Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Serikali yetu imekata shauri la kuleta na kutoa chanjo ya UVIKO kwa watanzania/wananchi wake. Imeweka wazi kabisa kuwa chanjo ipo na ni ya HIARI. Yaani, mtanzania atakayeridhia kuchanjwa atachanjwa.
Msimamo wa Serikali ni msimamo wetu watanzania. Serikali ni yetu na inatupasa kuiheshimu na kufuata uamuzi wake hasa ule ambao unagusa masuala ya afya na umetanguliwa na masuala ya kitaalamu.
Haipendezi na wala si jambo la kufurahiwa kuona mwananchi au kiongozi wa kiserikali, kisiasa au kidini akijitokeza hadharani kupinga na kukejeli chanjo ya UVIKO kama afanyavyo Askofu Gwajima. Askofu Gwajima ni kiongozi wa kidini na kisiasa.
Kuendelea kukosoa chanjo ya UVIKO hadharani kwa Askofu Gwajima ni kuonyesha jinsi anavyoikosoa hadharani Serikali na hata msimamo wa chama chake cha Mapinduzi kinachounda serikali husika. Lazima adhibitiwe kiserikali na kichama.
Kama kuna yeyote wa kupinga chanjo, afanye hivyo kwa kufaidi haki yake ya HIARI ya chanjo husika. Hakuna maana wala faida kujipambanua kwa umma na kuleta suitafahamu isiyo na mantiki. Serikali iheshimiwe!