benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza mkoani Tanga wakati akifungua kikao cha viongozi wa Dini pamoja na wadau wengine maendeleo kujadili mambo mbalimbali ikiwemo mikakati ya uhamasishaji na elimu kuhusu chanjo ya UVIKO 19 amesema zaidi ya Watanzania Milioni 11 wamepata chanjo ya UVIKO 19.
Waziri Ummy, ameeleza kuwa zaidi ya watu Milioni 11 kati ya Milioni 30.7 wamepatiwa Dozi kamili ya chanjo ya UVIKO 19 huku Serikali ikongeza vituo vya utoaji chanjo hadi kufikia 7,000 ndani ya miezi mitano kutoka vituo 550 vilivyokuwepo awali kitaifa.
Zoezi la chanjo ya UVIKO19 ambalo lilizinduliwa na Rais Samia Suluhu takribani mwaka mmoja uliopita limeonesha kuwa na mapokeo chanya kutoka kwa sehemu kubwa ya Watanzania.