Ikulu na Wizara ya Afya lugha gongana

Ikulu na Wizara ya Afya lugha gongana

mcfm40

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,452
Reaction score
3,152
Juzi rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza Muhimbili na kumwondoa mkurugenzi na bodi ingawa bodi ilishamaliza muda wake na mkurugenz kahamishiwa wizarani tu wala hajafukuzwa.

Ikulu ikadai Magufuli alikasirishwa sana kukuta mashine za MRI hazifanyikazi ndio maana kaisimanisha bodi,
Lakini jana kupitia Azam Tv Katibu mkuu wizara ya Afya Bw.Mbando alisema mashine haikutengenezwa kwa sababu Magufuli alisema bali ilikuwa tu kwamba akivyotenbekea pale mchakato wa kuikarabati mashine ulishakamilika.

Alisema tatizo lililokuwepo ni kwamba Phillips wanaidai serikali zaidi ya bil 7 ndio maana waligoma kuitengeneza hiyo nashine.

Sasa mchakato wa kupunguza deni ndio ulikuwa unaendelea na zilishapatikana bil3 kutoka hazina walizolipwa juzi hao Phillips ndipo wakakubali kuja kuifanyia mashine ukarabati.

Na hili linaleta maana zaidi kwa sababu wizara haiwezi kutoa bil3 ghafla tu bila kuwa zilikuwa kwenye mchakato.

Kwa hiyo hapa ikulu ilifanya usanii wa hali ya juu kuwaaminisha watanzania kwamba kulikuwa na uzembe pale muhimbili wakati uzembe ulikuwa serikalini. Serikali ilishindwa kulipa deni kwa wakati.

Na inasemeka hili jambo halikumfurahisha Kikwete kwa sababu lilipeleka picha kwamba serkali yake ilikuwa goigoi.

Wakati yeye anasema amefanya juhudi kubwa kuiboresha Muhimbili. Na kwamba tatizo km la juzi linajulikana kwamba ni ukata na ufinyu wa bajeti ndio kikwazo.

Kikwete amedaiwa kuiambia kamati kuu jana kwamba si lazima kudhalilisha uongozi uliopita ili kuonesha tu kwamba mtu anafanya kazi. Ndio maana sasa Magufuli amesitisha zile ziara za kushtukiza ili ajipange kwanza nini cha kuzungumza kuepuka kudhalilisha uongozi uliopita.

Haya ndio madhara ya Maigizo na kulazimisha kupendwa! Ikulu kuweni makini! Mwongozeni rais vizuri!
 
Hapa kazi tu.tuache kwanza tuko tunajenga nchi. baadaye maana Haijulikani saa wala siku atakayokuja
 
Magufuli sio mtu wa kuendeshwa kama unavyodhani..yaani hapa ndio kwanza inafuka moshi..subiri moto wake..
 
Pesa ipo kwenye mchakato miezi 2?!! Huyo pimbi nn? Magufuli huyo wasiongopee watu na huyo Kikwete ayo aliyasemea wapi?
 
Magufuli akianza kumsikiliza Mkwere atapoteza dira.Mkwere alikuwa mbovu hakuna namna lazima aonekane mbovu tu.
 
Naunganisha dot ya JMP kwenda hazina na kesho yake Muhimbili.
 
Juzi tu nilitukanwa sana na akina njiwa na Rungu kwenye uzi wa mgonjwa kampigia magufuli salute. Nilisema this is a very easy move for a president to do and political circus hata bint wa chekechea akiteuliwa kuwa rais anaweza tu. Nikatukanwa hoo cjui mm ni show off na profile yangu ya Copenhagen. Nikamalizia si tupo humu jf tuombe uzima.

Sina imani na magufuli and he'll terribly fail kwasababu wote ccm ni maboriti.

Let this post not distruct my focus in carrying boxes here. Nyambaff zetu!!
 
Tanzania bil.3 ghafla? hata mi nilishangaa,Pengine ni rais bora zaidi ya waliopita but si kwa hili.
 
Mimi namnukuu mzee jk alisema siku moja kwamba huyu mama
saada mkuya kwa madenu serikali inavyodaiwa angekuwa biashara au mtu binafsi asingetoka ndani kwa kudaiwa that means jk anajuwa madeni ni mengi na makubwa sana na hawawezi lipa
 
Mungu amsaidie mh Kikwete apate hekima kuwa muda wake wakuongoza hili taifa kama rais ulishapita. Ambacho hakufanikiwa kukifanya miaka kumi aliyokuwa madarakani hata weza kukifanya ndani ya hii wiki moja aliyo nje ya maadaraka, atulie aendeshe maisha yake.

Maana tukienda kwa staili hii hatutafika, labda ni mkumbushe wakati tu alipochukua madaraja Yeye 2005,Mkapa alikuwa akipita huko mabarabarani akizomewa wakati mwingine ilibidi afiche uso wake kwa kuzuga kusoma gazeti. so hii isimpe taabu sana akajikuta ana ingia kushindana na rais aliye madarakani. Ni ushauri tu.
 
Ndio maana kumbe JK jana alikuwa anazungumzia ziara za kushtukiza kwa kejeli sio! Sasa tutauona mpambano mkubwa kati ya Serikali (JPM) na CCM kamati kuu (JK). Hapo kila mmoja ni mpenda sifa na kila mtu anachombo chake chenye mamlaka.
Kuna kila dalili kuwa kipindi hiki kilichobaki cha miaka miwili cha Mwenyekiti wa CCM kuwepo madarakani lazima kitakuwa kikwazo kwa uongozi wa Magufuli. Kuna watakao bisha lakini huo ndio ukweli na chama huwa ndicho kilichoshika hatamu.
 
Juzi rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza Muhimbili na kumwondoa mkurugenzi na bodi ingawa bodi ilishamaliza muda wake na mkurugenz kahamishiwa wizarani tu wala hajafukuzwa.

Ikulu ikadai Magufuli alikasirishwa sana kukuta mashine za MRI hazifanyikazi ndio maana kaisimanisha bodi,
Lakini jana kupitia Azam Tv Katibu mkuu wizara ya Afya Bw.Mbando alisema mashine haikutengenezwa kwa sababu Magufuli alisema bali ilikuwa tu kwamba akivyotenbekea pale mchakato wa kuikarabati mashine ulishakamilika.

Alisema tatizo lililokuwepo ni kwamba Phillips wanaidai serikali zaidi ya bil 7 ndio maana waligoma kuitengeneza hiyo nashine.

Sasa mchakato wa kupunguza deni ndio ulikuwa unaendelea na zilishapatikana bil3 kutoka hazina walizolipwa juzi hao Phillips ndipo wakakubali kuja kuifanyia mashine ukarabati.

Na hili linaleta maana zaidi kwa sababu wizara haiwezi kutoa bil3 ghafla tu bila kuwa zilikuwa kwenye mchakato.

Kwa hiyo hapa ikulu ilifanya usanii wa hali ya juu kuwaaminisha watanzania kwamba kulikuwa na uzembe pale muhimbili wakati uzembe ulikuwa serikalini. Serikali ilishindwa kulipa deni kwa wakati.

Na inasemeka hili jambo halikumfurahisha Kikwete kwa sababu lilipeleka picha kwamba serkali yake ilikuwa goigoi.

Wakati yeye anasema amefanya juhudi kubwa kuiboresha Muhimbili. Na kwamba tatizo km la juzi linajulikana kwamba ni ukata na ufinyu wa bajeti ndio kikwazo.

Kikwete amedaiwa kuiambia kamati kuu jana kwamba si lazima kudhalilisha uongozi uliopita ili kuonesha tu kwamba mtu anafanya kazi. Ndio maana sasa Magufuli amesitisha zile ziara za kushtukiza ili ajipange kwanza nini cha kuzungumza kuepuka kudhalilisha uongozi uliopita.

Haya ndio madhara ya Maigizo na kulazimisha kupendwa! Ikulu kuweni makini! Mwongozeni rais vizuri!

Amka kumeshakucha naona unaota bado
 
Kwani JK anakabidhi lini ili naye apumzike jamani? Maana magufuri anaweza pata shida kuongoza
 
Back
Top Bottom