Mzee Kondo bin Kondo, aliyekuwa mpenzi mkubwa wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam ndiye aliyekuwa maarufu sana kwa kuuza samaki wa kubanika, sokoni Kariakoo.
Marehemu Mzee Sykes, pia alikuwamo kwenye harakati za haki za wafanyakazi; Bodi ya Elimu ya H.H. Aga khan, na ile ya taasisi ya Kiislamu ya Jamiatul-Islamia fi Tanganyika. Uwepo wa ‘mashujaa wa Uhuru’ kama Mzee Mshume Kiyate, Abdulwahid Sykes na Sherif L’aatasi, unalifanya soko la Kariakoo kuingia katika moja ya sehemu muhimu sana katika historia ya kugombania Uhuru wetu.
Said Chaurembo, ndiye aliyelijenga jumba hilo wakati ule ambao Waafrika wengi hawakuwa na uwezo wala kuwazia kujenga nyumba kubwa kama ile. Sheikh Abdallah Iddi Chaurembo ni nduguye Said Chaurembo. Yeye alipata kushika nyadhifa mbalimbali za kiuongozi katika jamii ikiwamo kuwa Imam Mkuu wa Msikiti wa Mtoro, mjumbe wa Maulid Committee na Kamati Kuu ya TANU Taifa.
Kwa miaka kadhaa, amepata pia kuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kiislamu ya Aljamiatul- Islamia, iliyokuwapo pale Barabara ya New Street (sasa Lumumba).
Abeid Karume, baada ya Mapinduzi matukufu kule Unguja, alizipiga marufuku taasisi pamoja na maduka ya Poni yaliyokuwa yamezagaa mjini Unguja na kuutangazia umma kwamba kila aliye na chake kwenye duka la poni aende akakichukue bure chini ya usimamizi wa Serikali ya Mapinduzi!
Sheikh Hassan Bakari ni kaka mkubwa wa Sheikh Muhiyidien Mkoyogole wa Temeke, na kiongozi wa Tariqa Qadiria. Yeye alikuwa na madrassa yake mahala hapo ambapo vijana wengi wa mjini walipitia kupata elimu ya Kiislamu. Tariqa Qadiria baadaye ilihamia kule Wailes, Temeke.
Baada ya uhuru kupatikana, Pombe Shop iliyokuwapo kwenye kona ya Kongo na Narung’ombe, ilivunjwa na kutengenezwa jengo lile zuri la DDC na Shirika la Maendeleo ya Dar es Salaam.
Ilikuwa ni mahala hapohapo kwa mbele kidogo, ndipo zilipokuwa ofisi za magari ya abiria ya Muhindi mmoja Jamal Ismail, zilizokuwa zikifanya safari ya kwenda na kurudi Morogoro, Tanga na Moshi. Mabasi mengine ni ya Champsi Mulji Babla na Abood Saleh Abood, maarufu Abood Bus, yaliyokuwa yakifanya safari ya kwenda Bagamoyo na Morogoro.
Hulali jmn kuna tatizoHilo jina la kariakoo limesambaa mikoani sijui kwanini! Mikoani pia kuna kariakoo
Nipo night mkuu!! so napeleka masaa huku mtandaoni!Hulali jmn kuna tatizo
Haha halafu kuna kiumbe amekuudhi nilikuonaNipo night mkuu!! so napeleka masaa huku mtandaoni!
Tena kesho asubuhi nikitoka Job nalala naamka naee ujiandae kushuhudia navomvua mtu nguo asubuhi kweupeee!Haha halafu kuna kiumbe amekuudhi nilikuona
Naona utasoma thread zote leo😆Nipo night mkuu!! so napeleka masaa huku mtandaoni!
Kuwa na subira mkuu,jaribu kukaa mbali na shetani,usijaribu kulipiza kisasi,mpuuze aliye kukosea huenda akajifunza na kujirudi,ni hayo tu mkuu.Tena kesho asubuhi nikitoka Job nalala naamka naee ujiandae kushuhudia navomvua mtu nguo asubuhi kweupeee!!
Wait and see na nilivovurugwaaaa hasira Zangu zotee atazibeba mbona!