'Idi Amin Hakuwa Muuaji, Mla Nyama za Watu' - Rais wa Venezuela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Idi Amin Hakuwa Muuaji, Mla Nyama za Watu' - Rais wa Venezuela

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Nov 26, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,221
  Likes Received: 4,013
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais wa zamani wa Uganda Idi Amin Tuesday, November 24, 2009 6:49 PM
  Rais wa Venezuela, Hugo Chavez amewaudhi maafisa wa serikali ya Uganda kwa kauli yake ya kudai kuwa rais wa zamani wa Uganda Idi Amin hakuwa muuaji na mla nyama za watu kama inavyosemekana. Rais wa Venezuela, Hugo Chavez amewaudhi maafisa wa serikali ya Uganda kwa kumtetea rais wa zamani wa Uganda Idi Amin kuwa hakuwa muuaji na mkatili kama inavyojulikana duniani.

  "Tulifikiria kuwa Amin ni muuaji mla nyama za watu" Chavez alisema alipokuwa akimuongelea Idi Amin ambaye anatuhumiwa kuwaua mamia ya wapinzani wake wakati wa utawala wake nchini Uganda kwenye miaka ya 1970.

  "Nina shaka kama Idi Amin alikuwa muuaji kama inavyosemekana, badala yake alikuwa mwanaharakati mtetezi wa nchi yake", alisema Chavez.

  Ingawa hakuna idadi kamili ya watu waliouliwa wakati wa utawala wa Idi Amin kuanzia mwaka 1971-1979, inakadiriwa kuwa watu 500,000 waliuliwa wakati huo.

  Mary Karoro Okurut, msemaji wa chama tawala cha Uganda akizungumzia kauli hiyo ya Chavez alisema kuwa mtu yoyote anayedhania kuwa Idi Amin alikuwa ni mtu mwema atakuwa na matatizo ya akili.

  "Idi Amin alikuwa ni mtu mkatili ambaye aliua raia wengi wa Uganda na kisha kukimbilia nje ya nchi. Mtu yeyote anayemtetea Amin atakuwa na matatizo".

  Naye sekretari wa rais Yoweri Museveni, Tamale Mirundi, alielezea rekodi ya Idi Amin ya kuwaua wapinzani wake akiwemo mmoja wa wake zake.

  "Kama unamuoa mwanamke na kisha baadae unamuua, huwezi kuitwa mume mzuri", alisema na kuongeza "Hivyo ndivyo alivyofanya Amin, aliwaua raia wengi wa Uganda hawezi kuitwa mtetezi wa nchi".

  Kumekuwa na mitazamo tofauti kuhusiana na Idi Amin baadhi ya watu wakiamini kuwa ukatili anaotuhumiwa kuufanya zilikuwa ni propaganda za kumchafua huku watu wengi wakiendelea kuamini kuwa Idi Amin ndiye mhusika mkuu kwa mauaji ya watu 500,000.

  Miongoni mwa mambo ya kikatili ambayo Idi Amin anatuhumiwa kuyafanya ni kuwaua watu na kula nyama zao na kuhifadhi nyama za watu kwenye majokofu.

  Maafisa wa serikali ya Uganda hawajasema chochote kama watachukua hatua zozote za kidiplomasia dhidi ya Venezuela.

  Venezuala haina ubalozi wake nchini Uganda.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3608254&&Cat=2
   
 2. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Viongozi wengi wa africa na duniani kote ni wauaji na especially inapotokea kuna upinzani. Hivyo hata Idd Amin lakini among those waliofanya uuaji. Lakini inatakiwa taarifa itolewe bila kuegemea upande wowote. Kwani hata hao waganda wenyewe hawana record exact kuwa jamaa aliua watu wangapi na kwanini.

  Wanahisi tu ambacho ni kitu kibaya. Chavez kasema inatakiwa kumuuliza kwanini alisema hivyo? Maana huwa kuna watu wengi wemezuliwa mambo mpaka yakazidi mpaka mfano Saddam Hussein na wengine wengi tu wapo.

  Hiyo ufanyika kama umeenda against interests za watu fulani. Hivyo tujiulize kipindi cha amini hakukuwa na watu wanainterest na uganda? If so kama alikuwa muuaji wa kiasi hicho kwanini alipewa ukimbizi wa kiasa?
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hugo Chavez is an idiot and a fool. Waliyo ishi na kupitia kipindi hicho cha Idi Amin wana jua uchungu na maumivu yake. Now I'm starting to think that this guys enjoys saying things he knows will be different from others. Yani yeye watu wakienda kulia yeye ni lazima aende kushoto.
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Idi Amin hakuwa kiongozi mzuri, lakini hakuwa cannibal kama tulivyokuwa tunasema Tanzania. Kama ni uuaji na ukatili, he was less cruel than Obote lakini ajbu ni kuwa kutokana na kuwa Obote alikuwa rafiki yetu hatukumchafua kama alivyochafuliwa Idi Amin. Hapa kwetu Tanzania kunacannibals lakini hata hawasemwi.

  Inawezekana kuwa Chavez ni Idiot lakini anayosema yana ukweli fulani.
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu kasema Idi Amin hakua muuaji. Is he serious? Hata kama kulikua na wauaji zaidi yake ni upumbavu kusema this guy was not a killer.
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  No doubt he was a killer, Chavez does not know the murders he committed.

  Kama anasema he was not a killer inawezekana hajui kabisa kilichotokea.
   
 7. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika mambo yaliyokwishawahi kuhusishwa na Unyama aliofanya Idd Amin akiwa rais wa Uganda ni ule wa kuwakusanya Vilema nchini Uganda kwa ma-tipper lorries na kwenda kuwamwaga kwenye mto Nile. Vyombo vingi vya habari kipindi hicho vikiwamo vya Tanzania vililishikilia bango sana jambo hili.

  Sasa wanajamvi, ningependwa kujuzwa ukweli kuhusu jambo hili maana wakati wa Nyerere ilikuwa ni vigumu kusikia kutoka upande wa pili maana vyombo vyote vilitakiwa viandike mambo anayoyapenda yeye tu.
  Na kama hilo ni kweli, The hague ilikuwa wapi kipindi hicho, au haikuwapo! Mbona hatujawahi kusikia akishtakiwa kwa hilo!

  Naomba kuondolewa tongotomgo kwenye hili.

  Nawasilisha
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,569
  Likes Received: 21,084
  Trophy Points: 280
  mimi kuhusi iddi amin
  najiuliza kwa nini tanzania haikupewa kibali cha united nation wala oau
  kuingia vitani?????/
   
 9. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,849
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Iddi Amini ni kweli alikuwa ni Dikteta, Lakini tunasema adui mpe jina baya hivyo sifa zingine ni za kupamba ubaya wake zaidi.
   
 10. Dumelang

  Dumelang JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 2,079
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Vita inakwenda na Propoganda alikuwa Dikteta ila kuna vitu hufanywa mapambio ili kumjengea mtu chuki zaidi machoni pa watu, sera za hivi zili fanywa sana na viongozi waliokuwa wakiamini katika ujamaa, Si Idd Amini peke yake wapo watu wengi, wengine ni watanzania enzi hizo waliimbwa mashuleni na wanafunzi kuhamasisha ubaya wao, waliimbwa na chipukizi,,,watu wakawachukia bila hata kuwafahamu.

  Watafute wazee na watu wa makamo au wajeshi waliopigana vita hii wajuao vema siasa za mzee Julius watakwambia. lakini pia Fuatilia sana vitabu vya historia ambanyo aviko hadharani, kuhusu Tanganyika-tanzania utapata sera nyingi mbovu za mzee Kambarage bila shaka waweza hata mchukia.
   
 11. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,838
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  hbu FF aje atuambie mana huwa anajikuta pioneere
   
 12. A

  Albimany JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Mimi i nilikutana na jamaa mmoja kutoka Sirlanka katika kufahamishana ninako toka nikamwambia East afrika akaniambia anakusikia Uganda kulikua Kiongozi ( Amini) alikua anakula nyama za watu walivyosikia wakati hule wavita.
   
 13. J

  Jonathan Kiula JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 317
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ningependa(siyo ningependwa)! the most of scandals were created and propagated by senior Jk
   
 14. J

  Jonathan Kiula JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 317
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kuhusu(siyo kuhusi),,united nations(siyo united nation)
   
 15. J

  Jonathan Kiula JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 317
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  there you are,kwenye mchakamchaka tuliimba sana ubaya wa Kambona bila kujua ukweli
   
 16. J

  Jonathan Kiula JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 317
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  srilanka(siyo sirlanka),ule(siyo hule),wa vita(siyo wavita)
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Oct 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 56,877
  Likes Received: 19,400
  Trophy Points: 280
  Hiki ndicho kilimponza Idi Amin:
  [​IMG]
  How can a slave be a master? wakatumwa Waafrika wenzake kummaliza.

  Ni mengi tu yaliyoandikwa kuhusu Idi Amin ni uongo, si hilo tu la vilema.
   
 18. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,367
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Mkuu umeleta maada ambayo imenikumbusha huko nyuma wakati nipo at the hill kuna kozi moja upande wa PS tulikuwa tunazungumzia leadership.
  Mwendesha kozi prof. akatoa mfano wa Idd Amin kuwa ni moja kati ya madikiteta waliwaikuwepo basi mimi nikagonda meza na kuamsha mkono nakusema its not true may he was a dictator in TZ but not in Uganda then also Kambarage was a dictator.
  Duh nilicho ambulia ni kuitwa siyo mtanzania,msaliti haya maneno nikutoka kwa wanafunzi wengine wakadiliki kusema eti mimi ni mganda.
  Zogo lilipo endelea prof. akaingilia na akanipa nafasi nikasema hivi ukienda Uganda wanakuambia Amin was a hero nakasema tena watz wanasema Kambarage hakuwa dictator kwasababu there is no real documents and bad conducts that are written on Nyerere mfano ukimuuliza Shivji kitabu chake cha Silent Class Struggle,Chake2 alikiandika lini na kwanini hakikuwa published wakati huo aliotaka?
  Historia nyingi zinakuwa too subjective ndo maana hadi leo watanzania hawana maandishi yanayoelezea mapungufu na udikiteta wa Kambarage etc Maandishi mengi yanaongelea MYTH kuhusu Amin.
   
 19. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hakuna ukweli wowote ni porojo tu za watanzani. Juzi tumisikia eti Igunga kuna makomando wameletwa, wewe unadhani hii kama mpita njio sio mtanzania kasikia hiyo kauli si anaipeleka kwao!
  Idd Amin, ana mabaya yake lakini mengi wamemsingizia mara anakula moyo wa binadamu
   
 20. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #20
  Oct 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 640
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  ingawaje waswahili wanasema lisemwalo lipo lakini wakati mwingine ni propaganda tu.Kuhusu Nyerere ni mengi ambayo ni mabaya yake hayakuandikwa na kwa unafiki wa watz hata ukiyaandika watakupuuza tu
   
Loading...