IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

Kwa kipindi kifupi tumegundua kuwa Rweyemamu tuliyemjua siye yule tena. Sasa yuko kwenye kundi la wateule wachache na amesahau alikotoka. Akumbuke kuwa hayo anayoandika sasa hivi asingeweza kuyasimamia alipokuwa akiiandikia RAI ya waungwana. Kwa sasa anaweza kuiandikia RAI, Mtanzania, na hata Ikulu kwa sababu vyombo vyote hivyo kwa sasa havimsaidii mwananchi wa kawaida zaidi ya kuwasafisha watu wanaoelekea kuifilisi nchi yetu. Salva akumbuke tu uongo njia yake siyo ndefu hata siku moja. Ipo siku vilio na machozi ya watanzania wanaokosa mahitaji muhimu kutokana na ufisadi wanaoupamba vitadaiwa mikononi mwake.
 
From: "Salvator Rweyemamu" rweyemamu.salvator@gmail.com
Date: Sun, January 2, 2011 11:29 pm
Subject: On Dkt Slaa na Madai yake dhidi ya Mheshimiwa Rais Kikwete kuhusu Dowans

Hi wakubwa

This is important in terms of kuweka ukweli sawa. Tunaomba msaada wenu kwa mujibu wa shughuli zetu za habari. Best regards na usiku mwema.


Salva


Sishangai, mida hii Salva mara nyingi anakuwa ameshalewa na yupo mitaa ya MK pale Kinondoni.
 
JK chapa kazi tulokuchagua ndo tuta kutathmini! walikataa kukutambua wakalala na kutafakari later wakatubu wakakutambua!! alipochaguliwa Meya wa Arusha walijifanya nao kuteua wa kwao siku zilipopita wakakanusha wakadai hawaendi mahakamni,
Slaa atuletee vithibitisho vya umiliki wa Dowans tuone ukweli wa Kauli zake,
 
From: "Salvator Rweyemamu" rweyemamu.salvator@gmail.com
Date: Sun, January 2, 2011 11:29 pm
Subject: On Dkt Slaa na Madai yake dhidi ya Mheshimiwa Rais Kikwete kuhusu Dowans

Hi wakubwa

This is important in terms of kuweka ukweli sawa. Tunaomba msaada wenu kwa mujibu wa shughuli zetu za habari. Best regards na usiku mwema.


Salva


Sishangai, mida hii Salva mara nyingi anakuwa ameshalewa na yupo mitaa ya MK pale Kinondoni.

jamani mimi naomba nijue .... who were the recipients of this e-mail from Salva..... mimi ninavyojua official letter inatolewa free to the press....
 
Kwa haraka haraka, nime note vitu vifuatavyo:


6. Hatari zaidi, Ikulu inasema kuwa ICC imeamua kuwa Dowans ilipwe na TANESCO kiasi cha sh bilioni 185. Huu ni upotoshaji mkubwa na wa kifisadi. Hukumu ya ICC inasema kuwa Dowans ilipwe $64.2 million, sawa na sh bilioni 97. Hiyo tofauti ya sh bilioni 88 ambazo Ikulu imeziongeza kwenye madai ya malipo ya Dowans zimetoka wapi na zinakwenda kwa nani?

Hapa kuna habari mpya, yaani ufisadi ndani ya ufisadi, Ndugu tupe habari zaidi kuhusu hesabu hizi. Mungu tuepushe balaa hili!!!
 
Na bado wataendelea kujichanganya sana
 
Kwangu mimi maneno ya Doctor Slaa dhidi ya mafisadi ni ABSOLUTE!!!
Kama waziri wa nishati malima hajui chochote kuhusu Dowans, ikulu nayo halikadhalika haijui mmiliki ni kwa nini basi maneno ya mwadilifu Slaa yasiwe kweli kwamba mmiliki ni Jk?
.
NAAMINI KWAMBA MMILIKI WA DOWANS NI JK MPAKA ATAKAPOTAJWA VINGINEVYO!!
.
 
Hivi msemaji wa rais ni rais? Salva ameandika kana kwamba yeye ndiye aliyetuhumiwa, pia aliyetuhumiwa ni JK siyo rais.
 
Huyu ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu yet he can't even spell jina la kwanza la DK. SLAA, eti anamuita "Dkt. Wilboard."

Pia kusema "Dkt Slaa aliwania urais wa Tanzania kupitia CHADEMA na akashindwa vibaya sana," ni ushabiki wa kitoto wa kisiasa ambao tulitarajia mtu kama Yusuf Makamba au Tambwe Hiza wa CCM wayasema, si mkurugenzi wa Ikulu. It's quite astonishing!

Huyu lazima amepewa kazi kama mshiko...! Si unajua tena Msemakweli kawataja wale waliokuwa mafisadi wa Elimu walio na Ma-Phd, nk, huyu nadhani naye yupo ktk kundi hili. Wakati kila gazeti lilikuwa linaandika Jina na Dr Slaa ktk kampeni zilizopita kwa usahihi, huyu jamaa ambaye ndiye msemaji wa anayeaminika na ikulu hawezi kutamka au hawezi kuliandika kwa usahihi jina la 'rais wa umma'! Ina maana huyu jamaa anampa JK majina feki sana ya viongozi wa mataifa mengine kama hata anakosea jina la mtu muhimu wa mwaka 2010 ambaye vyombo vyote vya habari vilimripoti kuliko kiongozi mwingine yoyote wa enzi hii??

Hii inanikumbusha pia kauli kama za akina Werema na watendaji wengine wa JK, napata picha kuwa JK anao mlima mkubwa wa kuvuna mawe na kusawazisha ili awe na watendaji makini wa kumsaidia, sembuse na kulisaidia Taifa hili.

Na alivyoiandika statement yenyewe utadhani wale jamaa wa mtaani wanaoshadadia mambo na kubadilishana maneno kama wanaokaa kijiweni. Sio kauli ya msemaji wa ikulu anayeweza kukurupuka kwa style hiyo, na inaonyesha wazi kama hayupo na fikra na utendaji makini bali ushabiki na hasira. Aibu kwa utendaji wa state house pia!

That should never be a State house press release! Its a shame we can value it.
 
Haya tuambieni,

nani mmiliki/wamiliki wa dowans????????? Mbona swali ni rahisi sana?? Kwa nini wanatafuta majibu magumu. Ok jk hahusiki, sawa, nani sasa.

Ofisi za brela ziko hapo mjini si watusaidie ili raisi wetu asiwe anaguswa bila sababu????

.
Watakuja na jina la mchovu mmoja sasa hivi na kusema huyu ndio mmiliki wa Dowans, kwa staili ile ile ya mchovu Gire wa Richmond.
.
 
kwani huyo dowans na richmond ni wakina nani mbona hawatajwi na kama ni kampuni yenye hisa wamiliki wa hisa ni wakina nani? mbona hawatajwi?
 
... Kwa nini hawampeleki mahakamani Dr. Slaa na kuuthibitishia umma kwamba Slaa ni mwongo?....

Thubutuuuuu!
Wataishia kupeleka malalamiko yao katika Mtanzania na Rai tu.
 
JK hawezi kuukwepa ukweli kuwa ana masilahi mazito ndani ya DOWANS.......na huu hapa ni ushahidi:-

a) Uteuzi wa Dr. Idrissa Rashid kuiongoza Tanesco ulijaa mizengwe kibao..............Dr. Rashid mwenyewe alikiri kuwa pamoja na kuwa nafasi hiyo ilitangazwa magazeti yeye hakuiomba ila JK alimwomba amsaidie kwenye nafasi hiyo...........Hivyo pamoja na sheria ya Tanesco kuweka wazi kuwa Mtendaji Mkuu wa Tanesco atateuliwa na Bodi, JK aliingilia Bodi kinyume na sheria pale alipombandika swahiba wake pale Tanesco..........................Swali la kujiuliza JK alikuwa anatetea masilahi ya nani kwa kuiingilia Bodi ya Tanesco?

b) Kwa vile Dr. Rashid hakuwa ameteuliwa na Bodi ya Tanesco hivyo na yeye hakuona sababu ya kuishirikisha Bodi tajwa katika utoaji wa zabuni ya uzalishaji wa umeme kwa Richmond na hata zabuni hiyo haikupitishwa kwa Bodi ya zabuni na matokeo yake kampuni kivuli ikapewa kazi hiyo..........Kulingana na rekodi zilizopo Brella, Richmond haijawahi kusajiliwa hapa nchini na hivyoufanyaji wake wa kazi ulikuwa ni batili na haikupaswa kupewa zabuni tajwa............Haya ni makosa ya kijinai yaani "criminal negligence" na JK anashindwa nini kumkabidhi swahiba wake Takukuru? Hapa inaonyesha kabisa hoja za Dr. Hosea kwa Wikileaks ni za kweli ya kuwa JK ndicho kikwazo kikuu cha utawala bora hapa nchini...............

c) Baada ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme ikaikabidhi kazi hiyo kwa DOWANS ambao walitumia dola za kimarekani 7.5 milioni kununua mitambo hiyo ya kuzalisha umeme kazi ambayo ilikuwa ndani ya uwezo wa Tanesco.........................na hivyo hawakuhitaji mzabuni yeyote..........................

d) Tanesco kwa matendo yao walimhalalisha Dowans kuwa mzabuni wa kumrithi Richmond bila ya kupata kibali cha Bodi ya zabuni....

e) Baada ya mkataba kuisha Tanesco wakaishinikiza serikali kununua mitambo ya DOWANS kwa bei ambayo ilikuwa ni zaidi ya mara 20 ya bei ambayo Dowans walinunulia mitambo tajwa.......na ili kuishinikiza serikali kuinunua mitambo ya DOWANS, Tanesco wakaamua kuitumia Mahakama Kuu kwa kuwazuia Dowans wasiondoke na mitambo yao kwa amri ya Mahakama.....................bila sababu za kimsingi.........

f) Kutokana na uvunjaji huo wa mkataba kwa kutumia visingizio vya kuwa Dowans hawajalipa kodi, Msuluhishi akaibandika Tanesco jumla ya Tshs 185 Bilioni ikiwa ni zaidi ya mara 18 ya gharama ambazo Dowans walinunulia ile mitambo...............

g) Mwanasheria Mkuu ametoa ushauri Dowans walipwe huku uamuzi huo haujatoa sababu ni maeneo yapi Tanesco ilikuwa imekiuka huo mkataba kitendo ambacho kwa AG makini angeligangamala kuhakikisha analifungua shauri upya hapa Dar kupinga tuzo ambayo hata sababu za Tuzo hiyo hazifahamiki.........................Katika hukumu hiyo Msuluhishi aliahidi kutoa sababu lakini sababu hizo hakuzitoa sasa mdaiwa ataonaje kuwa katendewa haki? Hivi tuna AG au tunambabaishaji ambaye anadai ameipitia hiyo hukumu na ameona ipo beneti na tuilipe tu...............Hawa ndiyo wateule wa JK ambao kazi yao kuu ni kujenga mazingira ya kulipora taifa hili changa..........

h) JK hayuko tayari kumfikisha mahakamani Dr. Idrissa Rashid kwa sababu alimpeleka pale Tanesco kwenda kulipora hilo shirika la umma na hasa ukizingatia ya kuwa JK alivunja sheria za tanesco kuhakikisha Dr. Rashid anakwenda pale tanesco kulifilisi shirika hilo na mzigo wa hasara hizo kutupiwa raia wanyonge ambao kosa letu ni kumvumilia JK ambaye hana sifa ya kuliongoza taifa hili masikini duniani........

i) Haya ni mazingira yanaonyesha ya kuwa JK ni mshiriki kwenye mradi wa Dowans na hata kama jina lake halipo ila linawakilishwa na swahiba wake wa karibu Rostam Aziz kama ushahidi huu kwenye hukumu ya Dowans unavyothibitisha ambao tanesco wenyewe waliutumia ................................

RostamAziz.jpg


Hii evidence bwana Ruta.... imekaa vizuri na imetulia, na kama kuna wale wanaobisha, hii reference ya copy ya hukumu inatoa majibu kamili na waje na hoja nyingine.

Watanzania wanahitaji kauli toka kwa kamanda anayeona mbali - Dr Slaa, na sio toka kwa watu wasioona mbele kama akina Salva. Nchi yetu hii haiwezi kuendelea kushikiliwa (captivity) na watu wasioona mbele, wasio na dira na uchungu kwa taifa hata kidogo, bali wao wanavuna kama vile wapo 'shamba la bibi yao'! Haiwezekani tena.
Hii ni nchi ya Umma, wanahitaji ustawi. Iliyobaki ni kuwalipua tu ili wananchi waupate ukweli wa aina ya watawala wanaoshikilia na kufunga umaskini wao, na hao watawala wabovu wawajibike bila kusubiri wananchi wachukue maamuzi wenyewe mikononi!

Dr Slaa, unalo jukumu kulipasha Taifa kuhusu dira na mwelekeo wa kuelekea ukombozi dhidi ya uozo huu ulioachwa kulimaliza taifa, na umma wake unaoangamia kwa umaskini kila kukicha!
 
Sikutarajia Salva atoe kauli tofauti na hiyo.. zaidi ya yote sikutarajia aje na ufafanuzi wowote [ kwa kuwa hana jipya], anachosahau ni kuwa sasa kila kitu kipo wazi na mengi yatazidi kufichuka mpaka atachoka kutetea uwongo. Huku Wikileaks ikiendelea kutuletea habari zaidi za uozo wao... Tumefikia patamu jamani rusheni makombora mpaka ikulu ichoke kukinga hatimaye watakubali ukweli.. ALUTA KONTINUA
 
Jamani mbona kila baya awe anasukuwa tu JK, tatizo ni nini hasa ndugu zetu?

Hii sasa inafika mahali mpaka inaudhi kweli. Ndiyo maana tangu sasa bora ikulu iwekiwaporomosheeni matusi ya nguoni hivyo ndiyo mkome na umbeambea wenu huo.
Matusi hayabadilishi ukweli, subirini Wikileaks watoe nao muwaporomoshee matusi..
 
kwangu mimi maneno ya doctor slaa dhidi ya mafisadi ni absolute!!!
Kama waziri wa nishati malima hajui chochote kuhusu dowans, ikulu nayo halikadhalika haijui mmiliki ni kwa nini basi maneno ya mwadilifu slaa yasiwe kweli kwamba mmiliki ni jk?
.
Naamini kwamba mmiliki wa dowans ni jk mpaka atakapotajwa vinginevyo!!
.

mmiliki wa dowans ni jakaya mrisho kikwete
 
Hakika ikukulu imeingiliwa na madudu katika historia ya nchi yetu,
mkurugenzi wa mawasiliano ikulu anakurupuka na kutoa taarifa kutoka taasisi nyeti kama ikulu, badala ya kutumia oficial language anatumia lugha za mitaani kama anamuandikia barua kimada wake, ni aibu.
Mjibuni Dk Slaa kwa hoja makini sio upupu ulioandika, nilitegemea mnasema mmepeleka shauri mahakamani kumbe ni mambo yenu ya "tumpuuze" ili mje muumbuke kama Epa na Richmond. Sikupendi S.Rweimamu kwa kukubali kutumiwa na fisadi
 
Hiyo wala si lugha kali kama watu wanavyotaka kusema. Lakini kama mtu angesoma ila Tz Daima between lines, hakuna sehem ambayo ilimuhusisha Kikwete kwamba ndiye mmliki zaidi ya Title.

Habari ilikuwa by implications na ile ilikuwa ni politics. Kwa bahati mbaya Ikulu nao wameingia na sasa watakuwa wanafanya kazi ya kukanusha. Wangekaa kimya na wakaishughulikia DOWANS kivingine wangepata heshma zaidi kuliko kuhangaika kukanusha.

Kiuhalisia Kikwete hawezi kuwa mmiliki ila by implications.


why not mmiliki expressly!
 
Kama kweli serikali inawafahamu wamiliki wa Dowans haitoshi tu kusema kuwa JK siyo mmiliki wa Dowans na kwamba Dr. Slaa ni mwongo.

Je kutuambia wamiliki wa Dowans kutaigharimu nini serikali? kuna siri gani katika kuwataja hao wamilki?

Dk. Slaa aishika pabaya Ikulu

• Yatumia maneno ya kejeli, mtaani kujibu hoja zake

na Edward Kinabo

KURUGENZI ya Mawasiliano Ikulu imeelezea kukerwa kwake na hatua ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kumtaja rais Jakaya Kikwete kuwa alihusika katika uzembe uliosababisha taifa kutakiwa kuilipa kampuni ya Dowans sh bilioni 185 kama fidia.

Taarifa kali ya Ikulu iliyobeba ujumbe wenye maneno ya kebehi na ya mitaani ya kumwita Dk. Slaa mtu ‘aliyechanganyikiwa' na ‘mzabinazabina' ilisainiwa na Salvatory Rweyemamu ambaye kabla ya kwenda Ikulu alikuwa mmoja wa wahariri watendaji aliyekuwa akiheshimika kwa kutumia lugha fasaha na ya staha.

Rweyemamu katika taarifa yake hiyo iliyoonyesha waziwazi kuandikwa na mtu mwenye hasira, chuki na dharau ama kwa Dk. Slaa, CHADEMA na Tanzania Daima alikwenda mbele na kumwita kiongozi huyo wa kisiasa kuwa ni mtu hatari.

Sehemu ya maneno makali ya Rweyemamu kwa Dk. Slaa ni kama yale aliyosema, "Na kama kweli Dk. Slaa ametoa kauli hii na kusema maneno ya namna hii basi sasa Watanzania wanayo kila sababu na haki ya kuamini kuliko wakati mwingine wowote kuwa mzee huyu (Slaa) sasa amechanganyikiwa na ni mtu wa hatari sana kwa utulivu wa nchi hii."

Rweyemamu aliendelea kueleza, "Kama Dk. Slaa anataka kweli kujua wamiliki wa Kampuni ya Dowans, basi atafute ukweli huo na aachane na tabia ya kutapatapa na uzabinazabina yenye lengo la kuwapaka watu watope."

Ikulu ambayo katika mazingira ambayo si rahisi kuyaeleza imekuwa na desturi ya kukanusha kwa nguvu kubwa kila wakati jina la Rais Kikwete linapohusishwa na sakata la kashfa ya Richmond/Dowans.

Hii ni mara ya pili kwa Ikulu kufanya hivyo baada ya mara ya kwanza kuchukua hatua kama hiyo wakati Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, alipokanusha hoja zilizokuwa zikijaribu kumhusisha Rais Kikwete na uhusiano wake na mkataba wa Richmond.

Wakati Ikulu ikikanusha mara kwa mara kuhusishwa kwa Kikwete katika sakata la Richmond/Dowans kwa namna yoyote ile, upo ushahidi wa kibunge (rejea ripoti ya Kamati Teule ya Mwakyembe) unaoonyesha kwamba, maamuzi kuhusu mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura ulioipa ushindi Richmond ulijadiliwa na Baraza la Mawaziri lililokuwa chini ya uenyekiti wa rais mwenyewe.

Kama hiyo haitoshi, gazeti moja la kila wiki linalomilikiwa na kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambalo Rweyemamu amepata kuwa mmiliki wake, limepata kuchapisha katika ukurasa wake wa mbele barua ikionyesha barua aliyoandika aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kwenda kwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini kuhusu suala la Richmond ambayo nakala yake ilikwenda pia kwa Rais Kikwete.

Uamuzi wa jana wa Rweyemamu kuandika taarifa kali dhidi ya Dk. Slaa unakuja siku chache baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa migogoro ya kibiashara hivi karibuni kuamuru Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) kuilipa Dowans fidia kubwa baada ya kuvunja mkataba nayo kinyume cha taratibu.

Katika mahojiano maalum na gazeti Tanzania Daima Jumapili, la juzi Dk. Slaa alikaririwa akisema chanzo cha suala zima lililopelekea Dowans kutakiwa kulipwa fidia hiyo ni uzembe wa serikali na Rais Kikwete mwenyewe kwani ndio waliohusika katika kuileta kampuni ya Richmond ambayo baada ya kuonekana ya kitapeli iliamua kurithisha kazi zake kwa Dowans.

Ikulu katika taarifa yake hiyo kwa sababu zisizojulikana ilijikuta ikipotoka ama kwa makusudi au kwa kutojua ilipoeleza kuwa gazeti la Tanzania Daima lililonukuu maelezo ya Dk. Slaa, linamilikiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakati taarifa zilizopo kwa msajili wa magazeti zinaeleza bayana kwamba, gazeti hilo ni la watu binafsi.

Ikipinga maelezo ya Dk. Slaa kuhusu uhusiano wa rais Kikwete na Dowans, taarifa hiyo ya Ikulu ilisema, "Huu ni uongo wa mchana, ni uzushi wa karne na propaganda ya hatari. Kwa hakika na kwa namna isiyoweza kuelezeka kwa ufasaha, tumeshtushwa sana na kauli hii ya Dk. Slaa

"Mheshimiwa Rais Kikwete siyo mmiliki wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Dowans. Hakupata kuwa mmiliki, siyo mmiliki na wala hatakuwa, hata siku moja, mmiliki wa kampuni hii." Ikitumia lugha kali dhidi yake Ikulu iliwataka wananchi wampuuze Dk. Slaa ikidai kuwa ni mzushi na amechanginyikiwa.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Dk.Slaa kuitwa mzushi na vigogo wa serikali kwani mara kwa mara anapoibua maovu amekuwa akipingwa kwa kuitwa jina hilo ingawa anayoibua huthibitika kuwa na ukweli ndani yake.

BARUA YA SALVA KWA VYOMBO VYA HABARI HII HAPA


yaani hii yooote nini???? tuambieni tu nani mmiliki tutanyamaza
 
Kwanini tusianzishe na kijarida cha ku-document haya mambo na maoni yetu then tuyagawe mitaani? nadhani tutawasaidia wengi! hata kama baadhi yetu wanasema ni uzushi, wakumbuke hakuna uzushi usio na ukweli! JK atatuangamiza! full stop

ndg yangu Elli nakubaliana na wewe moja kwa moja, ni wazo zuri sana na la ufasaha, ni vizuri wa Tanznia walio wengi na hawana access na mtandao wayaone maoni yetu na naamini yatawabadilisha wengi, nipo tayari kwa hiyo project nasubiri go ahead ya wadau.
 
Back
Top Bottom