Jinsi Makomando wa Israel walivyowaokoa mateka 102 waliofichwa Uganda kwa dakika 58

kalipeni

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
1,533
1,242
JINSI MAKOMANDO WA ISRAEL WALIVYOWAOKOA MATEKA 102 WALIOFICHWA UGANDA KWA DAKIKA 58

Serikali ya Israel imeapa kulipa kisasi kwa shambulio la kushtukiza la kundi la wanamgambo wa Hamas ambalo ni baya zaidi katika historia ya miongo ya hivi karibuni.

Tayari mashambulizi dhidi ya ukanda wa Gaza ambao upo chini ya utawala wa Hamas yamechachamaa. Wakati baadhi ya mataifa yakitaka vita vikomeshwe, Marekani chini ya Rais Joe Biden imekuwa mstari wa mbele kuitetea Israel na imeahidi kuipa msaada wa aiana yoyote katika makabiliano yao mapya dhidi ya Hamas.

Juni 27, 1976, ndege ya Air France 139 kutoka Tel Aviv kuelekea Paris ilitua kwa muda mfupi mjini Athens, Ugiriki. Wakati ndege inapaa kuendelea na safari, abiria wanne ghafla wakaamka kutoka kwenye viti vyao. Walikuwa na bastola na guruneti mikononi mwao.

Na punde tu baada ya kuchukua udhibiti wa ndege, mmoja wao alimuagiza rubani kuelekea mji wa Benghazi huko Libya. Miongoni mwa watekaji nyara wanne walikuwa raia wawili wa Palestina na wawili wa Ujerumani.

Mmoja kati ya wanne hao, Bridget Kullman, alitoa pini ya guruneti na kutishia kwamba atalipua ndege ikiwa kuna yeyote ambaye atakuwa mkaidi, amesema Jian Haratov, abiria aliyekuwa kwenye ndege.

Baada ya kutua na kuwa kwa mapumziko ya saa saba huko Benghazi na ndege hiyo kujazwa mafuta, watekaji nyara walimuagiza rubani kuipeleka ndege hiyo uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda.

Wakati huo, Uganda ilikuwa inatawaliwa na dikteta Idi Amin ambaye alikuwa anawaunga mkono kikamilifu na watekaji wale.

Watekaji nyara hao walikutana na wenzao wengine katika uwanja wa ndege wa Entebbe.
1697132150676.png


Waliwatenganisha abiria wa Kiyahudi na kudai kuachiwa huru kwa wafungwa 54 wa Palestina waliokuwa wamefungwa magerezani katika nchi mbalimbali kote duniani. Pia walitishia kuua abiria ikiwa madai yao hayatatimizwa.

Entebbe ipo takriban kilomita 4000 kutoka Israel. Hivyo basi, operesheni ya kunusuru abiria hao huenda hata haingefikiriwa. Watu wenye hasira katika mji wa Tel Aviv walikuwa wameanza kuandamana.

Baadhi ya waliokuwa wameshikwa mateka walikuwa watu wa karibu na Waziri Mkuu wa Israeli Yitzhak Rabin. Kulikuwa na shinikizo kubwa sana kuhakikisha abiria wanaachiwa huru kwa kila namna.

KUTENGWA KWA ABIRIA WA KIYAHUDI'

Sarah Davidson, mmoja kati ya abiria waliotekwa nyara, anasema watekaji nyara waligawanya abiria mara mbili. "Waliandika majina ya watu na kuwaagiza kwenda chumba kingine. Na baada ya muda wakagundua kuwa wanaotajwa ni Wayahudi tu."

Abiria 47 ambao hawakuwa Wakiyahudi waliachiwa huru. Na wakasafirishwa hadi Paris kwa kutumia ndege maalum. Huko, majasusi wa Mossad walizungumza nao na kujua mengi kuhusu eneo la Entebbe.

1697132669267.png


Jasusi wa Mossad alipanda ndege nchini Kenya na kusafiri hadi Entebbe kuupiga picha uwanja huo wa ndege. Hususan eneo la abiria la uwanja huo ambapo abiria hao walikuwa wameshikiliwa mateka. Eneo hilo pia lilikuwa limetengenezwa na kampuni ya Israeli.

Ramani ya eneo la abiria ilipatikana kutoka kwa kampuni hiyo na wakaanza kupanga namna ya kutekeleza shambulizi.

"KAMPENI INAJUMUISHA WACHEZAJI HODARI"

Makomando 200 kutoka jeshi la Israeli walichaguliwa kushiriki kwenye kampeni hiyo. Lakini timu hiyo ya makomando ilikuwa inakabiliwa na changamoto nyingi. Itakuwaje ikiwa taa zingezima usiku katika uwanja wa ndege? Au ikiwa wanajeshi wa Idi Amin walikuwa wamesimamisha magari yao katika njia ya kuruka kupaa ndege? Kulikuwa na changamoto kadhaa zinazofikiriwa.

Serikali ya Israeli iliashiria kuwa ni muhimu kujadiliana na watekaji nyara na kuchukua muda wao kuandaa operesheni ya kikomando. Bar Lev, aliyekuwa afisa wa jeshi aliyeaminika kuwa rafiki wa Idi Amin alichaguliwa kufanya mazungumzo.

Alifanya mazungumzo mara kadhaa na Idi Amin. Hata hivyo, abiria hao hawakuokolewa. Zaidi, Idi Amin alisafiri hadi Port Louis, mji mkuu wa Mauritius, kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika. Na hatua hiyo ikatoa muda zaidi kwa Israeli kujipanga.

NDEGE ILIJAZWA MAFUTA

Changamoto kubwa ilikuwa ni kwenda umbali wa kilomita 4000 na kurejea kwa kilomita hizo hizo. Kwa hiyo, ndege hiyo ikajazwa mafuta na ndege nyengine ikiwa angani.

Brigedia Jenerali Dame Shamron ndiye aliyepewa nafasi ya kuongoza operesheni hiyo na Luteni Kanali Jonathan Netanyahu alipewa jukumu la kusimamia operesheni yenyewe.

Israeli ilikuwa na machaguo matatu. La kwanza ni kupata usaidizi wa anga kufanya shambulizi, la pili ni kufika eneo hilo kwa boti na la tatu ni kufika Uganda kwa njia ya barabara kutoka Kenya.

Na hatimaye, wakaamua kutumia ndege kufika Entebbe, na wanajeshi wa Uganda wakaarifiwa kuwa Idi Amin anarejea kutoka nje ya nchi.

Julai 4, ndege 4 zikapaa katika rasi ya Sinai huko Israeli. Walivuka bahari ya shamu kwa umbali wa mita 30 kutoka usawa wa bahari ili wasinaswe kwenye rada za Misri, Sudan na Saudi Arabia. Wakiwa njiani, makomandoo wa Israeli walivaa sare zilizofanana na za wanajeshi wa Uganda.

DAKIKA6 TU

Waziri Mkuu Rabin alilijulisha baraza la mawaziri mpango wake baada ya ndege kuondoka. Baada ya kusafiri kwa saa saba, ndege ya kwanza ikatua katika uwanja wa ndege wa Entebbe takriban saa saba usiku.


Walikuwa na dakika sita ndege kutua na kuanza kuchukua hatua dhidi ya watekaji nyara. Na hapo ndipo taa katika njia ya ndege zilipoanza. Mlango ulifunguliwa dakika nane kabla ya ndege kutua.

Muda mfupi baada ya ndege kutua, rubani alisimama katikati ya njia na wanajeshi wanaoruka kwa miavuli wakawa wako tayari. Kikosi hicho kilitakiwa kuweka taa za dharura kwa ndege zitakazowasili baadaye.

GARI AINA YA MERCEDES

Gari aina ya Mercedes ilitolewa kutoka ndani ya ndege. Ilikuwa inafanana na ile ya Rais Amin. Ilifuatiwa na gari mbili aina ya Land Rover za makomando. Gari likaanza kwenda kwa kasi kuelekea eneo la kutoka. Makomando waliagizwa wasifyatue risasi hadi watakapofika eneo la kutoka.

1697133574268.png



Wanajeshi wa Israeli walifikiria kuwa wanajeshi wa Uganda wataelewa kwamba Idi Amin alikuwa ameenda kuonana na waliotekwa nyara. Lakini wanajeshi wa Israeli hawakujua kuwa Idi Amin alikuwa ameanza kutumia gari ya rangi nyeupe siku chache zilizopita.

Na hiyo ndio sababu wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanalinda nje ya eneo la kutoka walianza kufyatua risasi. Na papo hapo wakapigwa risasi na makomando wa Israeli kwa kutumia bunduki zisizokuwa na sauti.

Na baada tu ya risasi kufyatuliwa, kamanda akamwambia kila mmoja atoke ndani ya magari na kutembea hadi eneo la abiria. Makomando walitumia spika kuwaambia abiria kwa lugha ya Kiyahudi na Kiingereza kwamba wao ni wanajeshi wa Israeli na kuwa wamekwenda kuwaokoa.

Waliwaambia abiria wasalie eneo la chini na kuwauliza mateka walikuwa wapi kwa lugha ya Kiyahudi.

1697135327728.png


Abiria walionyesha mlango mmoja ambao ulikuwa unakwenda hadi kwenye ukumbi mkuu. Makomando wakaingia kwenye ukumbi huo wakiwa wanatupa maguruneti.

Watekaji nyara pia nao walianza kufyatua risasi punde tu baada ya kuona makomando wa Israeli.

Watekaji wote waliuawa katika tukio hilo la kufyatuliana risasi huku abiria watatu nao wakiaga dunia.Kipindi sawa na hicho, ndege mbili zaidi za Israeli zikawa zimewasili zikiwa na wanajeshi. Ndege ya nne ilikuwa ni ibebe abiria. Ililetwa Entebbe bila yeyote.
Na ndani ya dakika 20, abiria walikuwa wanasafirishwa kwa kutumia gari aina ya Land Rover. Wakati huo, wanajeshi wa Uganda walifyatua risasi na kuzima taa za uwanja wa ndege.
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akizuru kaburi la kaka yake Jonatan aliyeuawa Entebbe


"Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akizuru kaburi la kaka yake Jonatan aliyeuawa Entebbe"

Ni mwanajeshi mmoja pekee wa Israeli aliyeuawa katika operesheni hiyo. Naye ni Luteni Kanali Netanyahu. Kaka wa waziri mkuu wa sasa wa Israeli, Benjamin Netanyahu.
Wanajeshi walimbeba Netanyahu ambaye alikuwa amepata majeraha hadi kwenye ndege. Na ndege ikaondoka dakika ya 58 baada ya kutua Entebbe.
Netanyahau alifariki dunia akiwa njiani. Lakini pia operesheni hiyo ilisababisha vifo vya watekaji nyara 7 na wanajeshi 20 wa Uganda. Abiria mmoja hakuweza kurejea, kwasababu alikuwa amelazwa katika hospitali moja mjini Kampala.
Asubuhi ya Julai 4, abiria 102 waliokuwa wamenusuriwa na makomando wa Israeli waliwasili Tel Aviv kupitia mjini Nairobi. Na hii yote ilichukuliwa kuwa kampeni ya kijasiri zaidi katika historia ya Israeli.
"Tulipotua katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion, kundi la Waisraeli lilikuwepo kutulaki kwa heshima kubwa sana. Waziri Mkuu Rabin na baraza lake la mawaziri walikuwa wamekuja kutulaki," amesema Luteni Kanali Moore.
 
Netanyahu kuanzia baba yake alikuwa ni zionist. Yoni was ambitious and I don't think some of his army colleagues liked him.
Kuna dhana nyingi ya jinsi alivyouwawa. Ila wanasema it was a friendly fire. Three bullets in the chest! Kama yule aliyetumwa na waingereza kumuua Desert Fox, General Rommel, alivyokufa...friendly fire!!!
 
Netanyahu kuanzia baba yake alikuwa ni zionist. Yoni was ambitious and I don't think some of his army colleagues liked him.
Kuna dhana nyingi ya jinsi alivyouwawa. Ila wanasema it was a friendly fire. Three bullets in the chest! Kama yule aliyetumwa na waingereza kumuua Desert Fox, General Rommel, alivyokufa...friendly fire!!!
Maelezo Mazuri sana chief.
 
Back
Top Bottom