Ikulu na Wizara ya Afya lugha gongana

Ikulu na Wizara ya Afya lugha gongana

Ndio maana kumbe JK jana alikuwa anazungumzia ziara za kushtukiza kwa kejeli sio! Sasa tutauona mpambano mkubwa kati ya Serikali (JPM) na CCM kamati kuu (JK). Hapo kila mmoja ni mpenda sifa na kila mtu anachombo chake chenye mamlaka.
Kuna kila dalili kuwa kipindi hiki kilichobaki cha miaka miwili cha Mwenyekiti wa CCM kuwepo madarakani lazima kitakuwa kikwazo kwa uongozi wa Magufuli. Kuna watakao bisha lakini huo ndio ukweli na chama huwa ndicho kilichoshika hatamu.

Bado miaka miwili? Si walisema Rais ndo mwenyekiti wa chama pia?
 
Atulie tu mzee muda umepita vitabu vimefungwa sasa zama mpya kitabu kipya. . .Mdau mmoja kasema hapo juu Mungu ampe busara ya kukubali changamoto zitazojitokeza katika uendeshaji wa serikali hii

Kazi ya kujenga Taifa lazima wengine waumie, nyundo zivunjike, makoleo yakatike. . . .
 
Mm hapa nina hoja ya ulakini kidogo.si kwel kikwete kaumia,ikumbukwe kuwa hata kikwete pia alikuwa anafanya hizi ziara.

Lakin kikubwa ni kwamba tunachotaka kuona sisi ni matokeo ya utendaji,na ikumbukwe kuwa ni uongozi mbili tofauti na kila uongozi una strategy zake.kama taasisi mapungufu ni lazima kwaiyo hupaswi kuyalea yakaendelea kuwa mapungufu kisa ukiboresha utawakwaza watu.w real need improvement and this is possible with Magufuli
 
Yaacheni yatawale tawaleni. Kwani magufuli hakuwa kwenye baraza la mawazir la dhaifu? Kwani hajui kinachodndelea. Mnawadharau sana watanzania.

Yote ni maboriti na hayawezi kutoa kibanzi kwenye...

Tawaleni! Tawaleni! Tawaleni! Hadi mvimbiwe. Hamna huruma mnakomba na kusafisha hela ya watanzania kwenye hazina . Nyinyi ni binadam wa aina gani hamna utu
 
Juzi rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza Muhimbili na kumwondoa mkurugenzi na bodi ingawa bodi ilishamaliza muda wake na mkurugenz kahamishiwa wizarani tu wala hajafukuzwa.

Ikulu ikadai Magufuli alikasirishwa sana kukuta mashine za MRI hazifanyikazi ndio maana kaisimanisha bodi,
Lakini jana kupitia Azam Tv Katibu mkuu wizara ya Afya Bw.Mbando alisema mashine haikutengenezwa kwa sababu Magufuli alisema bali ilikuwa tu kwamba akivyotenbekea pale mchakato wa kuikarabati mashine ulishakamilika.

Alisema tatizo lililokuwepo ni kwamba Phillips wanaidai serikali zaidi ya bil 7 ndio maana waligoma kuitengeneza hiyo nashine.

Sasa mchakato wa kupunguza deni ndio ulikuwa unaendelea na zilishapatikana bil3 kutoka hazina walizolipwa juzi hao Phillips ndipo wakakubali kuja kuifanyia mashine ukarabati.

Na hili linaleta maana zaidi kwa sababu wizara haiwezi kutoa bil3 ghafla tu bila kuwa zilikuwa kwenye mchakato.

Kwa hiyo hapa ikulu ilifanya usanii wa hali ya juu kuwaaminisha watanzania kwamba kulikuwa na uzembe pale muhimbili wakati uzembe ulikuwa serikalini. Serikali ilishindwa kulipa deni kwa wakati.

Na inasemeka hili jambo halikumfurahisha Kikwete kwa sababu lilipeleka picha kwamba serkali yake ilikuwa goigoi.

Wakati yeye anasema amefanya juhudi kubwa kuiboresha Muhimbili. Na kwamba tatizo km la juzi linajulikana kwamba ni ukata na ufinyu wa bajeti ndio kikwazo.

Kikwete amedaiwa kuiambia kamati kuu jana kwamba si lazima kudhalilisha uongozi uliopita ili kuonesha tu kwamba mtu anafanya kazi. Ndio maana sasa Magufuli amesitisha zile ziara za kushtukiza ili ajipange kwanza nini cha kuzungumza kuepuka kudhalilisha uongozi uliopita.

Haya ndio madhara ya Maigizo na kulazimisha kupendwa! Ikulu kuweni makini! Mwongozeni rais vizuri!

Mijadala ya hivi haina maaana tena kwasababu kilichokuwa kimekwama kimekwamuliwa na tayari maisha yanaendelra, sisi hatutaki kujua nani alifanyaje sahivi tunaangalia watu waendelee kutibiwa kama kawaida. Tushachelewa jamani tuache majungu tufanye kazi sasa. Ni muda wa kazi
 
Pole kaka, umeandika kwa uchungu sana, pole ndugu yangu
 
Billion tatu kwa serikali ni kitu gani?
Mkakati wa miezi kumi na mbili kupunguza deni?

Kama hivyo ndivyo, tutaeleza vipi hela ya bodi ya mikopo? Nayo ilikuwa mikakati wakati walisema dhahiri hakuna pesa?

Magufuli ana kazi ya ziada. Lazima aondoe watu wa Kikwete ili afanikiwe. Ni kazi ngumu sana maana alikuwa bado anateua watu wakati muda wake umeisha. Mkapa hakuwahi kufanya hayo.

Obviously, Magufuli hawezi kuondoa uzembe bila Kuonyesha udhaifu mkubwa wa Kikwete. Ndiyo maana aliitwa dhaifu.
 
halafu kuayazungusha huku mjini bila sababu gharama zote hizo zinatosha kujenga hospital nyingine

Ndio maana unakuta marais wastaafu wanalazimisha kuendelea kulipwa na serekali mpaka watakapoaga dunia, unajua sababu ni nini? wengi ni wafujaji hivo hata wakipewa kiinua mgongo cha kuondoka jumla watashindwa kuendesha maisha yao. Sipati picha eti CT scan ilikuwa imekufa zaidi ya miezi mitatu hela hakuna lakini unanunua magari ya kuwasha wakati unaaminisha umma chama chako kitashinda kwa kishindo. Mtu kama huyo hata ukimpa bilioni moja kama kiinua mgongo akaanzishe maisha yake ni dhahiri baada ya miaka michache atageuka kuwa ombaomba.
 
Juzi rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza Muhimbili na kumwondoa mkurugenzi na bodi ingawa bodi ilishamaliza muda wake na mkurugenz kahamishiwa wizarani tu wala hajafukuzwa.

Ikulu ikadai Magufuli alikasirishwa sana kukuta mashine za MRI hazifanyikazi ndio maana kaisimanisha bodi,
Lakini jana kupitia Azam Tv Katibu mkuu wizara ya Afya Bw.Mbando alisema mashine haikutengenezwa kwa sababu Magufuli alisema bali ilikuwa tu kwamba akivyotenbekea pale mchakato wa kuikarabati mashine ulishakamilika.

Alisema tatizo lililokuwepo ni kwamba Phillips wanaidai serikali zaidi ya bil 7 ndio maana waligoma kuitengeneza hiyo nashine.

Sasa mchakato wa kupunguza deni ndio ulikuwa unaendelea na zilishapatikana bil3 kutoka hazina walizolipwa juzi hao Phillips ndipo wakakubali kuja kuifanyia mashine ukarabati.

Na hili linaleta maana zaidi kwa sababu wizara haiwezi kutoa bil3 ghafla tu bila kuwa zilikuwa kwenye mchakato.

Kwa hiyo hapa ikulu ilifanya usanii wa hali ya juu kuwaaminisha watanzania kwamba kulikuwa na uzembe pale muhimbili wakati uzembe ulikuwa serikalini. Serikali ilishindwa kulipa deni kwa wakati.

Na inasemeka hili jambo halikumfurahisha Kikwete kwa sababu lilipeleka picha kwamba serkali yake ilikuwa goigoi.

Wakati yeye anasema amefanya juhudi kubwa kuiboresha Muhimbili. Na kwamba tatizo km la juzi linajulikana kwamba ni ukata na ufinyu wa bajeti ndio kikwazo.

Kikwete amedaiwa kuiambia kamati kuu jana kwamba si lazima kudhalilisha uongozi uliopita ili kuonesha tu kwamba mtu anafanya kazi. Ndio maana sasa Magufuli amesitisha zile ziara za kushtukiza ili ajipange kwanza nini cha kuzungumza kuepuka kudhalilisha uongozi uliopita.

Haya ndio madhara ya Maigizo na kulazimisha kupendwa! Ikulu kuweni makini! Mwongozeni rais vizuri!

Hii kitu ndio maana nchi haisongi mbele. Na kama kuna kitu JPM atakosea ni kuwa royal kwa JK. Ni kweli kwamba kulikuwa na uzembe. Ni kweli kwamba wagonjwa hawapati tiba kwa wakati wengine wanakufa vifo vya uzembe wa serikali. Wagonjwa wako chini. Machine haifanyi kazi kwa deni la bil 7? Ndio useme ni ufinyu wa budget wakati kila siku uko angani kama popo kwa safari zaidi ya 400? This must be a joke!
Rais akiwa mwoga kwa watu wasio na madaraka basi hatafanya kitu. Lazima ajiamini kuwa hii sasa ni zamu yake. Vinginevyo jina tinga tinga halina maana kama nalo linakwama kwenye tope.
Tuache utani, tuache woga, awamu ya nne kuna maeneo imeboronga sana. Elimu sasa kuna division 5. Afya ndio hivyo, na hapo ni muhimbili, sijui huko ileje hali ikoje, uchumi maisha magumu kwa watu wa chini, dola moja zaidi ya sh. 2000, viwanda vyote dead. Hivi inahitaji degree kujua kuwa JPM ana kazi kubwa na anahitaji uhuru kuamua?
Ukistaafu kaa pembeni, muda wako umeisha.
 
Mijadala ya hivi haina maaana tena kwasababu kilichokuwa kimekwama kimekwamuliwa na tayari maisha yanaendelra, sisi hatutaki kujua nani alifanyaje sahivi tunaangalia watu waendelee kutibiwa kama kawaida. Tushachelewa jamani tuache majungu tufanye kazi sasa. Ni muda wa kazi
Huwezi zuia analysis ya matukio yaani hata ukijikwaa mbele ya kijiwe lazima watu waongelee hilo. Acha wapiga kura wajadili sababu viongozi wakijua kuwa wanaangaliwa hadi na sisimizi wapo watakaobadili nyendo na utendaji wao. . .

Mijadala iendelee bila kashfa, matusi wala kejeli
 
natamani tusogeze siku mbele halafu turudi nyuma tuone! maana mambo ya uraisi yana .....nyingi, kila ajae anataka awe bora kuliko aliepita, ndio lengo, upite pale aliposhindwa mwingine...
 
Yaacheni yatawale tawaleni. Kwani magufuli hakuwa kwenye baraza la mawazir la dhaifu? Kwani hajui kinachodndelea. Mnawadharau sana watanzania.

Yote ni maboriti na hayawezi kutoa kibanzi kwenye...

Tawaleni! Tawaleni! Tawaleni! Hadi mvimbiwe. Hamna huruma mnakomba na kusafisha hela ya watanzania kwenye hazina . Nyinyi ni binadam wa aina gani hamna utu

Halafu bora wangetawala basi tuone ubunifu ama maendeleo ya kweli, bali utashangaa chama kinalazimisha kuongoza lakini wakiwa madarakani hata toothpick wanaagiza nje!! Ukisikia ahadi za viwanda unajua kumekucha lakini wapi, ukitokea uchaguzi unaona ni mbinu tu na jeshi linatumika kuhakikisha wanashinda na sio kwa kukubalika kwa chama chao.
 
Ndio maana kumbe JK jana alikuwa anazungumzia ziara za kushtukiza kwa kejeli sio! Sasa tutauona mpambano mkubwa kati ya Serikali (JPM) na CCM kamati kuu (JK). Hapo kila mmoja ni mpenda sifa na kila mtu anachombo chake chenye mamlaka.
Kuna kila dalili kuwa kipindi hiki kilichobaki cha miaka miwili cha Mwenyekiti wa CCM kuwepo madarakani lazima kitakuwa kikwazo kwa uongozi wa Magufuli. Kuna watakao bisha lakini huo ndio ukweli na chama huwa ndicho kilichoshika hatamu.

Hata me nimeliona jana na hata JPM naye kaliona ndo maana akawa anamjibu kwa kejeli
Je ataendelea kutembelea ofisi za umma kwa kushtukiza?
 
Lakini jana kupitia Azam Tv Katibu mkuu wizara ya Afya Bw.Mbando alisema mashine haikutengenezwa kwa sababu Magufuli alisema bali ilikuwa tu kwamba akivyotenbekea pale mchakato wa kuikarabati mashine ulishakamilika.

Hivi katibu mkuu wizara ya afya lazima awe Mbando? Hawezi patikana katibu mkuu mwingine toka mikoa mingine atakayeendana na kuiva na kazi ya Magufuli bila longo longo zilizoficha hisia za kISIASA ZA U-KASKAZINI AU LOLOTE?

Hivi ilikuwa lazima aongee angesema No comment kwa mfano tatiz lingekuwa wapi? AU angesematunashukuru mheshimiwa raisi na wizara ya fedha kuwezesha matengenezo ingemsumbua nini?

Hawa ndio makatibu mizigo miezi miwili michakato,michakato Raisi ondoa huyo weka mwingine
 
'Mchakato' neno la hovyo sana.

Watu wanakufa halafu nyie mnaleta mambo ya michakato?
 
Back
Top Bottom