Ikulu na Wizara ya Afya lugha gongana

Ikulu na Wizara ya Afya lugha gongana

Eti kwamba bilioni 3 zilikuwa zimekaa pale wizarani zinamsubiri Magufuli akawashtue zikatengenze mashine? Ni kweli kuna mtu anaweza kuliamini hili? Ikulu walikuwa wanatafuta upenyo wa kumpasiha magufuli wakaona hapo ndio penyewe bila kufukiria kwamba watu tuna akili timamu za kuchambua mambo!
 
uangalie na uendelevu wake. Ikiwa deni la billion 7 na zimelipwa chini ya nusu (billion 3) maanake tatizo bado lipo! Je hili deni lilitokeaje, litaishaje na tutaendeleaje bila kujirudia? Hayo ndiyo tunatakiwa kujadili na kujulishwa


Hivi unajua kuwa wale mafundi wa Phillips wanakula na ma Technician wa X-RAY/CT-Scan Tanzania Mzima? Kama hujui basi watafute Kinondoni au nenda Billicannas utapata habari ya mjini
 
Mijadala ya hivi haina maaana tena kwasababu kilichokuwa kimekwama kimekwamuliwa na tayari maisha yanaendelra, sisi hatutaki kujua nani alifanyaje sahivi tunaangalia watu waendelee kutibiwa kama kawaida. Tushachelewa jamani tuache majungu tufanye kazi sasa. Ni muda wa kazi
Lakini pia ni vyema tukamtambua aliyekuwa akikwamisha maendeleo,ni ujinga kusema tu eti kwa kuwa watu jana na leo wametibiwa basi hakuna haja ya kumjua mhujumu wetu na kumshughulikia ili asirudie tena kuhujumu,kumbuka hii si mara ya kwanza kwa mashine hiyo kuharibika na kukaa muda mrefu bila kutengenezwa.
2nd June 2012 Email Print Comments

Kipimo cha CT Scan

Scan Muhimbili yaharibika BY ROMANA MALLYA

Kipimo cha CT Scan Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kimeharibika kwa muda wa miezi sita sasa hali inayosababisha usumbufu kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo na kuandikiwa kipimo hicho.Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka hospitalini hapo, kimesema licha ya uongozi wa hospitali kuwa na taarifa hizo lakini hakuna juhudi zilizofanyika.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa, ukosefu wa kipimo hicho umesababisha wagonjwa kupata huduma hiyo nje ya hospitali na kuleta usumbufu.

"Kinachoshangaza wiki iliyopita hospitali iliandaa bonanza la michezo linalogharimu kiasi cha milioni 15/-lililoshirikisha Kurugenzi mbalimbali lakini mambo ya muhimu kama haya imeshindwa kuyashughulikia," kimeeleza chanzo hicho na kuongeza:

"Kifaa hicho kimeharibika kabla ya madaktari kugoma, tulifikiri kitashughulikiwa kwa wakati ili wagonjwa wanaofika hapa wapate huduma ndani ya hospitali yao ya umma lakini matokeo yake daktari anaandika vipimo kisha mgonjwa anaambiwa huduma hiyo haipo na kulazimika kwenda nje ya hospitali, hii ni aibu," chanzo hicho kimebainisha.

Kadhalika, kimeeleza kuwa, mara kwa mara mashine za hapo zimekuwa zikilalamikiwa kuharibika na kusababisha usumbufu kwa wagonjwa ambao wamekuwa wakiitegemea hospitali hiyo kama mkombozi wa maradhi yanayowasumbua.

Afisa Uhusiano wa hospitalini hapo, Aminiel Aligaesha, alipoulizwa kuhusiana na tatizo hilo kwa njia ya simu alisema kuwa yupo kwenye mkutano.

Januari mwaka huu gazeti hili liliandika habari kuhusu kuwepo kwa baadhi ya vipimo vikubwa ndani ya hospitali hiyo kushindwa kutolewa kutokana na vifaa vyake kuharibika huku baadhi ya dawa za kufanyia vipimo kutokuwepo.

Katika taarifa hiyo baadhi ya vipimo vilivyokuwa havifanyi kazi ni vile vya magonjwa yahusuyo upimaji wa damu kama figo, ini sukari, mafuta (CCP) na mengine havifanyiki kwa sababu dawa za kufanyia zimeisha.

Pia taarifa hiyo ilieleza kuwa, karatasi (film) za vipimo vya MRI na CT Scan zilikuwa hazipo.

Kadhalika mapema mwezi uliopita NIPASHE ilipata taarifa kuwa mashine nyingine ambayo kazi yake ni kukata vinyama kwa ajili ya kupima ugonjwa wa kansa kwa mgonjwa pia imeharibika.
 
Na kwa nini mkurugenzi wa muhimbili hakuwajibishwa? Zaidi sana alihamishwa, .

Swali linguine kwa nini katibu mkuu wa wizara hakuwajibishwa kwa huo uzembe kama kweli Magufuli "alichukizwa" sana? Jamani achene usanii fanyeni kazi kwa uhalisia uliopo! Si lazima kuigiza!
 
Pesa ipo kwenye mchakato miezi 2?!! Huyo pimbi nn? Magufuli huyo wasiongopee watu na huyo Kikwete ayo aliyasemea wapi?

Usipate kipindupindu cha mdomo kama hujui kinachoendelea.mbona waalimu wanaidai serikali madeni ya miaka na hawajalipwa..wee tambua serikali yetu ni stress tupu.kulipa madeni hawataki ila kuagiza mashangingi na kusafiri ndo ilikuwa kazi yao.nitakushangaa sana kama unaona ajabu hela kuproccesiwa miezi miwili wakati hiyo ni michache sana kwa Tanzania hii.
 
Ni wazi kwamba mh raisi atakapo katkata nyaya zote za uchotaji wa mali za umma atakuja kupata upinzani nabuadui mkubwa kwa hao waliozoea kula mali za umma.
Tunamuomba mh raisi aendlee na kasi hiyo hiyo kwani yeye ndio kiongozi wa nchi sasa.
Nina uhakika wanao leta hoja zao za kumpinga raisi ndio hao wa nyonyaji wa mali za uma ha walala hoi.
Mh raisi kaza mkono wako. Wanao pata taabu na walio pata taabu ni wengi kuliko hao mafisadi

Ongea kwa uwazi sio kimafumbo maana wanao haribu mali za umma ni wana ccm na wala hakuna ubishi na watakao mkwamisha rais wetu wamo ndani ya ccm wapinzani hawana mwanya wa kuiba hivyo basi rais anachotakiwa ni kukata mirija yote bila kujali uana chama wao ndani ya ccm
 
Mungu amsaidie mh Kikwete apate hekima kuwa muda wake wakuongoza hili taifa kama rais ulishapita. Ambacho hakufanikiwa kukifanya miaka kumi aliyokuwa madarakani hata weza kukifanya ndani ya hii wiki moja aliyo nje ya maadaraka, atulie aendeshe maisha yake.

Maana tukienda kwa staili hii hatutafika, labda ni mkumbushe wakati tu alipochukua madaraja Yeye 2005,Mkapa alikuwa akipita huko mabarabarani akizomewa wakati mwingine ilibidi afiche uso wake kwa kuzuga kusoma gazeti. so hii isimpe taabu sana akajikuta ana ingia kushindana na rais aliye madarakani. Ni ushauri tu.
Yeye mwenyewe alikuwa akifurahia Mkapa kudhalilika sasa kwa wengine Halleluya kwake imekuwa nongwa?
 
ila patamu hapa. je magufuli atafanyaje sasa? Ataendelea kufanya kazi kwa kuonesha uongozi uliopita ulikuwa goigoi au atafanyaje ili awaridhishe watanzania kwamba kweli analeta mabadiliko na hapohapo asiwaudhi uongozi wa serikali iliyopita? Ama kweli magu yupo njia panda!
 
Swali linguine kwa nini katibu mkuu wa wizara hakuwajibishwa kwa huo uzembe kama kweli Magufuli "alichukizwa" sana? Jamani achene usanii fanyeni kazi kwa uhalisia uliopo! Si lazima kuigiza!

Mkuu unakumbuka mbwembwe za baba riz alipokabidhiwa ofisi?Matokeo yake ameishi angani kama mbayuwayu kwa miaka mitano. Ccm ni ileile na makomeo ni ccm, tusitegemee jipya.
 
Eti kwamba bilioni 3 zilikuwa zimekaa pale wizarani zinamsubiri Magufuli akawashtue zikatengenze mashine? Ni kweli kuna mtu anaweza kuliamini hili? Ikulu walikuwa wanatafuta upenyo wa kumpasiha magufuli wakaona hapo ndio penyewe bila kufukiria kwamba watu tuna akili timamu za kuchambua mambo!

Kwani wakati mzee Lowassa anawaambia hii nchi ina pesa nyingi sana hamkuelewa??!!
Ni suala la vipaumbele na uamuzi wa dhati. . . .

Kwani chai mawizarani huwa ni shilingi ngapi, ukiwaambia hazina nataka pesa sasa hivi ukiwa Rais wao wanajua wapi sio muhimu watatoa tu. . . .

Tuendelee kuangalia hii live series
 
Ndio maana kumbe JK jana alikuwa anazungumzia ziara za kushtukiza kwa kejeli sio! Sasa tutauona mpambano mkubwa kati ya Serikali (JPM) na CCM kamati kuu (JK). Hapo kila mmoja ni mpenda sifa na kila mtu anachombo chake chenye mamlaka.
Kuna kila dalili kuwa kipindi hiki kilichobaki cha miaka miwili cha Mwenyekiti wa CCM kuwepo madarakani lazima kitakuwa kikwazo kwa uongozi wa Magufuli. Kuna watakao bisha lakini huo ndio ukweli na chama huwa ndicho kilichoshika hatamu.
Rais ni Rais tu hakuna cha chama wala mpambano!Hakuna mtu anayeweza kugombana na dola,Rais ana kila kitu
 
Tukitegemea kuwa JPM ataleta mabadiliko ambayo ndiyo kiu ya kila mtanzania tutakuwa tumeweka imani zetu mahali pasipo salama.
Hatukatai Kama Magufuli ni mtendaji mzuri ila amezungukwa na watendaji wabovu na Chama kilekile kilichowaumiza watanzania kwa miaka zaidi ya 50 sasa. Kubomoa mfumo ulioota mizizi ndani ya CCM na kuirudisha ile CCM ya wafanyakazi na wakulima ni ngumu zaidi ya kuiangusha mlima kilimanjaro. Tusubiri tuone, ila tujue hata dhahabu ukiitupa ndani ya dambo haitaitwa dhahabu tena bali uchafu!!
 
We pimbi kweli mchakato wa malipo miezi 2. Tafuta nyumbu wenzio hapa tumestuka
 

Hivi unajua kuwa wale mafundi wa Phillips wanakula na ma Technician wa X-RAY/CT-Scan Tanzania Mzima? Kama hujui basi watafute Kinondoni au nenda Billicannas utapata habari ya mjini
Nani aliwateua hao Phillips? Jiridhishe kwa kufanya uchunguzi wa taarifa sahihi siyo kuhemka kwa maneno ya mitaani. Technician wapi waloajiriwa na Phillips au walioajiriwa na Muhimbili/Wizara ya Afya?
 
kuna political victims hapo ,it seems MRI na CT SCAN ziliharibika longtime ago na uongozi wa MNH ulitoa taarifa wakulaumiwa ni "Mdaiwa"
 
kuna political victims hapo ,it seems MRI na CT SCAN ziliharibika longtime ago na uongozi wa MNH ulitoa taarifa wakulaumiwa ni "Mdaiwa"

Hasa ndilo hilo. Mdaiwa anarushwa mpira kwa wadogo. Yaani kama baba anayeharibu ili kuficha aibu anamsingizia mtoto! Mashine zinapoharibika serikali (wizara) inapewa taarifa siku hiyohiyo. sasa wanapotaka kutuaminisha eti uzembe u[po muhimbili na sio kwa serikali wajue watanzania siku hizi tumeelimika!
 
Je, mbona magufuli halutoa ufumbuzi wa tatizo la kulalal chini? nalo hilo linasababishwa na watendaji wa muhimbili?
 
Kwani wakati mzee Lowassa anawaambia hii nchi ina pesa nyingi sana hamkuelewa??!!
Ni suala la vipaumbele na uamuzi wa dhati. . . .

Kwani chai mawizarani huwa ni shilingi ngapi, ukiwaambia hazina nataka pesa sasa hivi ukiwa Rais wao wanajua wapi sio muhimu watatoa tu. . . .

Tuendelee kuangalia hii live series

hahaha umeongea pointi kubwa. Wanajua vzuri hela zilizpo kama kelele hazikupigwa hazitoki! Pesa ipo lakini inaenda kwenye matumizi yasiyo ya ulazima! Ni kweli baba Lowasa na sumaye walifichua hii siri!
 
Je, mbona magufuli halutoa ufumbuzi wa tatizo la kulalal chini? nalo hilo linasababishwa na watendaji wa muhimbili?

Ufumbuzi kuna wa papo kwa papo, muda mfupi ujao na yatakayosubiri. . . Sasa kaka unataka ajenge wodi au awa discharge??!!
 
Nadhani dhamira ya raisi kama ni ya dhati nami naamini hivyo ataweza kufanya makubwa na kuwafurahisha wengi kuliko hao wachache ndani ya chama ambao wanajiona kuwa wana hati miliki ya nchi yetu.Akitekeleza ahadi zake japo robo atakuwa amejipambanua na kundi ndani ya chama mabezo na kuiombea dua mbaya serikali sidhani kama ni sahihi penye kukosoa tukosoe kwa nidhamu pia penye pongezi zitoke pia tukubali nchi ipo pabaya suala la uwajibikaji umekuwa msamiati mgumu.
 
Back
Top Bottom