Tamko hili hapa;
AMKO RASMI KUHUSU TUHUMADHIDI YA IDARA YA USALAMA WATAIFA
Katikasiku za hivi karibuni, kumejitokeza taarifa zenye tuhuma kadhaa dhidi ya Idaraya Usalama wa Taifa. Taarifa hizo zimekuwa zikitolewa kwenye vyombo vya habarizikiihusisha Idara hii na matukio ambayo yanaidhalilisha na kuzua maswali mengikwa wananchi. Kati ya tuhuma hizo ni tukio la kutekwa kwa Dr. STEPHEN ULIMBOKA,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari na madai ya kufanywa kwa mipango yakuwadhuru baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani. Gazeti moja la kila wikilimekuwa likurudia tuhuma hizo mara kwa mara kwa madai kwamba ni habari zauchunguzi na kuihusisha Idara.
Idarainataka kuwahakikishia wananchi kwamba taarifa hizo ni zaUZUSHI NA UONGO ambazo zina nia ya kuharibujina na sifa ya Idara. Taarifa hizo zimekuwa zikiunganishaunganisha vipande vyataarifa mbalimbali ili kukidhi malengo yaliyokusudiwa na wanaolitumiagazetihilo. Idara haikuhusika wala haihusiki na matukio yoyote yaliyotajwa katikatuhuma hizo. Hivyo tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo.
Matukio yaliyotajwa katikatuhuma hizo yanachunguzwa na Jeshi la Polisi ambacho ndicho Chombo ChenyeDhamana, na kwa Maslahi ya Taifa si vizuri kuachia upotoshaji huo uendelee.
Aidha,tunapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa uzushi na tuhuma zinazotolewa dhidi yaIdara hazitatuvunja moyo bali zitatuunganisha na hivyo kutuimarisha katika azmayetu ya kuhakikisha nchi yetu inaendelea kubaki salama kwa kushirikiana nawanachi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
Imetolewa na Idara ya Usalama wa Taifa,
Makao Makuu,
DAR ES SALAAM
26 Julai, 2012.