Idara ya Usalama wa Taifa yakanusha tuhuma

Idara ya Usalama wa Taifa yakanusha tuhuma

Status
Not open for further replies.
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visivyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze.

Hata Shaggy alishawahi mpa rafiki yake ushauri. ''Say it wasnt me!!''
 
sifa ya kuwa usalama wa taifa ni kuwa na shule ndogo nina jamaa kibao walifeli na ndo usalama wa taifa la tanganyika.hamna jipya ninyi ni mbwa tu wa kamata kamata
Na mimi nawafahamu jama kama watatu wa familia moja wote ni form4 failure yaani big zero NDIYO HUWAGA wanaandama na babamwanaasha
 
Wangekubali hata mimi ningeshangaa maana hata wanyama walijua kuwa watalipinga hili........ Hii ndio bongo akili kichwani
Kweli kabisa hata paka wangu hapa nyumbani anatikisa kichwa kuwa alijua watakakataa,lakini wakatae pia kuwa yule aliyekuwa anawasiliana na Dr.Uli sio mfanyakazi wao mbona Mwanahalisi la juzi limeanika kila kitu!!kama Zee la kulia( aka)zee la LIWALO NA LIWE alikanusha,dhaifu nae alikanusha sembuse nyie TISS??wanajulikana ni sawa na polisi hamna tofauti kwani naamini huwa hawaishikishi akili katika kufikiri.
 
Kwamba taarifa hizi zitawaimarisha na kuwaunganisha kuhakikisha nchi inabaki salama ni kauli ya kutisha. Hivi anayetishia usalama wa nchi hii ni nani kama si hao Zoka anaoapa kuhakikisha wanabakia salama?
 
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visivyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze.

Kwahiyo walipanga kumuumiza tu siyo?
 
hili wamekanusha na uchakachuaji wa kura zetu hawakukanusha tuwaelewaje,,,,..............ni kukiri ya kuwa wao ni wezi wakura?
 
pia IMEVIONYA baadhi ya vyombo vya habari nchini kuacha kujaribu kuihusisha na matukio ya mipango ya kuwadhuru baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani hapa nchini
 
ni wauaji! ni wao walimtesa dr uli,, PERIOD! hizi hadithi zao za afulelaulea, wakamhadithie dhaifu mwenzao VASCO!
 
Hii taasisi mimi nilishajua haipo kwa sababu yanayojiri hapa nchini ukiniambia kuna idara ya usalama halafu ufisadi wa kila aina unatokea napata wakati mgumu kuamini kama hawa jamaa wapo na wanapewa budget. Ni aibu kubwa kuwa na chombo kama hiki kisichojua hata wajibu wake shame on TISS shame on CCM mafisadi
 
Kubenea anatupatia sana watanzania na gazeti lake. Ila ni ukweli usiyopingika kuwa hana uwezo wa kupangilia uongo wake. Mara anakuja na habari ya uhakika kuhusu afisa wa Polisi kuwa ndiye aliyemteka Ulimboka mara aje na jina Rama. Angalia hata kwenye taarifa yake anasema Rama alikuwa anasisitiza kuwa Ulimboka atamke kama alitumwa na CDM wakati huo huo anasema taarifa toka ndani ya TISS ni kwamba chombo hicho kinaamini Ulimboka alitumwa na CDM. Unaona Kubenea anavyojaribu kuupotosha Umma wa Watanzania kuwa TISS wanaamini kuwa Ulimboka alitumiwa na CDM katika sakata la Mgomo kwa kumtaka Rama kuwa alikuwa akisisitiza hilo. Kwa akili ya haraka haraka najiuliza swali hili, "TAMKA KAMA CDM WALIKUTUMA" hiyo sentensi Mwanalalisi waiipata kutoka kwa nani? Ulimboka mwenyewe au mtumishi kutoka dara hiyo ya Usalama wa Taifa?
Sasa mbona wanajitetea ? wewe ndio wamekutuma uje ufute hiyo habari kwenye vichwa vyetu umechelewa ndugu yetu Jack zoka
 
Kubenea anatupatia sana watanzania na gazeti lake. Ila ni ukweli usiyopingika kuwa hana uwezo wa kupangilia uongo wake. Mara anakuja na habari ya uhakika kuhusu afisa wa Polisi kuwa ndiye aliyemteka Ulimboka mara aje na jina Rama. Angalia hata kwenye taarifa yake anasema Rama alikuwa anasisitiza kuwa Ulimboka atamke kama alitumwa na CDM wakati huo huo anasema taarifa toka ndani ya TISS ni kwamba chombo hicho kinaamini Ulimboka alitumwa na CDM. Unaona Kubenea anavyojaribu kuupotosha Umma wa Watanzania kuwa TISS wanaamini kuwa Ulimboka alitumiwa na CDM katika sakata la Mgomo kwa kumtaka Rama kuwa alikuwa akisisitiza hilo. Kwa akili ya haraka haraka najiuliza swali hili, "TAMKA KAMA CDM WALIKUTUMA" hiyo sentensi Mwanalalisi waiipata kutoka kwa nani? Ulimboka mwenyewe au mtumishi kutoka dara hiyo ya Usalama wa Taifa?
Mbona kama kueleweki?!kwa taarifa yako tu Wananchi wana imani na MWANAHALISI na kubenea kuliko hata TISS,DHAIFU,LIWALO NA LIWE na CCM.huu ujumbe wapelekee wenzako
 
gazeti la mwanahalisi wako sahihi sana. huku ndani kuna mvutano mkubwa sana unaendelea juu ya nini kifanyike baada ya makala ile ya mwanahalisi.

Upo mkuu!!? Tafadhari funguka mkuu, kipande chako hiki kimeniachia maswali mengi!! Ongeza japo aya mbili chini yake!!

Mkuu vp Mzee wa BOT bado ana-survive hapo kisiwani? Vp anarejea lini Bongo? Au alishapigwa biti na Vasco?
 
Jamani kama hawa ndiyo INTELLIGENCY ya nchi hii, basi nchi hii itakuwa ni ya watu WAJINGA sana kuliko nchi yeyote katika sayari hii. Unless neno INTELLIGENT lina maana nyingine kabisa na maana ambayo watu waote tunaifahamu dunia hii.

Hili tamko la TISS kweli limeivua nguo kabisa.
 
TISS wanaweweseka kwa wanayoyafanya, tatizo watumishi wa idara hiyo wengi wao akili ndogo (below average) wanayopanga huwa wanafikiri watu wajinga hawajui.
 
Wamhoji kwanza Zoka na Msangi then waje na makanusho yao!! Vinginevyo.......!!!

Hawana jipya kwanza wanashiriki kwa mambo mengi ya ovyo kabisa tufike mahari tuwakatae hawa watu kwani tayari ni majangiri ya nchi yetu kama wanajiita usalama wa raia wakati huo raslimali zetu zinapolwa, wananchi wanateswa mpaka kuuawa wanasemaje ni usalama wa taifa labda ni usalama wa familia zao siyo sisi wajue tu kuwa hatuna imani na idara hii tena hata waje na kauli gani hakuna kitu.
 
It is pathetic! kwa Idara kufikia kiwango cha kutoa statement ambayo ni extremely weak!.......reform kwenye Idara is long overdue........ili kulinda heshima ya Idara........Ni wakati muafaka wa ku-reshufle na kustaafisha baadhi ya key positions.......
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom