Ijue Comoro: Fursa za Biashara na Changamoto Zake

Fursakibao

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
6,681
11,123
Habari GT,

Nianze kwa kusema kuwa mimi sio muandishi mzuri ila nitajitahidi kuweka vitu katika mpangilio kwa kiasi chake.

Kabla ya kuangalia baadhi ya fursa za biashara zilizoko Comores na changamoto zake, hebu tuangazie kidogob jamii ya watu wa huku katika nyanja za siasa, uchumi na jamii kwa ujumla.

SIASA:
Comores inaundwa na visiwa 4 ambavyo ni Grande Comore, Anjoun, Moheli na Mayyote, japo Mayyote imeng'ang'aniwa na Mfaransa (kwa wale wanaotaka kuzamia Ufaransa hii ndio shortcut; ukifika Mayotte tu hesabu umeshafika Ufaransa).

Kwa sasa hali ya siasa kisiwani humu si shwari kwa sababu inasemekana raisi alieko madarakani amegoma kutoka baada ya mda wake, hivyo wenye zamu yao kuongoza mda wowote wanaweza kukinukisha wakipata support; kwa fununu za mtaani wenye zamu yao, wako tayari kulipa gharama yoyote kwa mtu yeyote atakaeweza kuwasaidia kumg'oa presida; kuna mengi ya kusema hapa ila sio lengo la uzi, hivyo nitashia hapo.

UCHUMI:
Hali ya uchumi wa nchi hii ni mbaya Sana, maana nchi kama nchi haina vitega uchumi zaidi ya bandari, airport, mitandao ya simu na biashara ya kuuza mafuta, gesi na umeme wanao zalisha kwa kutumia magenereta.

Asilimia kubwa ya wanachi Comores wana maisha magumu sana, kiasi kwamba wengi wao wanaishi kwa mlo moja tena kwa kula mikate na vipapatio vya kuku kwa asilimia kubwa (katika watu wanaojua kuutumia vizuri unga wa ngano basi ni wakomoro). huku ukila mapaja ya kuku au nyama ni ufahari.

Licha ya kuwa uchumi wao uko chini, chakushangaza pesa yao iko juu zaidi ya Dola na Euro na juu zaidi ya pesa zetu za madafu. Hapa wataalamu wa uchumi wanaweza kutusaidia how is it possible ukizingatia kuwa 99% ya mahitaji yao yote wanaagiza nje.

JAMII KWA UJUMLA
Jamii ya wakomoro imegawanyika katika makabila matatu ambayo ni waanjuan, wangazija na waanjoun.

Katika jamii za kikomoro, wanawake ndio wenye sauti kuliko wanaume. huku ukioa unatakiwa ukaishi ukweni (mwanaume hana saut) suala la kuchepuka huku ni la kawaida kwa wanandoa; utachapiwa hadharani na huna la kusema.

ustaarabu katika jamii hizi ni sifuri, watu wanakunya hadharani bila kuona aibu; ilimradi tu kuwe na maji ya kuchambia basi mtu atavua nguo na kunya pembeni yako.

watu wa huku wanakula bila kunawa; maji ya kunawa utapewa baada ya kula ama usipewe kabisa

KWA uvivu hawa jamaa wamewashinda wazanzibar; japo nadhani uvivu wa hawa unachangiwa na mlo hafifu.

99% ya watu wa huku ni waislamu; uzuri wao hawana ule ujinga kama wa Zanzibar. Phawana ubaguzi kwa watu wa dini nyingine)

Sasa twende Kwenye Lengo la Uzi.

Inaendelea uk.23....
 
Nina rafiki yangu mcomoro huja Dar kupata matibabu..wiki iliyopita niliongea nae kuhusu fursa zilizopo comoro akaniambia Satoh ukileta viatu vya kimasai utapiga sn hela kule,Ila kutokana na mishe zangu nimekuwa mzito sn wa kudeal na hiyo ishu

Kwa wenye mitaji mikubwa ukiwekeza kwenye afya km hospital au zahanati unatoboa maana wacomoro wengi wanakuja kutibiwa Dar.Ukienda hospitali ya Apollo wamejaa sn pale
 
Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Vipi kwenda visa vinahitajika?
 
Nina rafiki yangu mcomoro huja Dar kupata matibabu..wiki iliyopita niliongea nae kuhusu fursa zilizopo comoro akaniambia Satoh ukileta viatu vya kimasai utapiga sn hela kule,Ila kutokana na mishe zangu nimekuwa mzito sn wa kudeal na hiyo ishu

Kwa wenye mitaji mikubwa ukiwekeza kwenye afya km hospital au zahanati unatoboa maana wacomoro wengi wanakuja kutibiwa Dar.Ukienda hospitali ya Apollo wamejaa sn pale
Moja kati ya vitu nilivyofanyia research huku ni biashara hiyo ya afya. Kwa ufupi hiyo ni biashara ngumu Sana maana hata huku hospitali zipo ila inasemekana wakomoro hawataki kwenda kwenye hospitali zao maana wanapenda Sana kusafiri hivyo Dar imekuwa kam option yao Ili waweze kutembea kidogo.

Kwenye biashara ya viatu sina hakika kama inalipa kama rafiki yako alivyokuambia. Maana huku vipo na unaweza kumaliza mwezi usione hata mtu moja amevivaa.
 
Back
Top Bottom