KURUGENZI ya Mawasiliano Ikulu imeelezea kukerwa kwake na hatua ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kumtaja rais Jakaya Kikwete kuwa alihusika katika uzembe uliosababisha taifa kutakiwa kuilipa kampuni ya Dowans sh bilioni 185 kama fidia.
Taarifa kali ya Ikulu iliyobeba ujumbe wenye maneno ya kebehi na ya mitaani ya kumwita Dk. Slaa mtu ‘aliyechanganyikiwa' na ‘mzabinazabina' ilisainiwa na Salvatory Rweyemamu ambaye kabla ya kwenda Ikulu alikuwa mmoja wa wahariri watendaji aliyekuwa akiheshimika kwa kutumia lugha fasaha na ya staha.
Rweyemamu katika taarifa yake hiyo iliyoonyesha waziwazi kuandikwa na mtu mwenye hasira, chuki na dharau ama kwa Dk. Slaa, CHADEMA na Tanzania Daima alikwenda mbele na kumwita kiongozi huyo wa kisiasa kuwa ni mtu hatari.
JK hawezi kuukwepa ukweli kuwa ana masilahi mazito ndani ya DOWANS.......na huu hapa ni ushahidi:-
a) Uteuzi wa Dr. Idrissa Rashid kuiongoza Tanesco ulijaa mizengwe kibao..............Dr. Rashid mwenyewe alikiri kuwa pamoja na kuwa nafasi hiyo ilitangazwa magazeti yeye hakuiomba ila JK alimwomba amsaidie kwenye nafasi hiyo...........
Hivyo pamoja na sheria ya Tanesco kuweka wazi kuwa Mtendaji Mkuu wa Tanesco atateuliwa na Bodi, JK aliingilia Bodi kinyume na sheria pale alipombandika swahiba wake pale Tanesco..........................Swali la kujiuliza JK alikuwa anatetea masilahi ya nani kwa kuiingilia Bodi ya Tanesco?
b) Kwa vile Dr. Rashid hakuwa ameteuliwa na Bodi ya Tanesco hivyo na yeye hakuona sababu ya kuishirikisha Bodi tajwa katika utoaji wa zabuni ya uzalishaji wa umeme kwa Richmond na hata zabuni hiyo haikupitishwa kwa Bodi ya zabuni na matokeo yake kampuni kivuli ikapewa kazi hiyo..........Kulingana na rekodi zilizopo Brella, Richmond haijawahi kusajiliwa hapa nchini na hivyoufanyaji wake wa kazi ulikuwa ni batili na haikupaswa kupewa zabuni tajwa............Haya ni makosa ya kijinai yaani
"criminal negligence" na JK anashindwa nini kumkabidhi swahiba wake Takukuru? Hapa inaonyesha kabisa hoja za Dr. Hosea kwa Wikileaks ni za kweli ya kuwa JK ndicho kikwazo kikuu cha utawala bora hapa nchini...............
c) Baada ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme ikaikabidhi kazi hiyo kwa DOWANS ambao walitumia dola za kimarekani 7.5 milioni kununua mitambo hiyo ya kuzalisha umeme kazi ambayo ilikuwa ndani ya uwezo wa Tanesco.........................na hivyo hawakuhitaji mzabuni yeyote..........................
d) Tanesco kwa matendo yao walimhalalisha Dowans kuwa mzabuni wa kumrithi Richmond bila ya kupata kibali cha Bodi ya zabuni....
e) Baada ya mkataba kuisha Tanesco wakaishinikiza serikali kununua mitambo ya DOWANS kwa bei ambayo ilikuwa ni zaidi ya mara 20 ya bei ambayo Dowans walinunulia mitambo tajwa.......na ili kuishinikiza serikali kuinunua mitambo ya DOWANS, Tanesco wakaamua kuitumia Mahakama Kuu kwa kuwazuia Dowans wasiondoke na mitambo yao kwa amri ya Mahakama.....................bila sababu za kimsingi.........
f) Kutokana na uvunjaji huo wa mkataba kwa kutumia visingizio vya kuwa Dowans hawajalipa kodi, Msuluhishi akaibandika Tanesco jumla ya Tshs 185 Bilioni ikiwa ni zaidi ya mara 18 ya gharama ambazo Dowans walinunulia ile mitambo...............
g) Mwanasheria Mkuu ametoa ushauri Dowans walipwe huku uamuzi huo haujatoa sababu ni maeneo yapi Tanesco ilikuwa imekiuka huo mkataba kitendo ambacho kwa AG makini angeligangamala kuhakikisha analifungua shauri upya hapa Dar kupinga tuzo ambayo hata sababu za Tuzo hiyo hazifahamiki.........................Katika hukumu hiyo Msuluhishi aliahidi kutoa sababu lakini sababu hizo hakuzitoa sasa mdaiwa ataonaje kuwa katendewa haki? Hivi tuna AG au tunambabaishaji ambaye anadai ameipitia hiyo hukumu na ameona ipo beneti na tuilipe tu...............Hawa ndiyo wateule wa JK ambao kazi yao kuu ni kujenga mazingira ya kulipora taifa hili changa..........
h) JK hayuko tayari kumfikisha mahakamani Dr. Idrissa Rashid kwa sababu alimpeleka pale Tanesco kwenda kulipora hilo shirika la umma na hasa ukizingatia ya kuwa JK alivunja sheria za tanesco kuhakikisha Dr. Rashid anakwenda pale tanesco kulifilisi shirika hilo na mzigo wa hasara hizo kutupiwa raia wanyonge ambao kosa letu ni kumvumilia JK ambaye hana sifa ya kuliongoza taifa hili masikini duniani........
i) Haya ni mazingira yanaonyesha ya kuwa JK ni mshiriki kwenye mradi wa Dowans na hata kama jina lake halipo ila linawakilishwa na swahiba wake wa karibu Rostam Aziz kama ushahidi huu kwenye hukumu ya Dowans unavyothibitisha ambao tanesco wenyewe waliutumia ................................