Tanx muda mwingine tunatakiwa kuthink ahead tusibeze Sana na kukejeli maarifa ujuzi na taarifa Kama hizi ni Kama tools ya kusaidiana tuyafikie malengoInaendekea.....
FURSA ZA BIASHARA
kama nilivyoeleza hapo juu hii nchi haina kitu chochote Inachozalisha kitu ambacho kinapelekea kuwepo kwa fursa nyingi za biashara.
Kitovu cha biashara ni mji wa Moroni - Grande Comores na asilimia kubwa ya biashara huku zinafanywa na Watanzania, Waanjouni na wabushi (Wamadagascar).
Fusra nyingi za kupiga pesa ziko kwenye bidhaa za chakula; hapa nina maanisha mali mbichi na mali kavu pamoja na biashara ya mifugo.
Bei za bidhaa hukun hubadilika kulingana na demand hivyo kama unataka kufanya biashara lazima ujue ni bidhaa gani haiko sokoni ambapo ukibahatisha kuleta na ukajikuta ni wewe mwenyewe utapiga pesa safi. kwa mfano sasa hivi hakuna mayai hivyo ikitokea mtu akaleta leo basi atauza trei moja kwa elf20.
Biashara ya mifugo nadhani ndio inalipa Sana ila ina changamoto zake.
CHANGAMOTO ZA KUFANYA BIASHARA HUKU
Moja ya changamoto kubwa inayo wakumba wafanyabiashara huku ni UTAPELI, NA HUJUMA; vinara wakubwa kwa utapeli na kuhujumu wafanyabiashara wenzao ni watanzania.
Kwa kifupi niseme kuwa watanzania walioko huku ni wabinafsi na wana roho mbaya sana. hawataki kuona wenzao wakifaidika.
Watanzania wengi walioko huku ni matapeli na wameharibu sana reputation ya watanzania wote