillips? Huyu aliyekuwa anakaimu kurudishwa kazini kwake ndo iwe nongwa?

Hili deni la billioni saba kwa kutengeneza mashine mbili nadhani hawajalipwa tangu enzi ya nyerere.


mri -muhimbili ilipatikana kipindi cha kikwete na CT- KIPINDI CHA MWISHO CHA MKAPA
 
Bora umemwambia huyo, hapa jukwaani kuna kundi liko hapa kuhakikisha eti kila anachofanya Magufuli anasifiwa na usiposifia basi wewe sio mzalendo!! Nikasema sidhani kama kusifia tu ndio kumjenga tena unaweza kukuta sisi tunaomponda kwa kiwango kikubwa ndio tunamfanya awe bora maana ili kutukata ngebe inabidi afanye kweli. Nakumbuka Obama aliwahi kusema kwenye kuitumikia America atasikiliza watu wake na hasa wale wapinzani wake maana wale ndio watampa ukweli bila kujipendekeza. Ila wengi wa hawa wanaosema asifiwe wanafikia hatua ya kutishia eti yeye sio kama JK na kwamba akikashifiwa atakuwa dictator!! Akiwa na dictator kwa kufanya chini ya kiwango ndio atazidi kutufanya ile asiimia 40 ya upinzani kupanda kuwa 50+. Yeye afanye kwa ubora wake sifa zinakuja automatically na sio kwa kulazimisha.

Rais Magufuli ni mwana sayansi wa kiwango. Mwana sayansi huchukua maamuzi kwa takwimu tofauti na wana siasa ambao maneno ni mengi. Kama kweli wapinzani (hasa wewe) wana nia njema na nchi hii kwa kumjenga afanye vizuri, kosoa juhudi zake kwa takwimu. Atawaelewa na kuchukua maamuzi yaliyo sahihi (informed decision). Tofauti na hili, maneno yako ni ya udaku tu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Juzi rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza Muhimbili na kumwondoa mkurugenzi na bodi ingawa bodi ilishamaliza muda wake na mkurugenz kahamishiwa wizarani tu wala hajafukuzwa.

Ikulu ikadai Magufuli alikasirishwa sana kukuta mashine za MRI hazifanyikazi ndio maana kaisimanisha bodi,
Lakini jana kupitia Azam Tv Katibu mkuu wizara ya Afya Bw.Mbando alisema mashine haikutengenezwa kwa sababu Magufuli alisema bali ilikuwa tu kwamba akivyotenbekea pale mchakato wa kuikarabati mashine ulishakamilika.

Alisema tatizo lililokuwepo ni kwamba Phillips wanaidai serikali zaidi ya bil 7 ndio maana waligoma kuitengeneza hiyo nashine.

Sasa mchakato wa kupunguza deni ndio ulikuwa unaendelea na zilishapatikana bil3 kutoka hazina walizolipwa juzi hao Phillips ndipo wakakubali kuja kuifanyia mashine ukarabati.

Na hili linaleta maana zaidi kwa sababu wizara haiwezi kutoa bil3 ghafla tu bila kuwa zilikuwa kwenye mchakato.

Kwa hiyo hapa ikulu ilifanya usanii wa hali ya juu kuwaaminisha watanzania kwamba kulikuwa na uzembe pale muhimbili wakati uzembe ulikuwa serikalini. Serikali ilishindwa kulipa deni kwa wakati.

Na inasemeka hili jambo halikumfurahisha Kikwete kwa sababu lilipeleka picha kwamba serkali yake ilikuwa goigoi.

Wakati yeye anasema amefanya juhudi kubwa kuiboresha Muhimbili. Na kwamba tatizo km la juzi linajulikana kwamba ni ukata na ufinyu wa bajeti ndio kikwazo.

Kikwete amedaiwa kuiambia kamati kuu jana kwamba si lazima kudhalilisha uongozi uliopita ili kuonesha tu kwamba mtu anafanya kazi. Ndio maana sasa Magufuli amesitisha zile ziara za kushtukiza ili ajipange kwanza nini cha kuzungumza kuepuka kudhalilisha uongozi uliopita.

Haya ndio madhara ya Maigizo na kulazimisha kupendwa! Ikulu kuweni makini! Mwongozeni rais vizuri!
Kama kweli JK aliyasema hayo basi si muda mrefu JPM atakabidhiwa uenyekiti wa Chaama
 
Siyo rahisi sana JK kumwendesha Magufuli, kumbuka watu wamemchagua Magufuli siyo CCM ... vile vile siyo rahisi sana JK. kuzungumza hayo maana hata yeye aliyafanya hayo hayo ya kushtukiza na Mkapa hakumkanya...kumbuka JK. ni mwenyekiti lakini wazee wa chama hasa MKAPA wapo nyuma ya Magufuli na kumbuka Magufuli ndiye mwenye Jeshi, polisi na TISS hivyo JK haiwezi nakuhakikishia...jana nilimuona akiongea kinafiki na akacheka kinafiki nafiki sana, kwa wanaomjua JK. huyu bwana ni mnafiki sana, kicheko chake cha jana ni cha kinafiki na bado ana fundo kubwa moyoni mwake juu ya magufuli, maana hakuwa chaguo lake na Alitishwa na akina Mkapa kuwa Chama kinakufia mikononi mwako, na yeye akapanic ndo uchaguzi ukawa vile............
 
Hili game, hili game, hili game, game sasa tough.....hili game, hili game.........ninekumbuka mistari ya Nature.....naona SIASA zimeanza kunoga, CCM wanataka kutoana roho.
 
Juzi rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza Muhimbili na kumwondoa mkurugenzi na bodi ingawa bodi ilishamaliza muda wake na mkurugenz kahamishiwa wizarani tu wala hajafukuzwa.

Ikulu ikadai Magufuli alikasirishwa sana kukuta mashine za MRI hazifanyikazi ndio maana kaisimanisha bodi,
Lakini jana kupitia Azam Tv Katibu mkuu wizara ya Afya Bw.Mbando alisema mashine haikutengenezwa kwa sababu Magufuli alisema bali ilikuwa tu kwamba akivyotenbekea pale mchakato wa kuikarabati mashine ulishakamilika.

Alisema tatizo lililokuwepo ni kwamba Phillips wanaidai serikali zaidi ya bil 7 ndio maana waligoma kuitengeneza hiyo nashine.

Sasa mchakato wa kupunguza deni ndio ulikuwa unaendelea na zilishapatikana bil3 kutoka hazina walizolipwa juzi hao Phillips ndipo wakakubali kuja kuifanyia mashine ukarabati.

Na hili linaleta maana zaidi kwa sababu wizara haiwezi kutoa bil3 ghafla tu bila kuwa zilikuwa kwenye mchakato.

Kwa hiyo hapa ikulu ilifanya usanii wa hali ya juu kuwaaminisha watanzania kwamba kulikuwa na uzembe pale muhimbili wakati uzembe ulikuwa serikalini. Serikali ilishindwa kulipa deni kwa wakati.

Na inasemeka hili jambo halikumfurahisha Kikwete kwa sababu lilipeleka picha kwamba serkali yake ilikuwa goigoi.

Wakati yeye anasema amefanya juhudi kubwa kuiboresha Muhimbili. Na kwamba tatizo km la juzi linajulikana kwamba ni ukata na ufinyu wa bajeti ndio kikwazo.

Kikwete amedaiwa kuiambia kamati kuu jana kwamba si lazima kudhalilisha uongozi uliopita ili kuonesha tu kwamba mtu anafanya kazi. Ndio maana sasa Magufuli amesitisha zile ziara za kushtukiza ili ajipange kwanza nini cha kuzungumza kuepuka kudhalilisha uongozi uliopita.

Haya ndio madhara ya Maigizo na kulazimisha kupendwa! Ikulu kuweni makini! Mwongozeni rais vizuri!
Ulitamani kilichofanywa na Magufuli kingefanywa na Lowassa, lakini ndo basi tena. Tingatinga lishatinga Ikulu linafanya yake at the same time tunawashughulikia mamluki wenu.
 
Hii post yako inawakilisha kabisa udhaifu wa kiccm kukimbilia kwenye ukabila, huyo katibu mkuu amejibu kitaalamu wewe unataka ajibu kisiasa ili kutaka mwanasiasa apate sifa za kijinga. Si wote mandezi na ndio maana huoni watu wote wakisifia hatu za Magufuli kitu ambacho wanaccm mngependa kuona eti watu wote wanasifia. Enzi za kusifia hata maigizo zimepitwa na wakati. Atende kazi tuone weledi na sio kutafuta sifa za kijinga wakati hamna kitu.
Mkuu afadhali nicomment kwenye hii yako, maana huyo uliyemjibu nimeisoma post yake nikabaki nashangaa jinsi elimu isivyotusaidia waswahili, kwa mtindo huu hii Nchi kutoka kiuchumi ni ngumu sana, kupenda sifa tu bila kukosolewa.
 
Mijadala ya hivi haina maaana tena kwasababu kilichokuwa kimekwama kimekwamuliwa na tayari maisha yanaendelra, sisi hatutaki kujua nani alifanyaje sahivi tunaangalia watu waendelee kutibiwa kama kawaida. Tushachelewa jamani tuache majungu tufanye kazi sasa. Ni muda wa kazi
uangalie na uendelevu wake. Ikiwa deni la billion 7 na zimelipwa chini ya nusu (billion 3) maanake tatizo bado lipo! Je hili deni lilitokeaje, litaishaje na tutaendeleaje bila kujirudia? Hayo ndiyo tunatakiwa kujadili na kujulishwa
 
kuna haja ya kuwachunguza watu wenye itikadi za u-kaskazini hususani walioajiriwa serikalin hawa pia ni wapinzani rasmi wa ccm,huyo mbando amejibu kisiasa sana suala la kiutendaji inaonesha dhahiri alikuwa ananufaika na uharbifu wa mashine hzo
 
Rais Magufuli ni mwana sayansi wa kiwango. Mwana sayansi huchukua maamuzi kwa takwimu tofauti na wana siasa ambao maneno ni mengi. Kama kweli wapinzani (hasa wewe) wana nia njema na nchi hii kwa kumjenga afanye vizuri, kosoa juhudi zake kwa takwimu. Atawaelewa na kuchukua maamuzi yaliyo sahihi (informed decision). Tofauti na hili, maneno yako ni ya udaku tu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA

Watu munajua upambe mpk raha, hamtaki kabisa kusikia Rais akikosolewa, kila atakachofanya yy ndio yupo sahihi.....haya mkuu ngoja wengine tuendelee kufuatilia mchezo mpk mwisho.
 
Ndio maana unakuta marais wastaafu wanalazimisha kuendelea kulipwa na serekali mpaka watakapoaga dunia, unajua sababu ni nini? wengi ni wafujaji hivo hata wakipewa kiinua mgongo cha kuondoka jumla watashindwa kuendesha maisha yao. Sipati picha eti CT scan ilikuwa imekufa zaidi ya miezi mitatu hela hakuna lakini unanunua magari ya kuwasha wakati unaaminisha umma chama chako kitashinda kwa kishindo. Mtu kama huyo hata ukimpa bilioni moja kama kiinua mgongo akaanzishe maisha yake ni dhahiri baada ya miaka michache atageuka kuwa ombaomba.
kuna tatizo kwenye mifumo yetu ya serikali.. na ndiyo inatakiwa irekebishwe mapema iwezekananvyo
 
Juzi tu nilitukanwa sana na akina njiwa na Rungu kwenye uzi wa mgonjwa kampigia magufuli salute. Nilisema this is a very easy move for a president to do and political circus hata bint wa chekechea akiteuliwa kuwa rais anaweza tu. Nikatukanwa hoo cjui mm ni show off na profile yangu ya Copenhagen. Nikamalizia si tupo humu jf tuombe uzima.

Sina imani na magufuli and he'll terribly fail kwasababu wote ccm ni maboriti.

Let this post not distruct my focus in carrying boxes here. Nyambaff zetu!!

Mkuu, mimi naamini makomeo ni mtenda kazi haswaa ila nakuhakikishia, kwa ccm aliyomo hatafika kokote. Hizo safari zake za kushtukiza ni geresha tu, mkwere alishavaa kimasai akavamia muhimbili lakini ndio rais aliyeongoza kuwaumiza watanzania.Mpeni muda makomeo rangi yake halisi mtaiona.
 
Mkuu umenifurahisha sana kwa jicho lako kuona ndani kabisa ya maigizo haya. Kumbe Tanzania tuna watu makini wanaoweza kupambanua hali halisi na maigizo. Hongera sana . Nashauri viongozi wetu kuwaangalia waatu kama hawa, vinginevyo nchi yote itageuka kuwa ya maigizo!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Magufuli akianza kumsikiliza Mkwere atapoteza dira.Mkwere alikuwa mbovu hakuna namna lazima aonekane mbovu tu.


Upo sahihi Super Sub Steve, ni kawaida ya waswahili kutafuta visingizio, lakini ukweli hubakia ukweli siku zote, kwenye hiyo awamu usanii ulikithiri, ni kweli nobody was serious with public health services,

Tujiulize swali, Magufuli alitaka kumlipia Chacha Makenge gharama za vipimo vya MRI, yule Dr. aliyekuwa naye akasema watafanya utaratibu wenyewe kama Mhimbili ili akapimwe, je utaratibu huo ulikuwa unamsubiri Magufuli ajitolee kulipa gharama za vipimo vya Makenge? na je kitu gani kilimfanya Makenge akafanyiwe vipimo the next morning na kuanzishiwa matibabu immediately?
 
Ndio maana kumbe JK jana alikuwa anazungumzia ziara za kushtukiza kwa kejeli sio! Sasa tutauona mpambano mkubwa kati ya Serikali (JPM) na CCM kamati kuu (JK). Hapo kila mmoja ni mpenda sifa na kila mtu anachombo chake chenye mamlaka.
Kuna kila dalili kuwa kipindi hiki kilichobaki cha miaka miwili cha Mwenyekiti wa CCM kuwepo madarakani lazima kitakuwa kikwazo kwa uongozi wa Magufuli. Kuna watakao bisha lakini huo ndio ukweli na chama huwa ndicho kilichoshika hatamu.

juzi nilipost uzi humu kuwa kikwete ajiuzulu uenyekiti wa ccm watu wakaniona nina chuki binafsi,kikwete must go
 
Bil 26 za bunge lakatiba hukushangaa?

Mh kwani zilikuwa za ghafla yaani siku moja maagizo siku ya pili utekelezaji? Sema nimeanza kuhisi wa escrow wamerudisha chenji ndomana hazikuwa na kazi wakaona wampaishe Mheshimiwa.
 
Na kiukweli ukisoma body language ya Kikwete inaonesha kabisa hafurahishwi na mtindo wa Magufuli wa kumdhalilisha kwamba alikuwa mzembe! Kikwete ni mtu wa kupenda sifa. Kuonesha madhaifu yake inamkosesha raha sana!
 
Back
Top Bottom