Ikulu Dar: Rais Yoweri Museveni na Rais Samia Suluhu washuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta

Mhe. Rais Museveni na Mhe. Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania
Sasa kuna tatizo. Kutokana na tatizo la mabadiliko ya mazingira (climate change), mataifa makubwa duniani yameweka mkakati wa kuacha kutumia mafuta kwa ajili ya magari na mitambo. Norway kwa mfano, wanasema kufikia 2050 wataacha kabisa shughuli za kuchimba mafuta.

Uingereza wanasema watapiga marufuku magari ya kutumia diesel kufikia 2025 nadhani. Japan, Germany na hata China, wote wanasema ndani ya miaka 15 ijayo wanataka kutoka kwenye kutumia mafuta kwenye magari na kuingia kwenye magari ya umeme (from internal combustion engines to electric vehicles)

Sasa hii inamaanisha nini kwa nchi kama Tanzania ambazo hadi sasa zimekalia tu uchumi wa mafuta bila kuuendeleza? Ina maana ndani ya miaka 20 ijayo, mafuta yatakuwa si mali kitu. Hata ukigundua una mafuta mengi kama bahari ya Hindi, hayatakusaidia tena kwa kuwa dunia imeanza kuondoka toka tekinolojia ya mafuta kwenda teknolojia ya umeme!

Hivyo basi, kama kweli tunataka kufaidika na rasilimali ya mafuta tuliyonayo, ni lazima iendelezwe ndani ya kipindi cha miaka kumi ijayo. La sivyo haya mafuta yatakuwa na rasilimali isiyohitajika tena duniani, na ndani ya kipindi cha miaka kumi ijayo tutaanza kushuhudia kuporomoka kwa bei ya mafuta kadiri magari ya umeme yanavyoingia sokoni. Leo hii hata Lamborghini wamesema wataacha kutengeneza gari za mafuta!

 
Uganda pia wanataka Gesi kutoka Tanzania, lkn speed ya kusambaza gesi hapa Tanzania bado ni ndogo sana,
bado watanzania walio wengi hawajafaidika na gesi yetu.

Kabla hatujaiuza Uganda na Kenya kwanza gesi hiyo itufaidishe kwanza ndipo tuiuze nje.
 
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni leo tarehe 20 Mei, 2021 atafanya ziara ya kikazi ya siku 1 hapa nchini kwa Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa hapa nchini Mhe. Rais Museveni na Mhe. Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni za uwekezaji katika mradi huo (Host Government Agreement) utakaofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.

========

Shughuli inaanza kwa nyimbo za Taifa na wimbo wa Afrika Mashariki. Gerson Msigwa anaanza kwa kutoa ufafanuzi wa wingi wa mikataba inayosainiwa kwenye bomba hilo.

Msigwa amefafanua mkataba wa leo ni makubaliano kati ya nchi ya Tanzania na kampuni itakayotekeleza mradi, amesema miradi mikubwa kama huu wa mafuta unaohusisha zaidi ya pande moja huambatana na utiaji saini wa mikataba kadha kadha hivyo hakuna kujirudia kwa utiaji saini wa mikataba.

Mkataba wa bomba la mafuta umetiwa saini na waziri wa nishati, Medard Kalemani shuhuda akiwa mwanasheria mkuu wa Tanzania, Prof. Kilangi na kwa upande wa kampuni ya EACOPP ni mkuregunzi mkuu wa kampuni hiyo, Martin John na atashuhudiwa na rais wa utafiti na uzalishaji wa Total Afrika, Nicholaus Teraz.





========

Pia soma

Hivi kwann mikataba ni siri ya serikali?
 
Mara Pap Mtawala kikongwe wa UG amekuwa 1st Gentlemen. Watoto wa kike sio wakuwaamini sana. Tunaweza jikuta Dodoma inahamia Kampala. Tunasema mikataba ya bomba kumbe hati za ndoa.
Rais Samia pengine anao umri wa mama yako mzazi. Jaribu uwe na adabu japo za kinafiki.

Watu wa aina yako ndio mnaoanzisha uzi wa kudharau serikali ya sasa kila siku, ujumbe wenu wa msingi kabisa ni akili za kipumbavu kama hizi.
 
Huo utakuwa ni utiaji saini wa ujenzi wa bomba la maziwa, la mafuta walishamaliza zamani.
 
Back
Top Bottom