"IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?

Pumzika mkuu, hutobadirisha misimamo ya watu kwa kuandika au kuzungumza hata kama ungekuwa na sauti kali au nene kama simba. Toa mchango wako, na endelea na maisha mengine.
Hutowea kushinda kwa kubishana humu. Humu tupo watu wa kila namna.
Lala pumzika na shemeji, akifurahi moyo wako unaimarika. Hata ukipumzika vizuri utaamka uko vizuri, na afya yako itaimarika.
Ubarikiwe sana.
Amen, nimefarijika sana na ushauri huu na haswa kuhusu ile part ya shemeji yako!.
P
 
Amen, nimefarijika sana na ushauri huu na haswa kuhusu ile part ya shemeji yako!.
P
Karibu sana kaka, maisha haya mafupi sana ,tujaribu kubalance. Ukishupaa shingo na vidole humu utajikuta hufanyi lolote lako binafsi, na hutokuwa na muda na mkeo au familia yako kwa ujumla.
Enjoy your life brother usizijali sana kelele za humu. Nafahamu kuna wakati unatoa majibu ya ufasaha unadhani wata ridhika nayo, lakini wanakuja kivingine. Wewe ni mmojo humu tuko wengi, hutoweza ku satisfy watu humu kwa majibu.
Andika atakaye soma na kuelewa aelewe, asiyetaka aache.
tafuta kitabu kimoja kinaitwa " The COURAGE TO BE DISLIKED. Tafuta amani ya moyo wako, achana na sisi usiotuona wala kutufahamu.
 
Wanabodi,
Mimi mwenzenu ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea pia kwa kujitolea, nimehudumu kwenye sekta ya habari kwa takriban zaidi ya miaka 30, hivyo jicho langu limeona mengi, lizania.

Paskali.
Ukisafiri wakati haya yanaendelea AUILE KAULI YA MAREHEMU JPM YA ASILI YA JINA LAKO NDO IMERUDI
 
Ukisafiri wakati haya yanaendelea AUILE KAULI YA MAREHEMU JPM YA ASILI YA JINA LAKO NDO IMERUDI
Naona Rais Magufuli alikuwa sawa alipo.uita Mr Njaa, he is using too much effort for nonissues. Magufuli angekuwapo angetupa translation ya Luhaga Mpina - naye anaenda hukohuko. Wameona kuna vacancy CHADEMA wanachangamkia tenda.
 
Watu Waafrika Weusi bado hawajastaarabika.
Wanaweza kufanya chochote wakati wowote bila kuthamini kizazi cha baadae.
Wao wanacho thamini ni Ugali tu. Ugali wao wa leo, TU Basi.
Case Closed.
 
Halafu badala ya kujibu hoja kwa hoja wa vipengele wao wanajibu kisiasa tu...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
... 'Kwa faida ya nani'... Hili swali namna ulivyolipachika kila paragraph kamwe hauwezi kupata majibu yake sahihi, maana kila kipengele kinagusa maslahi binafsi ya walioubuni na kuuingia.

Utakachoweza kupata hapa ni majibu ya chawa wapumbafu waliomwagwa Jf kupambana na hoja za great thinkers kama hizi kwa majibu mepesi ya kijinga.

Tangia mwanzo mwa sakata hili, waTz wote wenye mapenzi mema na nchi hii wakiwemo wanasiasa, wameuliza maswali hayo ya msingi, lakini hakuna kiongozi wa Serikali hata mmoja kuanzia Samia mwenyewe aliyekuja na jibu 'lililojaa' na la ukweli.

Hivyo kumaliza mwaka mzima bila ya kutolewa majibu ya maswali ya msingi ya mkataba huu ni kwamba nchi yetu sasa imeuzwa dhahiri na inaongozwa na genge la mibaka uchumi.

Nimesema haya kutokana na ninanyoona namna 'sura' nzima ya mhimili ya Serikali inayolilinda jambo hili bila ya kuwa na majibu.

Kwa hiyo utatu wa mhimili: (Serikali, Bunge na Mahakama) vyote vipo corrupted, wote walishashiba, hakuna mmojawapo anayeweza na atakayeweza kusimama na wananchi kukaripikia mkataba huu mbaya, maana wote hao kwa nafasi zao mmoja mmoja na familia zao ni wanufaika wa ubovu wa mkataba huu wa kiMangungo huku dhima na madhila yake yakilihusu Taifa na waTanganyika wote.

Vinginevyo, Rais asingekubali, Wabunge wasingekubali, mahakama zisingepindisha hukumu kwa kesi zinazofunguliwa ili kutafsiri uhalali wa mkataba huu.

Nini kifanyike sasa kwa sababu majibu ya... 'Kwa faida ya nani'... tulishayapata kutokana na ushahidi wa kimazingira?
 
Back
Top Bottom