Simiyu: Utata kesi Askari Polisi aliyetuhumiwa kumjeruhi mtoto wake kisha kesi kufutwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Miezi mitano tangu kutokea kwa tukio la Askari Polisi, Abati Benedicto kumjeruhi mtoto wake mwenye umri wa miaka 7 na kesi kufikishwa mahamani, kesi hiyo imefutwa kwa kinachodaiwa kuwa ni kukosekana kwa mashahidi wa kuthibitisha tuhuma zilizomkabili askari huyo aliyekua akifanya kazi kituo cha polisi Bariadi mkoani Simiyu.

Chanzo: Azam TV

==============

UPDATES...
Kwa wale wafuatiliji wa habari mbalimbali watakuwa wanakumbuka, juu ya tukio ambalo lilitokea Januari 15, 2023, la Askari namba H.4178 Abati Benedicto wa Kituo cha Polisi Bariadi kutuhumiwa kumpiga hadi kumjeruhi vibaya Mtoto wake mwenye umri wa miaka 7 (jina linahifadhiwa).

Tukio hilo lilianza kuripotiwa katika vyombo vya Habari Januari 20, 2023 ambapo Askari huyo alidaiwa kumjeruhi mtoto wake sehemu mbalimbali za mwili wake.

Tukio lilivyokuwa
Mtoto huyo anayesoma katika Shule ya binafsi ya Mjini Bariadi Mkoani Simiyu alifanyiwa ukatili wa kipigo na baba yake kwa madai kuwa hajui kusoma na kuandika.

Mtoto huyo alikutwa na majeraha sehemu za mgongo, kichwa na masikioni ambapo imeonekana pia alikuwa na majeraha makubwa ambayo ni mapya na mengine ya muda mrefu.

Wakati wa mahojiano na waandishi wa Habari akiwa amelezwa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwa ajili matibabu, mtoto huyo alidai alikuwa anapigwa na baba yake kwa kutumia waya wa pasi na wakati mwingine kumchoma na pasi yenye moto.

Baada ya tukio hilo kuripotiwa Polisi, mtuhumiwa alikamatwa kisha kufikisha Kituo cha Polisi Bariadi na Januari 23 Jeshi la Polisi lilijitokeza mbele ya waandishi wa Habari na kusema kuwa aliyefanya kitendo hicho ni Askari Polisi.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu wakati huo, Blasius Chatanda ilieleza kuwa ni kweli Baba wa mtoto aliyefanya ukatili huo ni Askari wa jeshi hilo, katika Kituo cha Polisi Bariadi na anashikiliwa jeshi hilo.

Ilieleza kuwa tarehe 15/1/2023, saa 11:00 katika kambi ya Kituo cha Polisi Wilaya ya Bariadi, Askari wa Jeshi la Polisi namba PC H.4178 Abati Benedicto Nkalango (27) alimshambulia mtoto wake aitwaye Benedicto Abati (7) mwanafunzi wa Shule ya Msingi Gappa kwa kumpiga na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha makubwa.

photo_2023-06-22_15-09-02.jpg

Askari namba H.4178 Abati Benedicto wa Kituo cha Polisi Bariadi anaetuhumiwa kumpiga hadi kumjeruhi vibaya mtoto wake mwenye umri wa miaka 7 akitoka mahakani kusikiliza kesi yake.

Mahakamani
Februari 17, 2023 Askari huyo alifikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili, ambapo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bariadi mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Mariam Nyangusi, mtuhumiwa alisomewa mashtaka yanayomkabili na mwendesha mashtaka wa Serikali Daniel Masambu ambayo ni kufanya ukatili dhidi ya Mtoto.

Kesi hiyo namba 8/2023 ikisomwa kwa mara ya kwanza mwendesha mashtaka akieleza Mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa Januari 15, 2023 katika eneo la 'Line Polisi', Mtaa wa Malambo mjini Bariadi.

Masambu alieleza kuwa mtuhumiwa alimchapa mtoto wake kwa fimbo na kumjeruhi maeneo mbalimbali ya mwili wake kinyume na kifungu Cha 169 A kifungu kidogo Cha 1 na Cha 2 Cha Sheria ya kanuni ya adhabu sura 16 marejeo ya mwaka 2022.

Hata hivyo mtuhumiwa alikana kosa hilo, huku mwendesha mashitaka akielezea Mahakama kuwa upelelezi umekamilika na kesi hiyo kupangwa kuanza kusikilizwa hoja za awali March 2, 2023.

Kesi kufutwa
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mashitaka Mkoa wa Simiyu, ilieleza kuwa kesi hiyo ilifutwa mahakamani Mei 22, 2023, baada ya mashahidi kushindwa kujitokeza mara tatu mfululizo.

Ilielezwa kuwa kesi hiyo iliitwa mara 8 mahakamani kabla ya kufutwa, ambapo Ofisi ya Mashitaka ilipeleka Polisi Hati 3 za kuitwa shaulini (Samas) mashahidi wa kesi hiyo.

Ofisi hiyo ilieleza kuwa Hati zote 3 zilijibiwa na jeshi la polisi, kuwa mashahidi wanaohitajika hawapo Bariadi na hawajulikani walipo, ndipo kesi ikafutwa.

Katika Hati hizo, Mashahidi waliokuwa wanatafutwa ni Mtoto, mama mzazi wa mtoto, pamoja na Mama mlevi (mama wa kambo) wa mtoto ambaye alikuwa akiishi na mtoto wakati akipigwa.

Kilichobainika
Uchunguzi uliofanyika umeonyesha kuwa majibu yote yaliyotolewa ni Jeshi la Polisi yalikuwa ya uongo, kwani mashahidi wote watatu hakuna ambaye alitoweka na wote walikuwepo na mpaka sasa wapo mjini Bariadi.

Imebainika kuwa Jeshi la Polisi liliamua kwa maksudi kuharibu kesi hiyo kwa kutopeleka mashahidi Mahakamani, likiwa na lengo la kumlinda Askari wake asichukuliwe hatua.

Mbali na hilo baada ya kesi kufutwa, Askari huyo alipewa uhamisho na kupelekwa katika Wilaya ya Meatu mkoani hapa.

Tulimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa, Edith Swebe kuzungumzia madai hayo, ambapo alisema wao kama jeshi la polisi hawawezi kuingilia maamuzi ya mahakama.

“Suala la mashahidi kupelekwa mahakamani au kutokupelekwa hilo lipo uko mahakamani sisi hatuhusiki, Ofisi ya mashitaka na Mahakama wao watakuwa wanajua, kazi yetu ni kukamata na kumfikisha mahakamani mtuhumiwa” alisema Swebe…

Kamanda Swebe alikiri Askari huyo kuhamishwa akieeleza kuwa “ hizo zilikuwa taratibu zetu za jeshi katika kumuonya kwa kitendo alichokifanya na tulimpa onyo akirudia tena atachukuliwa hatua zaidi ya hizi”.

Wazazi/walezi wa mtoto wanena
Madai ya kuwa Mama mazazi wa mtoto, mtoto mwenyewe kuwa hawajulikani walipo, yanapingwa na Mama wa mtoto huyo, Bibi yake pamoja na Babu wa mtoto, ambao wanataka haki itendeke.

Rehema Kaliwa mama wa mtoto anasema kuwa mtoto wake tangu amefanyiwa ukatili na Baba yake (walishatengana) mwanae anaishi kwa Babu na Bibi yake katika mtaa wa Malambo mjini Bariadi.

"Wanadanganya ni wahongo sana, hatujawahi kupokea barua yeyote ambayo inatutaka kwenda mahakamani kutoa ushahidi, yaani tukipata hiyo barua hata leo Mwandishi tunaenda, mtoto yupo tena hapa hapa mjini, mimi nipo na baba na bibi yake wote wapo”…

“ Kwanza hatujui hiyo kesi kama ilikwenda mahakamani, sisi tulisikia kwenye vyombo vya habari kuwa Baba wa mtoto kapelekwa mahakani, lakini hakuna mtu ambaye amekuja kututafuta twende mahakamani wala barua” alisema Rehema.

Naomi John Bibi wa mtoto huyo ambaye anaishi naye kwa sasa, anasema siku zote mtu mnyonge kupata haki inakuwa ngumu kama ambavyo imewatokea wao ambapo wanawaomba viongozi wa mkoa na Wizara kuingilia kati suala hilo.

Naomi anasema kuwa mjukuu wake anaishi naye muda mrefu na alikabidhiwa na maofisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wakiwepo na jeshi la polisi, ambapo anashangaa kusikia mtoto na mama hawapo.

“Hatujawahi kuona mtu yeyote anakuja hapa anamtaka mtoto tumpeleke mahakamani, hata mama yake yupo kila siku hapa, baba wa mtoto baada ya kutoka mahabusu alikuwa anaonana na mtoto kila siku shuleni, iweje leo waseme mtoto hayupo?” anahoji Naomi.

Naye Ramadhani Kisija Babu wa mtoto anaiomba serikali kuwasaidia haki iweze kutendeka kutokana na kitendo kilichofanywa na askari huyo kwa mjukuu wao kuwa cha kinyama.

“Huyu mtoto anaongea kila kitu ambacho alikuwa anafanyiwa, na walijua wakimpeleka mahakamani ataongea kila kitu, na Baba yake atafungwa, sasa waliona wadanganye ili kesi ifutwe, sisi wenyewe hatujui lini ilifutwa, lini ilipelekwa mahakamani na kama wakitaka mashahidi hata leo tupo tayari,” alisema Ramadhani.

Ustawi wa jamii.
Ofisa ustawi wa jamii Halmashauri ya Mji wa Bariadi Siwema Chungu, anasema kuwa wao kama moja ya watu wanaohusika kwenye jambo la mtoto huyo waliitwa polisi kwa ajili ya kutoa ushahidi.

Chungu anaeleza kuwa tangu wametoa maelezo yao polisi hawajawahi kuitwa mahakamani nako kwa ajili ya kutoa maelezo juu ya tukio hilo, na wala hawakupewa taarifa kama kesi hiyo ilipelekwa mahakamani.

Afisa Ustawi wa jamii huyo anaeleza kuwa baada ya tukio, walimchukua mtoto kisha kumpeleka hospitali na baada ya kupona walimkabidhi mama mzazi mtoto huyo pamoja na Bibi na Babu yake.

Hata hivyo Chungu naye anakiri kuwa mtoto huyo na wazazi wake wapo Bariadi na hawajawahi kutoka au kukosekana endapo wangelihitajika.

“Wazazi na walezi wa mtoto wapo hapa mjini, ni wakazi wa hapa hapa mjini, sisi kila siku tunawasiliana nao na tunakwenda kila wakati nyumbani kumwangalia mtoto,” alisema Chungu.
 
Aisee,pazeni sauti hadi huyo askari afungwe!UKATILI dhidi ya watoto haukubaliki kamwe!
 
View attachment 2665388

Hivi kuna mtu anamwelewa vizuri huyu IGP wa sasa? Au zile roho za kikurya za kikatili kazipleleka kazini? Hao askari waliokuwa wanidanganya mahalama kwa kusaini uwongo nakuupeleka mahakamani kuwa mashahidi hawajulikani walipo wanafanya nini kazini mpaka leo? RPC Simiyu inaonekana anamlinda mhalifu. km IGP ameshindwa kuwawajibisha hao askari pamoja na RPC tunamwomba Amiri Jeshi Mkuu aingilie haki itendeke, huyo askari arudishwe mahakamani kesi isikilizwe mashahidi ndiyo hao wapo hapo Bariadi. Km jeshi la polisi linaficha uhalifu yaani unyama km huo itamlinda nani, RPC bila hata aibu eti tumemwonya, yeye ni mahakama, anajua kwa mujibu wa sheria alistahili adhabu ipi? Kwa hiyo RPC Simiyu ameshakuwa mahakama? Tunaomba haki itendeke na tupate mrejesho km wenye nchi hii.
 
Back
Top Bottom