IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

IKULU: Kikwete si mmiliki DOWANS!

Hapa Dr Slaa, kule Wickleaks! Ikulu sasa joto iko juu!
Na kama kweli Dk. Slaa ametoa kauli hii na kusema maneno ya namna hii basi sasa Watanzania wanayo kila sababu na haki ya kuamini kuliko wakati mwingine wowote kuwa mzee huyu (Slaa) sasa amechanganyikiwa na ni mtu wa hatari sana kwa utulivu wa nchi hii.
 
hahahahahahaha! Nashindwa hata nichangie nini!! eti kuna jamaa hapo juu amechangia kwamba ikulu ni wacheza kiduku hahahahha! Kanikumbusha funga kapeni ya CCM pale jangwani Mkwere alivyomaliza kuhutubia tu akasema "...Weka mziki" lakini kabla ya hapo Mzee mwinyi alishatangulia kusema kuwa "...Atakuja hapa, mtaona atakavyocheza mziki"
 
Maneno ya kila siku mpaka yanachosha kila ouvu ukikemewa au baya kukosolewa watu hawataki kujibu hoja, ama watasema udini au uvunjifu wa amani au mtu hatari kwa taifa. Hivi huu ujinga utasemwa mpaka lini?? Salva jibu hoja siyo matusi ,EBu tutafakari
1. Kila mtu anajua kuwa Dr Rashid aliajiliwa Vodacom baada ya kustaafu Ugavanor wa benki kuu.
Inasemekana kuwa RA anamiliki share kubwa Vodacom hivi kuajiliwa kwa post kubwa katika campuni ni lazima shareholders wakubwa wajue na ikibidi waridhie hivyo RA aliridhia Dr. Rashid kuajiliwa Vodacom.
Na pia inasemekana kuwa RA ni rafiki wa Karibu na watu walio Ikulu Bwana mkubwa mwenyewe akiwa mmoja wao hivyo Dr Rashid kuteuliwa kuwa MG wa TANESCO inawezekana kabisa kati ya marefree wake mmoja wapo ni RA nafikiri hii ni logic!!
Kwa mambo yalivyosemwa tangu RICHMOND mpaka DOWANS na RA kuhusishwa kote huko na kwa ukimya wa IKULU muda wote huo , wakijitia uzuzu ati hawajui nani mmliki wa RICHMOND na DOWANS na sasa badala ya IKULU kututajia majina na vielezo halali vya kutuhakikishia nani mmiliki wa DOWANS inajibu kihuni mmhmm mimi sisemi
 
Hii historia ndeeeeeefu ya IKULI inasaidia nini?

IKULU YA KIKWETE, TUAMBIENI, NANI ANAMILIKI DOWANS?

Kukataa kujibu ni kukubali kuwa DOWANS ni ya JAKAYA MRISHO KIKWETE.
 
Hiyo wala si lugha kali kama watu wanavyotaka kusema. Lakini kama mtu angesoma ila Tz Daima between lines, hakuna sehem ambayo ilimuhusisha Kikwete kwamba ndiye mmliki zaidi ya Title.

Habari ilikuwa by implications na ile ilikuwa ni politics. Kwa bahati mbaya Ikulu nao wameingia na sasa watakuwa wanafanya kazi ya kukanusha. Wangekaa kimya na wakaishughulikia DOWANS kivingine wangepata heshma zaidi kuliko kuhangaika kukanusha.

Kiuhalisia Kikwete hawezi kuwa mmiliki ila by implications.

Tatizo hapa si kuwa mmiliki moja kwa moja lakini huyu kama mkuu wa nchi hawezi kukwepa kujua kuwa nani mmiliki wa Dowans.Yeye ana mbinu nyingi za kujua mmiliki.Lakini kakwepa kuzungumzia.Salva atakanusha sana lakini ipo siku atajua.
 
Jamani mbona kila baya awe anasukuwa tu JK, tatizo ni nini hasa ndugu zetu?

Hii sasa inafika mahali mpaka inaudhi kweli. Ndiyo maana tangu sasa bora ikulu iwekiwaporomosheeni matusi ya nguoni hivyo ndiyo mkome na umbeambea wenu huo.

Hii ni sawa na Bondia Tyson kupiga watu makonde ovyo akidai kufanya mazoezi ya ngumi.
Mmeshikwa pabaya sasa mnatoa ya nguoni matusi yakiwashinda mtaanza ngumi na hata kubananga watu.
 
Na kama kweli Dk. Slaa ametoa kauli hii na kusema maneno ya namna hii basi sasa Watanzania wanayo kila sababu na haki ya kuamini kuliko wakati mwingine wowote kuwa mzee huyu (Slaa) sasa amechanganyikiwa na ni mtu wa hatari sana kwa utulivu wa nchi hii.

Nukuu hii tena kwako haitusaidii.Toa hoja.Au unaunga mkono upupu huo?
 
Shuleni kwetu, mtu mmoja hakwenda mchakamchaka asubuhi kwa sababu aliuhusudu usingizi. Alipotafutwa na mwalimu wa zamu, akajifanya kichaa. Watu wakambeba kumpeleka hospitali ya vichaa. Akagoma akisema mimi siyo kichaa! Wakazidi kumbeba, naye akazidi kusema, mimi siyo kichaaxn. Je, wangemwaminije kama siyo kichaa? TAFAKARI....!

Kichaa ni Mwalimu wa Zamu kumwamini mkachaji wa mchaka mchaka kujifanya kichaa.
 
Naungana na Dr Slaa kusema mmiliki halali wa mitambo ya DOWANS ni JAKAYA MRISHO KIKWETE.
 
Hii historia ndeeeeeefu ya IKULI inasaidia nini?

IKULU YA KIKWETE, TUAMBIENI, NANI ANAMILIKI DOWANS?

Kukataa kujibu ni kukubali kuwa DOWANS ni ya JAKAYA MRISHO KIKWETE.

Tazama hili nalo! Kwani Ikulu ndio kwa msajili wa mashirika? kwenda BRELA ukaulize.
 
Hivi Kikwete anamiliki Dowans kama Rais au kam Kikwete?

Endapo anamiliki Dowans kama Kikwete kwa nini mtumishi wa ikulu anamtetea?
Kwa nini Kikwete mwenyewe asijitetee?

Dr Slaa hakusema Dowan inamilikiwa na Rais katika maana kwamba kila Rais wa Tanzania atakaye kuja atakuwa mmiliki by default.

Kikwete ni mmilikiwa wa Dowans kama mtu binafsi, sioni haja ya Salva kujipendekeza kama kiuno katika sakata hili.
 
Tatizo hapa si kuwa mmiliki moja kwa moja lakini huyu kama mkuu wa nchi hawezi kukwepa kujua kuwa nani mmiliki wa Dowans.Yeye ana mbinu nyingi za kujua mmiliki.Lakini kakwepa kuzungumzia.Salva atakanusha sana lakini ipo siku atajua.

Mie nilifikiri Rais ni Silaa? kumbe alishindwa vibaya sana kwenye kura eeenhhh.
 
Hivi Kikwete anamiliki Dowans kama Rais au kam Kikwete?

Endapo anamiliki Dowans kama Kikwete kwa nini mtumishi wa ikulu anamtetea?
Kwa nini Kikwete mwenyewe asijitetee?

Dr Slaa hakusema Dowan inamilikiwa na Rais katika maana kwamba kila Rais wa Tanzania atakaye kuja atakuwa mmiliki by default.

Kikwete ni mmilikiwa wa Dowans kama mtu binafsi, sioni haja ya Salva kujipendekeza kama kiuno katika sakata hili.

Hata hupendezi, kushadidia uzabizabina!
 
Duh yaani huyu Rweyemamu sijui anaonekana ni kubwa la vilaza yaani taarifa yake haina mashiko kabisa duh hawa ndo wanateam wa kikwete hawa, ila maandishi yake yanafanana sana na ya huyu Dar
 
Ukweli unabaki pale pale, dowans ni kikwete na genge lake, jamani hebu tukataeni kufanywa wa......nge. Hivi tutadaiwaje na mtu tusiyemjua? Tukatae kuwalipa wahuni watatu akiba za watoto na wajukuu wetu, sita alishasema hao ni wahuni wachache sasa tunaanza siasa za by implication? What are we doing watanzania wenzangu?
 
Ikulu imetoa kauli za mipasho

Source: Hapa

NAULIZA swali hilo kwa makusudi, kwani ni ajabu hata wanaonifahamu watashangaa kwanini nauliza swali hili.

Wanajua kabisa kuwa najua kuwa Ikulu huwa hawakurupuki. Kama huwa hawakurupuki lakini wanachosema kinaashiria kuwa wamekurupuka bila kutafakari tuwaeleweje? Huo ndio msingi wa swali langu.

Si tabia njema sana mtu kuanza kutajataja kuhusu Ikulu. Ikulu kama alivyosema Baba wa Taifa ni mahali patakatifu. Hivyo kama ni patakatifu hatutegemei kuwa kuna vitu vichafu Ikulu, hatutegemei kuwa kuna watu wachafu Ikulu.

Hatutegemei kuwa na kauli chafu zinazotolewa na Ikulu. Pamoja na hayo tunatarajia kuwa Ikulu ni kwa watu makini, wanaotoa kauli makini zisizotiliwa shaka, kauli thabiti zilizofanyiwa utafiti kwa kuwa Ikulu kuna ishara zote zinazohusu maisha ya wananchi wote wa Tanzania, kijamii, kisiasa na Kiuchumi. Kwa ufupi unapotaja Ikulu, unataja kila kitu kuhusu maisha ya Watanzania.

Bahati mbaya sana Ikulu yetu inayopaswa kuheshimiwa, imekuwa tofauti na dhana hiyo ya Watanzania. Hali hii ni kama vile kumwona askofu msikitini, au sheikh kanisani ni lazima tutashangaa. Ikulu yetu siku imekuwa kama kijiwe cha kawaida sana. Samahani Watanzania wenzangu kwa kauli hiyo.

Siku hizi Ikulu unasikia, kibaka ameingia ameiba maua na amefanikiwa kuruka ukuta bila askari wa Ikulu kumwona wakati anaingia. Siku hizi unasikia kuna biashara Ikulu utadhani Watanzania hawawezi kumlipa Rais wao waliyemweka madarakani. Aibu gani hii kwa Ikulu yetu.

Mbaya zaidi siku hizi Ikulu yetu inataka kuvamiwa na ugonjwa wa uzembe wa kufikiri, ambao haupaswi kamwe kuwepo katika taasisi hiyo. Inavyotarajiwa na wengi, au hata isipotarajiwa inapaswa kuwa.

Unaposikia kauli hii ni ya Ikulu, basi ina hadhi tofauti, inapokelewa tofauti, inaonekana ni kauli iliyotafakariwa, ikafanyiwa utafiti, ikathibitishwa ndipo ikatangazwa. Katika mantiki hii sitegemei sana hata siku moja kuwa Ikulu inaweza kuomba radhi. Ikiomba radhi maana yake ilikurupuka kutoa tamko bila kufanya utafiti na hiyo ni hatari kwa nchi nzima.

Taarifa nyepesi isiyokidhi hata kuwajibu watoto wadogo, ni iliyowahi kutolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kuwahadaa Watanzania. Akisema kuwa wahusika wamepewa onyo na kuwahakikishia Watanzania kuwa hakukuwa na dalili zozote za rushwa katika sakata hili na Rais Jakaya Kikwete hahusiki na Richmond.

Luhanjo alisema: "Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na maneno na vijembe ati kuwa kuna mkono wa Rais Jakaya Kikwete katika kutoa tenda ya kuzalisha umeme wa dharura iliyopata Kampuni ya Richmond. Kiini cha maneno hayo ni kauli za baadhi ya wanasiasa zilizopazwa na baadhi ya vyombo vya habari.

"Tunapenda kusema, tena kwa msisitizo kuwa, maneno hayo si ya kweli na hayana msingi wowote. Rais hajahusika na uamuzi wa tenda hiyo kupewa kampuni ya Richmond. Hadi leo Ikulu pamoja na kukanusha uhusika wa Kikwete, haijawahi kuwa na kauli ya wazi kuwa wahusika wa Richmond walikuwa akina nani?
Kauli hiyo ya Ikulu ilitolewa na baada ya siku chache nchi iliingia gizani, na rais aliagiza mitambo ya IPTL iwashwe haraka. Ilikuwa kama kichekesho au Igizo.

Oktoba 21, 2009 Rais Kikwete alitoa agizo kuwa mitambo ya IPTL iwashwe. Oktoba 25, 2009 tayari meli yenye shehena ya mafuta iliwasili Dar es Salaam kwa ajili ya kutumika kwenye mitambo ya IPTL. Tulihoji kwa umakini na kwa kina bila woga, tena kwa ujasiri wa uzalendo, hivi kweli hakuna mkono wa rais katika giza lililoikumba nchi wakati huo, au katika hili suala la kukatika umeme?

Tulitafakari kuwa Rais Kikwete alitoa tangazo kuwa mitambo ya IPTL iwashwe, Oktoba 21, 2009, kisha tukaambiwa na William Ngeleja kuwa serikali imeagiza mafuta ya kutumia kwenye mitambo ya IPTL Arabuni. Baada ya siku chini ya sita, tukataarifiwa kuwa mafuta yameletwa na merikebu ya mizigo na yamefika bandari ya Dar es Salaam yakisubiri kupakuliwa ili mitambo hiyo iwashwe. Tena meli zingine inabidi zisogezwe haraka ili kupisha upakuaji wa shehena ya mafuta ya IPTL.

Tulijiuliza tena, meli toka Arabuni huchukua siku ngapi? Au mafuta yaliagizwa kabla ya Ikulu kuzungumza? Na ilikuwaje mafuta yakaagizwa kabla ya Ikulu kutoa tamko? Ikulu ilipataje kujua kuwa giza litaingia na nchi itatumia mitambo ya IPTL?

Ni wachache sana tuliokubali kuwa giza hili lilipangwa, tena kwa ajili ya kutafuta umaarufu wa kisiasa ambao hauna uzalendo hata kidogo, bali ni udhaifu mbaya sana wa uongozi, unaoashiria rushwa mpaka uongozi wa juu wa nchi.

Meli hii ilikimbia kiasi cha kuvunja rekodi ya safari za meli toka Arabuni kuja Tanzania chini ya muda wa siku sita tu! Iliwezekanaje? Kama kweli mafuta yalishaagizwa toka Arabuni kabla, kwanini yaliagizwa? Nani aliagiza? Alikuwa anatekeleza agizo lipi? Alijuaje amri ya rais kabla haijatamkwa? Alijuaje kuwa IPTL wangekubali kuwasha mitambo? Alijuaje kuwa IPTL hawana mafuta ya kuwasha mitambo? Niliacha maswali mengi kwa kauli hiyo ya Ikulu.

Nimeshtushwa tena na Kauli ya Ikulu kwa majibu mepesi kama yaliyotolewa mwaka jana yanayoacha shaka nyingi miongoni mwa watu makini wanaofikiri. Hivi Ikulu huwa wanasema yote wanayowaza bila kutafakari? Ikulu imekurupuka kujibu hoja ya Dk. Slaa kuhusishwa na Dowans, Kauli iliyotolewa na msemaji wake.

Kauli ya Rweyemamu inayonukuliwa ikisema "Na kama kweli Dk. Slaa ametoa kauli hii na kusema maneno ya namna hii basi sasa Watanzania wanayo kila sababu na haki ya kuamini kuliko wakati mwingine wowote kuwa mzee huyu (Slaa) sasa amechanganyikiwa na ni mtu wa hatari sana kwa utulivu wa nchi hii.

Vema, tuiulize Ikulu sasa, imeunda lini kitengo cha kushughulikia watu waliochanganyikiwa? Na imefanyia kazi kauli ngapi za watu waliochanganyikiwa? Kwanini imeanza na kauli ya Dk. Slaa. Na kama Ikulu imeshajua kuwa huyu mtu ni hatari kwa utulivu wa n chi mbona haimkamati? Hivi mtu aliyechanganyikiwa anaweza kuwa hatari kwa utulivu wa nchi?

Ikulu inaendelea kusema "Kama Dk. Slaa anataka kweli kujua wamiliki wa Kampuni ya Dowans, basi atafute ukweli huo na aachane na tabia ya kutapatapa na uzabinazabina yenye lengo la kuwapaka watu matope . Narudia kauli ya Nyerere, Ikulu ni pasafi, kama inaona inachafuliwa na Dk. Slaa kwanini yenyewe isiseme ukweli ili kujisafisha? Ikulu haikupaswa kuingia katika mgogoro na Dk. Slaa kuhusu ukweli wa Kampuni ya Dowans, badala yake ingejikita katika ukweli kututajia kama Kikwete hahusiki basi nani anahusika. Hii ndiyo hoja, bila kujali kama Dk. Slaa amesema au hajasema, maana Watanzania wengi wanajiuliza sana.

Ikulu imekuwa ikitumia muda mrefu ikikanusha mara kwa mara kuhusishwa kwa Kikwete katika sakata la Richmond/Dowans kwa namna yoyote ile, lakini upo ushahidi wa kibunge (rejea ripoti ya Kamati Teule ya Mwakyembe) unaoonyesha kwamba, maamuzi kuhusu mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura ulioipa ushindi Richmond (kampuni dada ya Dowans) ulijadiliwa na Baraza la Mawaziri lililokuwa chini ya uenyekiti wa rais mwenyewe. Sasa alijitoa lini katika uhusika huu? Kwanini Rweyemamu anaturudisha kwenye majibu mepesi ya Luhanjo?

Kama Ikulu yetu ipo makini, tayari Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema Dowans ni kundi la watu wachache wasio na uzalendo wanaojinufaisha na rasilimali za nchi.

Mbona Ikulu isiseme kuwa Pinda Kachanganyikiwa? Mbona Ikulu inatafuta wamiliki wa Dowans nje wakati wanaosema wanawajua wamiliki wa Dowans wapo Ikulu? Mbona huku ni kukurupuka kwa wasemaji wa Ikulu?

Samuel Sitta, Spika wa zamani na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa serikali iliyopo Ikulu anasema, Dowans ni kundi la watu wanaotaka kuhujumu nchi pesa ili kujiandaa na kinyang anyiro cha urais mwaka 2015.
Ikulu haisemi kuwa waziri huyu amechangayikiwa, wala haitaji tabia ya uzabinazabina, haitaji kuwa waziri huyu anapaka watu matope, wala hailalamikii kauli hizo kuwa ni za uchochezi zinazohatarisha utulivu wa nchi. Lakini Ikuku inashtushwa na kauli za nje ya Ikulu zinazofanana na zile zinazotolewa na mawaziri waliopo Ikulu.

Dk. Slaa anayefikiriwa kuwa amechanganyikiwa ndiye ametaja wamiliki wa Dowans, je, Ikulu isiyochanganyikiwa, iliyo makini, yenye kutoa matamko yaliyofanyiwa utafiti, sasa iseme wamiliki wa Dowans ambao wanataka taifa letu liangamie na kuua TANESCO ni kina nani?

Ikulu iwe wazi. Isimame hadharani iseme, wamiliki wa Dowans siyo sisi ni fulani. Wala haihitaji kununua vocha kupiga simu kuuliza ili itutajie. Pinda na Sitta wanapatikana Ikulu, waulizwe ili kumsafisha Kikwete. Lakini Pia hoja nyingine, Hivi Pinda na Samuel Sitta wapo tayari kukana imani zao, uzalendo wao ili waseme uongo kushiriki jinai hii ili sisi Watanzania tuangamie kwa kuwalipa kundi la wezi wa Kampuni ya Dowans?

Wasemaji wa Ikulu acheni kuaibisha Ikulu kwa kutoa majibu mepesi kwa mambo yanayohusu nchi yetu.
Kitu kibaya hakiwezi kutoa kitu kizuri. Uchafu hauwezi kukaa Ikulu, ni patakatifu. Kauli za Ikulu ziwe safi, thabiti na zisizo za kutiliwa mashaka.
Tamko lina gharama. Ikulu inapotoa tamko jepesi inafikiriwa inafanya mambo ya hali ya chini na hayo hayapaswi kuwepo Ikulu.
 
Back
Top Bottom