'Idi Amin Hakuwa Muuaji, Mla Nyama za Watu' - Rais wa Venezuela

wananchi wa Libya wanamkumbuka Gadafi sasa kwa mambo kama kumchafua mtu ili aonekane hafai na muuaji. Chavez yuko sawa proganda nyingi zilitengenezwa na Obotte na Nyerere ili kusimamisha kanisa Catholic Afrika mashariki na kuua umoja wa kiiskam ulioanza kukita mizizi ktk ukanda wa Afrika mashariki huku Idd Amin akiongoza harakati. Nawapenda sana Gadaf, Mugabe na Idd Amin kwani ndio viongozi shupavu hapa Afrika, wengine takataka.

Unamtukana Raisi wetu Jakaya?
 
Nitahitaji kukosolewa ikibidi, binafsi ninavyomjua Hugo Chaves(rais wa Venezuela) hawezi kusema maneno hayo. Hii itakuwa ni propaganda inayoandaliwa kuhakikisha hakuna ushirikiano wa kuimalisha umoja kati ya China, Afrika, na bara la Amerika ya Kusini. Lakini tuhuma za habari hii kutokuwa ya kweli zinazidi kupanda baada ya kufatilia chanzo cha habari(fuatilia source ya habari iliyotolewa kwenye post ya kwanza). Chanzo kinaonekana kama kimekaa kaa kama kujitangaza tanganza kupitia mgongo wa Rais wa Venezuela.
 
facts could be twisted! But the fact remain we know very little of Amini to argue anything different to his existing image. I guess more research, reading and exploration of the past will provide us part with facts! we should research and write significantly about about leaders of africa from their personal character to the global and local context of whcih their leadership emege, existed and died. This role must as well be taken by africans with different opinions - not to say africans can write better but their voices could contribution to creation of different perspectives.
 
Nahisi waganda wanafaidi baadhi ya matunda ya amini, kukimbiza wahindi wote kutoka uganda
 
Kama kuna jambo la maana alillo lifanya ni kuwafukuza wahindi na waarabu Uganda,tunahitaji spirit kama hizi katika kuchukua maamuzi magumu bila kujali wengine watasemaje.

Usichanganye wahindi na waarabu. Amin hakufukuza wahindi wala waarabu.

Amin aliwapa ultimatum wageni wote na kuweka deadline, majority ya wageni waliokataa kuondoa ubaguzi ni Wahindi na ilipofika deadline ikabidi waondoke. Waarabu kwa upande wao walikubali masharti ya Idi Amin na wakabaki.

Aliyewafanyia unyama wahindi na waarabu ni Abeid Amaan Karume kufikia mpaka kuamuru wabakwe kwa nguvu (forced marriage).
 
ukweli ni huo aliosema Chavez. Idd Amin hakuwa muuwaji wala hakuwahi kula nyama ya binadamu. Ni uongo na propaganda chafu za wapinzani wake akiwemo raisi wa sasa wa Uganda. Nimewahi kuongea na vijana wa zamani wakati wa Idd Amin ambao sasa ni wazee wamethibitisha kwamba jamaa alikuwa mzalendo wa kweli aliyetaka kila mganda kumiliki njia kuu za uchumi na rasilimali za nchi yake badala ya wageni (Wahindi). Leo hii Uganda wanalia, uchumi unamilikiwa na wageni wao wakibaki kuwa vibarua! Nitaweka link bdae inayoeleza tofauti ya Amini, Obote na Mu7.

iweke iyo link mzazi ili wapate funga midomo yao ya kufikiri na kusema idd amin ni mkatili
 
Iddi Amin is dead nw, mwachenapumzike kwa amani

  • A%20S-danger.gif

ukweli ni huo aliosema Chavez. Idd Amin hakuwa muuwaji wala hakuwahi kula nyama ya binadamu. Ni uongo na propaganda chafu za wapinzani wake akiwemo raisi wa sasa wa Uganda. Nimewahi kuongea na vijana wa zamani wakati wa Idd Amin ambao sasa ni wazee wamethibitisha kwamba jamaa alikuwa mzalendo wa kweli aliyetaka kila mganda kumiliki njia kuu za uchumi na rasilimali za nchi yake badala ya wageni (Wahindi). Leo hii Uganda wanalia, uchumi unamilikiwa na wageni wao wakibaki kuwa vibarua! Nitaweka link bdae inayoeleza tofauti ya Amini, Obote na Mu7.

Wewe unaujua asafi wa Idd Amini kuliko raisi wa Uganda!!
Au wewe unaujua usafi wa Idd Amini kuliko mwanae aliekuja kunana na familia ya Nyerere na kukiri udikteta wa baba yake?!! Toa boriti machoni kwanza ndiyo utaona vizuri kibanzi kwenye jicho la mwenzio.
 
.
.
****

Hugo Chavez is an idiot and a fool. Waliyo ishi na kupitia kipindi hicho cha Idi Amin wana jua uchungu na maumivu yake. Now I'm starting to think that this guys enjoys saying things he knows will be different from others. Yani yeye watu wakienda kulia yeye ni lazima aende kushoto.
 
****...

C.r.a.p

hugo chavez is an idiot and a fool. Waliyo ishi na kupitia kipindi hicho cha idi amin wana jua uchungu na maumivu yake. Now i'm starting to think that this guys enjoys saying things he knows will be different from others. Yani yeye watu wakienda kulia yeye ni lazima aende kushoto.
 
kwa kweli siasa ni mchezo mchafu, mambo mengi tunavyoyasikia na ukweli wake unapishana kwa sana. kama vile mgogoro wa madaktari ulivyokuwa ukizungumzwa na serikali na ukweli wenyewe, suali la Mwakyembe na ukweli wenyewe na mengi, hizi kesi mbili za karibu zinaonyesha jinsi gani siasa ilivyo mbaya, na ukizidiwa ukubali kuwa ww ni mchafu na ....
 
[h=1]Nyanjura na Kisubi, ni kizazi kipya cha Uganda na Afrika?[/h]
Mwandishi Wetu

235_nyanjura.jpg

Nyanjura Doreen

APRILI 11 ni siku yenye kumbukumbu nzito kwa nchi za Uganda na Tanzania. Siku kama hiyo mnamo mwaka 1979, majeshi ya ukombozi ya Tanzania na Uganda (wapiganaji wa msituni) yalifanikiwa kumtimua Iddi Amin kutoka Kampala, na kuandikwa historia ya kumaliza utawala wa kimabavu uliokuwa umedumu Uganda kwa zaidi ya miaka tisa.
Wakati ule ilionekana Iddi Amin, alikuwa amekaa miaka mingi madarakani. Leo hii Rais Yoweri Museveni, anakaribia kufikisha miaka 20 akiwa madarakani. Wameziba midomo ya watu wengine kusema na kuhoji na hili halikuwa ni lengo Rais Museveni, alipokuwa akiingia madarakani.
Ingawa ushindi huo wa 1979 ulipokewa kwa furaha na Waganda pamoja na ndugu zao Watanzania, bado kuna ukweli ambao hadi leo hii unaishia ndani ya mioyo ya Waganda. Pamoja na mabaya yote yaliyoandikwa na kutangazwa juu ya Iddi Amin, ukweli unabaki kwamba huyu ni rais pekee wa Uganda ambaye hakuwa na mali binafsi, hakuwekeza fedha nje ya nchi; alitumia fedha ya Uganda kwa maendeleo ya Uganda.
Hakuwa na fedha nje ya nchi, aliamini fedha zote ni zake na kama zake yeye Rais, basi fedha ni za Waganda. Alipokuwa akiikimbia Uganda, alikuwa na uwezo wa kubeba vitu vingi, lakini hata ndege ya Rais ambayo eti walienda kuinunua akiwa na fedha kwenye mkoba na yeye kuwa mtu wa kwanza kununua ndege kwa mtindo huo, hakuondoka nayo, aliicha maana aliamini si mali yake bali ni mali ya Waganda.
Inasemekana kwamba nyumba za ubalozi wa Uganda katika nchi nyingi zenye uhusiano na Uganda zilijengwa na Iddi Amin. Hata nyumba nzuri za mapolisi zilijengwa na Iddi Amin. Ingawa Iddi Amin alikuwa mtu ambaye hakuwa na elimu ya juu, lakini alipenda elimu. Vijana wote waliomaliza kidato cha sita wakati wa utawala wake na kushinda kwa daraja la kwanza, aliwapeleka wote kwa nguvu kujifunza ualimu, ili warudi na kuwafundisha watoto wengine.
Walimu wengi walipoikimbia Uganda kwa kuhofia usalama wa maisha yao, Iddi Amin, eti alitumia ndege yake ya Urais, kwenda Ghana, kusomba walimu na kuwaleta Uganda ili wawafundishe watoto wa Uganda. Yapo mengi mazuri aliyoyafanya Iddi Amin, lakini yalifunikwa kwa propaganda za kisiasa. Si lengo la makala hii kumtetea Iddi Amin, bali ni kutolea mfano wa Aprili 11.
Kumbukumbu nyingine mbaya ya tarehe hiyo ni ya mwaka huu alipokamatwa na kuwekwa ndani binti mdogo wa miaka 22, Nyanjura Doreen, kwa kuandika kitabu kinachomkosoa Rais Museveni.
Furaha ya kumfukuza Iddi Amin, imeanza kuleta machungu na masikitiko Uganda zaidi ya miaka 31 tangu Iddi Amin atoke madarakani.
Kwa vile Tanzania, ilishiriki kikamilifu kumfukuza Iddi Amin, haiwezi kukaa kimya, historia inapojirudia. Kuna haja kwa Watanzania kushirikiana na Waganda kulaani kitendo cha serikali ya Uganda kumkamata binti mdogo na kumfunga gerezani kwa kitendo cha kuandika kitabu.
Nyanjura Doreen na mwenzake Bagaya Ibrahim Kisubi, wameandika kitabu : “Is It The Fundamental Change?” wakilenga kufichua ukweli uliojificha juu ya maisha na utawala wa Rais Museveni wa Uganda. Wanasema Rais Museveni alipoingia madarakani, alitoa ahadi ya kuleta mabadiliko ya msingi. Kinachoonekana leo ni tofauti kabisa. Vijana hawa wawili na wengine wengi nchini Uganda, wamezaliwa wakati Rais Yoweri akiitawala Uganda, wamekuwa wamesoma hadi chuo kikuu, bado Rais ni yule yule.
Hilo ndilo swali lao kubwa. Kwamba mabadiliko ya msingi yanaweza kuwa na maana yoyote ile kwa kumtengeneza rais wa maisha? Kwa kuizika demokrasia na kunyamazisha vyama vya upinzani?
Walichofanya vijana hawa ni kukusanya maneno ya Rais Museveni mwenyewe, na kuhoji ukweli wa yale yote aliyoyatamka siku akiingia madarakani hadi leo hii. Na jibu ni kwamba wakati umefika wa “Mzee” kupisha kizazi kipya. Kitu ambacho Rais Museveni na serikali yake hawako tayari kukisikia, na ndicho kisa cha kumkamata na kumuweka Doreen na mwezake ndani.
Ninapoandika makala hii Doreen na mwenzake bado wako ndani hadi Jumanne ijayo (24.4.2012) watakaposomewa mashitaka. Lakini kuna shinikizo kubwa kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vyote jijini Kampala kutaka ifikapo mwanzo wa wiki hii Doreen ambaye ni makamu rais wa serikali ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda na mwenzake wawe wametolewa gerezani bila masharti yoyote. Vijana wameapa kufanya maandamano ya nguvu liwalo na liwe.
Unapofika wakati vijana wakawa tayari kwa lolote, ni hali ya kugopesha. Kwanza vijana ndiyo asilimia kubwa ya watu duniani. Siku vijana wakikubaliana kuungana na kuwa na sauti moja na kuamua kuingia mitaani; viongozi wanaotaka kuzeekea madarani watapata tabu kubwa.
Nilikutana na Nyanjura Doreen, jijini Mwanza siku ya Pasaka, akiwa na nakala chache za kitabu chake cha “Is it The Fundamental Change?” Ni vigumu kuamini kwamba msichana mdogo kama Doreen, anaweza kuwa na maneno ya kuongea; maneno ya kuwaomba viongozi waliokaa muda mrefu madarakani, waachie ngazi vijana chipukizi.
Aliniomba nikifanyie uhakiki kitabu chake na kukiweka kwenye magazeti ya Tanzania. Lengo lake kubwa lilikuwa ni kukisambaza kitabu hicho kabla ya kukizundua Jijini Kampala Aprili 11. 2012. Nafikiri alijua wazi kwamba uwezekano wa serikali ya Uganda kukizuia kitabu hicho kisizinduliwe na kusambazwa ulikuwa ni mkubwa.
Huo ulikuwa ujumbe tosha kwa serikali ya Uganda, kwamba mbinu za kizamani za kuzuia vitabu kusomwa, kuzuia vitabu kuzinduliwa, zimepitwa na wakati. Sasa kitabu kimefika Tanzania, kutoka hapa kitasambaa Kenya, Rwanda, Burundi na nchi nyingi za Kiafrika hata Ulaya na Marekani. Na kitendo cha kuwakamata waandishi wa kitabu hiki na kuwaweka ndani ni mtindo wa kizamani usiokuwa na tija.
Hata mtu ambaye alikuwa hana habari juu ya Nyanjara Doreen, sasa amemfahamu na atataka amfahamu vizuri kwa kutaka kufahamu ni kwanini binti mdogo kama huyo akamatwe na kuwekwa ndani, hiyo ikisaidia kitabu hicho kitafutwe kwa udi na uvumba.
Pamoja na hofu hiyo, alikataa kutokurejea Uganda. Alisema asingeweza kuikimbia nchi yake. Anajua ana haki zote za kutoa maoni na ni haki yake kutetea haki na kuhakikisha demokrasia na mabadiliko ya msingi yanatendeka nchini Uganda. Ni bora akamatwe, afungwe na hata ikibidi aifie nchi yake.
Nilishangaa kuona binti mdogo wa miaka 22 akiwa na ushupavu wa kiasi hicho. Na kweli siku mbili baada ya kukutana naye Mwanza, alikamatwa siku ya kukizindua kitabu chake na kutupwa gerezani.
Uzinduzi wa kitabu chao ulikuwa ni waina yake. Waandishi walivalia nguo za wasomba taka taka na kushikilia mifagio na vyombo vya kukusanyia takataka na kuelekea kwenye uwanja wa Katiba wa jijini Kampala ili kuusafisha waweze kuzindua kitabu chao kwenye uwanja ulio safi. Polisi waliwakamata wakiwa njiani kuelekea kwenye uwanjani.
Kwenye kitabu chao wananukuu maneno ya Martin Luther King; “Maisha yanaelekea mwishoni, siku tunapokaa kimya kwa mambo ya msingi” (tafsiri ni yangu). Pia wananukuu maneno ya Napoleon, pale aliposema kwamba “ Dunia inateseka, si kwa sababu ya vurugu na maasi ya watu wabaya, bali ni kwa sababu ya ukimya wa watu wema”.
Nyanjura Doreen na Bagaya Ibrahim Kisubi, hawakupenda kuwa kimya; walitaka kuyashughulikia mambo ya msingi: kutetea demokrasia, kutetea haki za binadamu, kutetea uhuru wa kujieleza.
Pamoja na ukweli wa kujua kitakachotokea; kukamatwa, kupigwa, kuwekwa ndani na wakati mwingine kupoteza maisha yao, bado waliendelea na mipango ya kukizindua kitabu chao.
Hili linashangaza. Ni ujumbe si kwa Rais Museveni peke yake, bali kwa marais wa Afrika ya Mashariki na Afrika nzima: kwamba mabadiliko ya msingi yataletwa na kizazi kipya. Matumizi ya silaha yanapitwa na wakati. Mbele yetu ni nguvu ya kizazi kipya mbayo kuizuia ni lazima mtu awe tayari kuwekwa kwenye rekodi ya mauaji ya kimbari.
Wahenga walisema: “mwenzako akinyolewa wewe tia maji”. Watanzania tunajifunza nini katika serikali ya Uganda kuwakamata na kuwashitaki waandishi?
 
Nyanjura na Kisubi, ni kizazi kipya cha Uganda na Afrika?

Mwandishi Wetu

235_nyanjura.jpg

Nyanjura Doreen

APRILI 11 ni siku yenye kumbukumbu nzito kwa nchi za Uganda na Tanzania. Siku kama hiyo mnamo mwaka 1979, majeshi ya ukombozi ya Tanzania na Uganda (wapiganaji wa msituni) yalifanikiwa kumtimua Iddi Amin kutoka Kampala, na kuandikwa historia ya kumaliza utawala wa kimabavu uliokuwa umedumu Uganda kwa zaidi ya miaka tisa.

Wakati ule ilionekana Iddi Amin, alikuwa amekaa miaka mingi madarakani. Leo hii Rais Yoweri Museveni, anakaribia kufikisha miaka 20 akiwa madarakani. Wameziba midomo ya watu wengine kusema na kuhoji na hili halikuwa ni lengo Rais Museveni, alipokuwa akiingia madarakani.
Ingawa ushindi huo wa 1979 ulipokewa kwa furaha na Waganda pamoja na ndugu zao Watanzania, bado kuna ukweli ambao hadi leo hii unaishia ndani ya mioyo ya Waganda. Pamoja na mabaya yote yaliyoandikwa na kutangazwa juu ya Iddi Amin, ukweli unabaki kwamba huyu ni rais pekee wa Uganda ambaye hakuwa na mali binafsi, hakuwekeza fedha nje ya nchi; alitumia fedha ya Uganda kwa maendeleo ya Uganda.

Hakuwa na fedha nje ya nchi, aliamini fedha zote ni zake na kama zake yeye Rais, basi fedha ni za Waganda. Alipokuwa akiikimbia Uganda, alikuwa na uwezo wa kubeba vitu vingi, lakini hata ndege ya Rais ambayo eti walienda kuinunua akiwa na fedha kwenye mkoba na yeye kuwa mtu wa kwanza kununua ndege kwa mtindo huo, hakuondoka nayo, aliicha maana aliamini si mali yake bali ni mali ya Waganda.

Inasemekana kwamba nyumba za ubalozi wa Uganda katika nchi nyingi zenye uhusiano na Uganda zilijengwa na Iddi Amin. Hata nyumba nzuri za mapolisi zilijengwa na Iddi Amin. Ingawa Iddi Amin alikuwa mtu ambaye hakuwa na elimu ya juu, lakini alipenda elimu. Vijana wote waliomaliza kidato cha sita wakati wa utawala wake na kushinda kwa daraja la kwanza, aliwapeleka wote kwa nguvu kujifunza ualimu, ili warudi na kuwafundisha watoto wengine.
Walimu wengi walipoikimbia Uganda kwa kuhofia usalama wa maisha yao, Iddi Amin, eti alitumia ndege yake ya Urais, kwenda Ghana, kusomba walimu na kuwaleta Uganda ili wawafundishe watoto wa Uganda. Yapo mengi mazuri aliyoyafanya Iddi Amin, lakini yalifunikwa kwa propaganda za kisiasa. Si lengo la makala hii kumtetea Iddi Amin, bali ni kutolea mfano wa Aprili 11.
Kumbukumbu nyingine mbaya ya tarehe hiyo ni ya mwaka huu alipokamatwa na kuwekwa ndani binti mdogo wa miaka 22, Nyanjura Doreen, kwa kuandika kitabu kinachomkosoa Rais Museveni.
Furaha ya kumfukuza Iddi Amin, imeanza kuleta machungu na masikitiko Uganda zaidi ya miaka 31 tangu Iddi Amin atoke madarakani.

Kwa vile Tanzania, ilishiriki kikamilifu kumfukuza Iddi Amin, haiwezi kukaa kimya, historia inapojirudia. Kuna haja kwa Watanzania kushirikiana na Waganda kulaani kitendo cha serikali ya Uganda kumkamata binti mdogo na kumfunga gerezani kwa kitendo cha kuandika kitabu.
Nyanjura Doreen na mwenzake Bagaya Ibrahim Kisubi, wameandika kitabu : "Is It The Fundamental Change?" wakilenga kufichua ukweli uliojificha juu ya maisha na utawala wa Rais Museveni wa Uganda. Wanasema Rais Museveni alipoingia madarakani, alitoa ahadi ya kuleta mabadiliko ya msingi. Kinachoonekana leo ni tofauti kabisa. Vijana hawa wawili na wengine wengi nchini Uganda, wamezaliwa wakati Rais Yoweri akiitawala Uganda, wamekuwa wamesoma hadi chuo kikuu, bado Rais ni yule yule.

Hilo ndilo swali lao kubwa. Kwamba mabadiliko ya msingi yanaweza kuwa na maana yoyote ile kwa kumtengeneza rais wa maisha? Kwa kuizika demokrasia na kunyamazisha vyama vya upinzani?

Walichofanya vijana hawa ni kukusanya maneno ya Rais Museveni mwenyewe, na kuhoji ukweli wa yale yote aliyoyatamka siku akiingia madarakani hadi leo hii. Na jibu ni kwamba wakati umefika wa "Mzee" kupisha kizazi kipya. Kitu ambacho Rais Museveni na serikali yake hawako tayari kukisikia, na ndicho kisa cha kumkamata na kumuweka Doreen na mwezake ndani.
Ninapoandika makala hii Doreen na mwenzake bado wako ndani hadi Jumanne ijayo (24.4.2012) watakaposomewa mashitaka. Lakini kuna shinikizo kubwa kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vyote jijini Kampala kutaka ifikapo mwanzo wa wiki hii Doreen ambaye ni makamu rais wa serikali ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda na mwenzake wawe wametolewa gerezani bila masharti yoyote. Vijana wameapa kufanya maandamano ya nguvu liwalo na liwe.
Unapofika wakati vijana wakawa tayari kwa lolote, ni hali ya kugopesha. Kwanza vijana ndiyo asilimia kubwa ya watu duniani. Siku vijana wakikubaliana kuungana na kuwa na sauti moja na kuamua kuingia mitaani; viongozi wanaotaka kuzeekea madarani watapata tabu kubwa.
Nilikutana na Nyanjura Doreen, jijini Mwanza siku ya Pasaka, akiwa na nakala chache za kitabu chake cha "Is it The Fundamental Change?" Ni vigumu kuamini kwamba msichana mdogo kama Doreen, anaweza kuwa na maneno ya kuongea; maneno ya kuwaomba viongozi waliokaa muda mrefu madarakani, waachie ngazi vijana chipukizi.

Aliniomba nikifanyie uhakiki kitabu chake na kukiweka kwenye magazeti ya Tanzania. Lengo lake kubwa lilikuwa ni kukisambaza kitabu hicho kabla ya kukizundua Jijini Kampala Aprili 11. 2012. Nafikiri alijua wazi kwamba uwezekano wa serikali ya Uganda kukizuia kitabu hicho kisizinduliwe na kusambazwa ulikuwa ni mkubwa.

Huo ulikuwa ujumbe tosha kwa serikali ya Uganda, kwamba mbinu za kizamani za kuzuia vitabu kusomwa, kuzuia vitabu kuzinduliwa, zimepitwa na wakati. Sasa kitabu kimefika Tanzania, kutoka hapa kitasambaa Kenya, Rwanda, Burundi na nchi nyingi za Kiafrika hata Ulaya na Marekani. Na kitendo cha kuwakamata waandishi wa kitabu hiki na kuwaweka ndani ni mtindo wa kizamani usiokuwa na tija.

Hata mtu ambaye alikuwa hana habari juu ya Nyanjara Doreen, sasa amemfahamu na atataka amfahamu vizuri kwa kutaka kufahamu ni kwanini binti mdogo kama huyo akamatwe na kuwekwa ndani, hiyo ikisaidia kitabu hicho kitafutwe kwa udi na uvumba.

Pamoja na hofu hiyo, alikataa kutokurejea Uganda. Alisema asingeweza kuikimbia nchi yake. Anajua ana haki zote za kutoa maoni na ni haki yake kutetea haki na kuhakikisha demokrasia na mabadiliko ya msingi yanatendeka nchini Uganda. Ni bora akamatwe, afungwe na hata ikibidi aifie nchi yake.

Nilishangaa kuona binti mdogo wa miaka 22 akiwa na ushupavu wa kiasi hicho. Na kweli siku mbili baada ya kukutana naye Mwanza, alikamatwa siku ya kukizindua kitabu chake na kutupwa gerezani.

Uzinduzi wa kitabu chao ulikuwa ni waina yake. Waandishi walivalia nguo za wasomba taka taka na kushikilia mifagio na vyombo vya kukusanyia takataka na kuelekea kwenye uwanja wa Katiba wa jijini Kampala ili kuusafisha waweze kuzindua kitabu chao kwenye uwanja ulio safi. Polisi waliwakamata wakiwa njiani kuelekea kwenye uwanjani.

Kwenye kitabu chao wananukuu maneno ya Martin Luther King; "Maisha yanaelekea mwishoni, siku tunapokaa kimya kwa mambo ya msingi" (tafsiri ni yangu). Pia wananukuu maneno ya Napoleon, pale aliposema kwamba " Dunia inateseka, si kwa sababu ya vurugu na maasi ya watu wabaya, bali ni kwa sababu ya ukimya wa watu wema".

Nyanjura Doreen na Bagaya Ibrahim Kisubi, hawakupenda kuwa kimya; walitaka kuyashughulikia mambo ya msingi: kutetea demokrasia, kutetea haki za binadamu, kutetea uhuru wa kujieleza.
Pamoja na ukweli wa kujua kitakachotokea; kukamatwa, kupigwa, kuwekwa ndani na wakati mwingine kupoteza maisha yao, bado waliendelea na mipango ya kukizindua kitabu chao.
Hili linashangaza. Ni ujumbe si kwa Rais Museveni peke yake, bali kwa marais wa Afrika ya Mashariki na Afrika nzima: kwamba mabadiliko ya msingi yataletwa na kizazi kipya. Matumizi ya silaha yanapitwa na wakati. Mbele yetu ni nguvu ya kizazi kipya mbayo kuizuia ni lazima mtu awe tayari kuwekwa kwenye rekodi ya mauaji ya kimbari.

Wahenga walisema: "mwenzako akinyolewa wewe tia maji". Watanzania tunajifunza nini katika serikali ya Uganda kuwakamata na kuwashitaki waandishi?

Very strange jinsi nchi zinavyoweza kuwa kama ukoo fulani ... watu wanachange lakni ... Tabia ya ukoo fulani remains constant!!

Sasa M7 amechukua kijiti!! anakimbiza ngwe yake!! Kweli kila kizazi na vugu vugu lake la ukombozi!!

Similar Discussions

Back
Top Bottom