Ijue Comoro: Fursa za Biashara na Changamoto Zake

Really?

Seriously?

Ni kweli na wala sina mpango wa kufika huko, route zangu ni Sheghen countries and UK.

Need i say more?

Hata wazungu wanaokuja Tanzania wana hiyari ya kuomba viza kwenye balozi zetu kwenye nchi zao, au viza on arrival airport, hujuwi kitu takataka tu.

Hakuna anayejiuwa kila kitu, ila huwezi kunidanganya vitu vidogo sana kwangu kama hivi.
Nimeanza kusafiri wakati Uingereza Watanzania tulikuwa tunaingia kwa entry tu airport hatukuwa tukiomba viza ubalozini kabla Wapemba hawajatuharibia mwaka 1995 na CUF yao.

Ndio sembuse Comoro nchi ambayo naamini bado swala la choo kwa kila nyumba bado mtihani ndio wawe na condition hizo?

Je una lingine?
Sijawahi kuona mzee mjinga kama wewe.
Si ukubali tu kuwa hujui.

Eti enzi mnaenda uingereza.
Hivi una hata passport kweli?
 
1comorian franc=0.0023USD

Iyo thaman unayosema ni ipi mkuu
Kama umesoma vizuri ukaelewa, nilisema sielewi kwanini pesa yao ina thamani ukilinganisha na ya kwetu.

Kwa mfano 1000 ya Comoro ni almost 5400 ya kwetu ukiipeleka kwenye USD unapata ngapi?
 
Iko hivi Comoros ni nchi ya kitu kidogo rushwa na ubwanyenye ni mwingi sana.
Kwa hiyo hata mambo yanavyoendeshwa ni lazima uwe na connection ya kukushika mkono.

1. Nilishuhudi mtanzania akiharibiwa matikiti maji yake kisa kakosana na mamlaka.

2.Ukiwa mgeni ukiwekeza uwekezaji mkubwa huyo aliyekushika mkono anaweza kukufanya kitega uchumi pia.

3.Usafiri ni ndege tena ATC na kuna vindege vingine vidogo nimesahau majina

4.Meli ni kwa ajili ya mizigo, by the time niko kule kuna kampuni ilikuwa inafanya research ya kupeleka meli na hata JMT kupitia JWTZ walitaka kupeleka meli za mizigo.

5.Nchi haiko stable kisiasa, Rais wa madarakani ka edit katiba kaongeza muda, halafu kamuweka lockdown raisi wa Zamani Sambi.

6.Visa, zipo za airport ila mpaka uwe na justificative za wapi unafikia, kifupi jamaa hawako systematic, walishawahi kumzuia jamaa fulani pale airport aliletwa na kampuni.

7.Ukitaka kuona sisi JMT ni matajiri nenda Comoros.

8.Mademu wakali wengi ni wa Kianjouan wana kama mixer.

9.Comoros iko kwenye arab league.

10.Mtanzania unaitwa Mdarisalama

11.Moroni kwa hapa kwetu ni kama pale Rangi tatu
Kutoka Zakhem mpaka Charambe, kwa anayepajua jenga picha hiyo.

12.Fursa za biashara ni za chakula sana sana,zamani mpaka nyama
Mchele( maele),magimbi, ndizi, mayai hivi utauza,jamaa hawaujui ugali.
Watu wanapeleka mpaka ndimu.

13.Kilimo:Ardhi ya Grande Comoros sehemu kubwa ina mawe, kilimo labda kisiwa cha Mohel na Anjouan.

14.Wabongo wapo mpaka mama ntilie, mafundi simu, wauza maduka. Asilimia kubwa ni wazanzibar kutoka na historical back ground kwani kuna mpaka majina ya sehemu kufanana
Mfano ngome kongwe kule kuna Ngome kazi kama sikosei.

15.Lugha ni Chikomore na Kifaransa, Kiingereza chako utawapata wachache, hata mademu itakuwa shida, bora uongee kiswahili wanakuelewa kidogo.

16. Muunganiko wa watanzia upo ila haupo thabiti sana kwa kweli, kuhujumiana, majungu kibiashara kupo sana.

Inatosha hapa
 
Inaendekea.....

FURSA ZA BIASHARA

kama nilivyoeleza hapo juu hii nchi haina kitu chochote Inachozalisha kitu ambacho kinapelekea kuwepo kwa fursa nyingi za biashara.

Kitovu cha biashara ni mji wa Moroni - Grande Comores na asilimia kubwa ya biashara huku zinafanywa na Watanzania, Waanjouni na wabushi (Wamadagascar).

Fusra nyingi za kupiga pesa ziko kwenye bidhaa za chakula; hapa nina maanisha mali mbichi na mali kavu pamoja na biashara ya mifugo.

Bei za bidhaa hukun hubadilika kulingana na demand hivyo kama unataka kufanya biashara lazima ujue ni bidhaa gani haiko sokoni ambapo ukibahatisha kuleta na ukajikuta ni wewe mwenyewe utapiga pesa safi. kwa mfano sasa hivi hakuna mayai hivyo ikitokea mtu akaleta leo basi atauza trei moja kwa elf20.

Biashara ya mifugo nadhani ndio inalipa Sana ila ina changamoto zake.

CHANGAMOTO ZA KUFANYA BIASHARA HUKU

Moja ya changamoto kubwa inayo wakumba wafanyabiashara huku ni UTAPELI, NA HUJUMA; vinara wakubwa kwa utapeli na kuhujumu wafanyabiashara wenzao ni watanzania.

Kwa kifupi niseme kuwa watanzania walioko huku ni wabinafsi na wana roho mbaya sana. hawataki kuona wenzao wakifaidika.

Watanzania wengi walioko huku ni matapeli na wameharibu sana reputation ya watanzania wote
Tanx muda mwingine tunatakiwa kuthink ahead tusibeze Sana na kukejeli maarifa ujuzi na taarifa Kama hizi ni Kama tools ya kusaidiana tuyafikie malengo
 
Back
Top Bottom