'Idi Amin Hakuwa Muuaji, Mla Nyama za Watu' - Rais wa Venezuela

kitu kimoja alichofanya amin ambacho nimekipenda ni kuwatimua mafisadi wa kihindi ambao walikimbilia Tanzania.
 
Wewe usitake kujifanya mjuaji wakati hujui unalosema. Hiyo clip ya hapo juu haijatoka kwenye filamu ya The Last King of Scotland au The Rise and Fall of Iddi Amin. Tumeliona jua kabla yako kaka!

Mnafiki mkubwa we! Huna ukubwa wala uzee.! Idd Amin hakuwa mbaya au katili kama wewe, marehemu baba yako wa Taifa, na wadanganyika wenzako mlivyotuaminisha. Mie nimekaa sana Uganda, yote mliokuwa mkiyazusha kuhusu Amin Waganda wanakana kabisa, wanasema vita ilianzishwa na Babu akitaka kumrudisha Obote madarakani, Babu alipeleka mamluki Uganda hasa kwenye vyombo vya usalama na majeshi ili wampindue Amini. Babu a.k.a Nierere ndo chanzo kikuu cha vita vya Kagera.
 
Mnafiki mkubwa we! Huna ukubwa wala uzee.! Idd Amin hakuwa mbaya au katili kama wewe, marehemu baba yako wa Taifa, na wadanganyika wenzako mlivyotuaminisha. Mie nimekaa sana Uganda, yote mliokuwa mkiyazusha kuhusu Amin Waganda wanakana kabisa, wanasema vita ilianzishwa na Babu akitaka kumrudisha Obote madarakani, Babu alipeleka mamluki Uganda hasa kwenye vyombo vya usalama na majeshi ili wampindue Amini. Babu a.k.a Nierere ndo chanzo kikuu cha vita vya Kagera.
(Proverbs 26:4) Do not answer anyone stupid according to his foolishness, that you yourself also may not become equal to him.

PS: Wewe ni ngosha gani uliyejaa pumba namna hii?
 
Baada ya Obote, ambaye alikuwa ni rafiki yake mkubwa na Nyerere kutimuliwa Uganda na Idd Amin, alikuja Tanzania kuchukua hifadhi. Hapo ndipo chokochoko ilipoanza huku vijana wa Ugananda waliokuwa Tanzania wakipewa mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya maandalizi ya vita. Miongoni mwa vijana hao ni rais wa sasa wa Uganda Yoweri Museven. Ni wakati huu ambapo Nyerere alikuwa anatumia propaganda chafu kuchafua jina la Idd Amin kwa kuwaaminisha watanzania kuwa mtu huyo alikuwa katili, na muuaji mkubwa. Hilo lilifanikiwa kwa watanzania kujenga chuki kwa rais huyo wa Uganda. Hata hivyo kwa wakati huo tayari uganda ilikuwa imepiga hatua kubwa sana ki uchumi. Katika hospitali za nchi hiyo kulikuwa na Televishen tena za rangi kila wodi kwa ajili ya wagonjwa. Miundombinu ilikuwa imara na huduma za jamii zilikuwa zikipatikana kwa urahisi. Ni wakati ambapo vikosi vya vijana wa Uganda vilivyokuwa upande wa Tanzania vikijulikana kwa jina la FRONASA chini ya uongozi wa Yoweri Museveni Vikaanza kufanya uchokozi kwa kuvuka mpaka na kwenda kufanya uhalifu upande wa Uganda. Mara kadhaa Amin alilalamika bila mafanikio. Ndipo alipotuma kikosi chake maalumu cha Marile troop kilichokuwa kikiongozwa na gen Oyite kuja kuwasaka wapiganaji wa FRONASA. Ndipo Nyere alipopata sababu ya kuingia Uganda.
 
@juma kidoto mbona museven likuja kupindua serikali iliyowekwa na nyerere uganda
 
Hivi kuna watu wanaamini amini alikuwa anakula nyama za watu .. sawa alikuwa dikteta ... Lakini kuamini alikuwa anakula nyama za watu ni akili mbayumbayu hizo ...

Sent from my HTC Incredible S using Tapatalk
 
Hivi kuna watu wanaamini amini alikuwa anakula nyama za watu .. sawa alikuwa dikteta ... Lakini kuamini alikuwa anakula nyama za watu ni akili mbayumbayu hizo ...

Sent from my HTC Incredible S using Tapatalk
naona mbwembwe kibaaao..siku utasahau utaandika sent from limousine,cardillac,jaguar,etc
 
wananchi wa Libya wanamkumbuka Gadafi sasa kwa mambo kama kumchafua mtu ili aonekane hafai na muuaji. Chavez yuko sawa proganda nyingi zilitengenezwa na Obotte na Nyerere ili kusimamisha kanisa Catholic Afrika mashariki na kuua umoja wa kiiskam ulioanza kukita mizizi ktk ukanda wa Afrika mashariki huku Idd Amin akiongoza harakati. Nawapenda sana Gadaf, Mugabe na Idd Amin kwani ndio viongozi shupavu hapa Afrika, wengine takataka.
 
3608254.jpg

Rais wa zamani wa Uganda Idi Amin Tuesday, November 24, 2009 6:49 PM
Rais wa Venezuela, Hugo Chavez amewaudhi maafisa wa serikali ya Uganda kwa kauli yake ya kudai kuwa rais wa zamani wa Uganda Idi Amin hakuwa muuaji na mla nyama za watu kama inavyosemekana. Rais wa Venezuela, Hugo Chavez amewaudhi maafisa wa serikali ya Uganda kwa kumtetea rais wa zamani wa Uganda Idi Amin kuwa hakuwa muuaji na mkatili kama inavyojulikana duniani.

"Tulifikiria kuwa Amin ni muuaji mla nyama za watu" Chavez alisema alipokuwa akimuongelea Idi Amin ambaye anatuhumiwa kuwaua mamia ya wapinzani wake wakati wa utawala wake nchini Uganda kwenye miaka ya 1970.

"Nina shaka kama Idi Amin alikuwa muuaji kama inavyosemekana, badala yake alikuwa mwanaharakati mtetezi wa nchi yake", alisema Chavez.

Ingawa hakuna idadi kamili ya watu waliouliwa wakati wa utawala wa Idi Amin kuanzia mwaka 1971-1979, inakadiriwa kuwa watu 500,000 waliuliwa wakati huo.

Mary Karoro Okurut, msemaji wa chama tawala cha Uganda akizungumzia kauli hiyo ya Chavez alisema kuwa mtu yoyote anayedhania kuwa Idi Amin alikuwa ni mtu mwema atakuwa na matatizo ya akili.

"Idi Amin alikuwa ni mtu mkatili ambaye aliua raia wengi wa Uganda na kisha kukimbilia nje ya nchi. Mtu yeyote anayemtetea Amin atakuwa na matatizo".

Naye sekretari wa rais Yoweri Museveni, Tamale Mirundi, alielezea rekodi ya Idi Amin ya kuwaua wapinzani wake akiwemo mmoja wa wake zake.

"Kama unamuoa mwanamke na kisha baadae unamuua, huwezi kuitwa mume mzuri", alisema na kuongeza "Hivyo ndivyo alivyofanya Amin, aliwaua raia wengi wa Uganda hawezi kuitwa mtetezi wa nchi".

Kumekuwa na mitazamo tofauti kuhusiana na Idi Amin baadhi ya watu wakiamini kuwa ukatili anaotuhumiwa kuufanya zilikuwa ni propaganda za kumchafua huku watu wengi wakiendelea kuamini kuwa Idi Amin ndiye mhusika mkuu kwa mauaji ya watu 500,000.

Miongoni mwa mambo ya kikatili ambayo Idi Amin anatuhumiwa kuyafanya ni kuwaua watu na kula nyama zao na kuhifadhi nyama za watu kwenye majokofu.

Maafisa wa serikali ya Uganda hawajasema chochote kama watachukua hatua zozote za kidiplomasia dhidi ya Venezuela.

Venezuala haina ubalozi wake nchini Uganda.
'Idi Amin Hakuwa Muuaji, Mla Nyama za Watu' - Rais wa Venezuela

ukweli ni huo aliosema Chavez. Idd Amin hakuwa muuwaji wala hakuwahi kula nyama ya binadamu. Ni uongo na propaganda chafu za wapinzani wake akiwemo raisi wa sasa wa Uganda. Nimewahi kuongea na vijana wa zamani wakati wa Idd Amin ambao sasa ni wazee wamethibitisha kwamba jamaa alikuwa mzalendo wa kweli aliyetaka kila mganda kumiliki njia kuu za uchumi na rasilimali za nchi yake badala ya wageni (Wahindi). Leo hii Uganda wanalia, uchumi unamilikiwa na wageni wao wakibaki kuwa vibarua! Nitaweka link bdae inayoeleza tofauti ya Amini, Obote na Mu7.
 
wananchi wa Libya wanamkumbuka Gadafi sasa kwa mambo kama kumchafua mtu ili aonekane hafai na muuaji. Chavez yuko sawa proganda nyingi zilitengenezwa na Obotte na Nyerere ili kusimamisha kanisa Catholic Afrika mashariki na kuua umoja wa kiiskam ulioanza kukita mizizi ktk ukanda wa Afrika mashariki huku Idd Amin akiongoza harakati. Nawapenda sana Gadaf, Mugabe na Idd Amin kwani ndio viongozi shupavu hapa Afrika, wengine takataka.

mia mkuu! Unayosema ndio hayo Waganda wanayosema kuwa Uganda haijapata raisi mzalendo kama Amini. Ni propaganda za Uingereza na majirani wa Uganda ndio waliozusha uongo huo! Kila mtu ana mapungufu yake, na Amin hakukamilika lakini si kwa kiwango kama tunavyolazimishwa kuamini.
 
Kama kuna jambo la maana alillo lifanya ni kuwafukuza wahindi na waarabu Uganda,tunahitaji spirit kama hizi katika kuchukua maamuzi magumu bila kujali wengine watasemaje.
 
hizo zilikuwa siasa za Tanzania ili wapate sababu ya kumpiga. tanzania walitumiwa tu. kanisa kubwa east africa la katoriki ilikuwa lijengwe Uganda but Amin akaweka vikwazo so ili mpango wao utimie alitakiwa atoke. alikua mkatili kama viongozi wote wa africa walivyo lakini si kwa kiasi ambacho wanasema wabaya wake.
 
naona mbwembwe kibaaao..siku utasahau utaandika sent from limousine,cardillac,jaguar,etc

Kaka ingia duniani tumia tapatalk .. utajua kwamba si Mimi ninaye andika .. maandishi yakuwepo yenyewe btw hata kama ningekuwa naandika Mimi do u have any problem with that ..?

Sent from my HTC Incredible S using Tapatalk
 
Kwa jinsi nilivyoshuhudia propaganda za aljazeera, cnn, bbc na vyombo vinginevyo,kwamba ghadafi kaua waandamanaji 6000 kwa ndege, kumbe ni uwongo, na then ninavyoona ugaidi unaofanywa na baadhi ya mataifa halafu yakasingizia upande wa pili basi ninashawishika kwamba iddi amini alisukiwa zengwe ili aondoke!

Iddi amini alimess na wayahudi kwa kusappoti kwake palestina,(mnakumbuka raid of entebbe)
iddi amini aliwafanya wazungu wambebe kama mfalme, nadhani hii pia wazungu walimmaindi kinyama
nyerere alikuwa akisapoti vikundi vya waasi, kina museveni waliopiga kambi nchini tanzania ili wamng'oe amini, na wanajeshi wa amini walipofanya mutiny wakakimbilia tanzania, ambayo haikuwaarrest, iddi amini akawafuatia huko huko ndani ya ardhi ya tanzania.

Kwa maadui wote hawa aliojijengea, lazima coordination kati ya wazungu na tanzania kumg'oa amini ilikuwa possible, ndiyo maana securty council halikuitisha ceasefire, na wala halikupitisha azimio la kumaliza mgogoro kwa amani. Kwa hiyo ni dhahiri zengwe la propaganda za kuua watu 500,000 lilikuwa lazima lisukwe tu kulegitimize invasion!.
 
Kwa jinsi Chavez alivyo na roho nyeusi ni lazima aone aliyoyafanya Amin ni kawaida sana.
 
chavez ni kichaa-kichwa yake inamatatizo-anatakiwa afanyiwe uchunguzi wa akili yake,maana matamko yake anayoyatoa mengi huwa ni ya kipumbavu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom