Kwanini baadhi ya watu humtaja Idd Amin kama mzalendo? Soma hapa...

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,224
22,303
Kila binadamu ana pande zake mbili, ubaya na uzuri, kwa hiyo hata Amin naye alikuwa na mazuri yake ingawa yanafunikwa na maovu yake. Kama ilivyokuwa kwa wazalendo wengine wa kiafrika waliopata kuongoza nchi zao miaka ile baada ya uhuru Amin naye alikuwa ni mtu wa kutaka maendeleo ya haraka. Hili halipingiki. Amin anatajwa kuweka alama nyingi kwenye miundombinu ya Uganda hasa upande wa jeshi. Hakuwa mtu wa maneno mengi.

Pia Amin hakuwa mtu wa kujilimbikizia mali kama ilivyo kwa viongozi wengi wa kiafrika. Hakuna popote pale Amin anatajwa kuhusika na ufisadi na kujilimbikizia mali. Pamoja na ukatili wake sijaona akituhumiwa kuhusika na ufisadi wala kujilimbikizia mali. Amin yuko kwenye kundi moja viongozi wachache waliowahi kuongoza bila kujilimbikizia mali kama vile hayati Nyerere na Sankara. Kuna madikteta waliokuwa makatili vilevile mafisadi kama vile Mobutu na Bokassa.

Amin ni miongoni mwa viongozi wachache sana barani Afrika aliyekuwa haogopi kuwapa za uso mabeberu. Alikuwa ni mwiba mkali kwa mabeberu hasa alipoupata uenyekiti wa AU. Hapa anakaa kundi moja na Gadafi, Mugabe, Sankara, Nyerere na wazalendo wengine wachache.

Tukiziangalia pia namba huenda Amin kaua watu wachache kwasababu yeye alikuwa anamfuata mbaya wake tu na kumpoteza tofauti na viongozi wengi ambao kosa la mtu mmoja linaweza likapoteza kijiji kizima. Kwa mfano dikteta Mobutu aliwaua wanafunzi wengi wa Chuo Kikuu Lubumbashi kisa tu kuandamana. Hata viongozi wanaotajwa kuwa wa kidemokrasia wameshawahi kuhusika na mauaji mengi ya raia wasio na hatia kwasababu ya kuwa na itikadi tofauti. Amin yeye alikuwa anadili na mhusika mkuu. Ingawa sababu hii haimfutii makosa yake ila kwa namba Amin ana unafuu kuliko inavyotajwa.

Pamoja na mazuri yake bado Amin alikuwa mpuuzi kujitengenezea maadui wa ndani. Huwezi kuwaua watu wako ukabaki salama. Wazalendo karibu wote hawajawahi kudumu madarakani kwa upumbavu wa kuwabana sana raia wasiwe na mawazo tofauti hali inayopelekea upinzani wa kichinichini na mwisho wake huwa ni mapinduzi au kiongozi kuuwawa. Haiwezekani nchi nzima watu wakafanana mawazo.
 
Kitendo cha kuwafukuza wahindi mpaka leo ukienda Kampala wafanyabishara ni Waganda wenyewe, hii imekaa vizuri.

Isitoshe ubaya mwingi wa Idd Amin ni propaganda za Nyerere tu na zamani watu hawakuwa na access ya kupata taarifa ambazo ni independent, unategemea RTD kupata taarifa sasa kina Ben Kilo watatangaza habari gani?
 
Back
Top Bottom