Kenya 2022 General Election

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,986
photo1660576172.jpeg
Tume ya Uchaguzi Huru na Mipaka (IEBC) imemtangaza aliyekuwa Naibu Rais, William Ruto (55) kuwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano kwa tiketi ya Chama cha UDA kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 9, 2022

Tume imesema Ruto amepata Kura 7,176,141 sawa na asilimia 50.49 huku akifuatiwa na Raila Odinga kutoka Chama cha Azimio la Umoja

Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati ametangaza matokeo hayo baada ya siku sita za kuyasubiri tangu siku iliyopigwa kura, Agosti 9, 2022.

Ruto amewashinda wagombea wenzake ambao ni Raila Odinga, mgombea wa Chama cha Agano, David Waihiga ambaye Agosti 14 alitangaza kushindwa, pamoja na Profesa George Wajackoyah wa Chama cha Roots.

William Ruto (UDA)
50.49%
7,176,121 Votes

Raila Odinga (AZIMIO)
48.85%
6,942,930 Votes

George Wajackoyah (RPK)
0.44%
61,969 Votes

David Waihiga (AGANO)
0.23%
31,987 Votes
 
15 August 2022
Bomas
Nairobi, Kenya


IEBC Chairman Wafula Chebukati, mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi - IEBC



Mwenyekiti wa IEBC Bw. Wafula Chebukati , makamishna na watumishi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka -IEBC aelezea waliyoyapitia katika kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi huu wa 2022 ikiwemo watumishi kutishiwa, makamishna wawili kujeruhiwa n.k lakini kwa vile yeye Wafula Chebukati na watumishi wa IEBC walikula kiapo kusimamia uchaguzi basi pia ni wajibu wao kuhitimisha zoezi la kutangazwa kwa mshindi wa urais pamoja na changamoto zote .
 
Kupambana na Ruto sio kwenye majukwaa tuu lakini hata kwa wizi hawamuwezi ingawa najua wizi safari hii hajafanya ila Ruto wakati wa Moi alipachika watu Kenya nzima idara nyeti ili walinde maslahi yake akijua siku moja atagombea urais na anavyoijua Kenya angeweza hujumiwa. Ruto ni Hustler sio mchezo.
 
Hongera nyingi kwake. Na pole nyingi kwa Raila Odinga! Maana hatakuwa tena na nafasi ya kutimiza ndoto zake. Ni wakati wake sasa kupumzika na kucheza na wajukuu zake.

Wakenya wameamua kuondokana na utawala wa kikoo! Naamini siku moja na sisi tutaondokana na utawala wa CCM.
 
Back
Top Bottom