Idara ya Usalama wa Taifa yakanusha tuhuma

Status
Not open for further replies.

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,366
11,154
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visivyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze.
Tamko hili hapa;

TAMKO RASMI KUHUSU TUHUMA DHIDI YA IDARA YA USALAMA WATAIFA

Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza taarifa zenye tuhuma kadhaa dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Taarifa hizo zimekuwa zikitolewa kwenye vyombo vya habari zikiihusisha Idara hii na matukio ambayo yanaidhalilisha na kuzua maswali mengi kwa wananchi. Kati ya tuhuma hizo ni tukio la kutekwa kwa Dr. STEPHEN ULIMBOKA, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari na madai ya kufanywa kwa mipango ya kuwadhuru baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani. Gazeti moja la kila wiki limekuwa likirudia tuhuma hizo mara kwa mara kwa madai kwamba ni habari za uchunguzi na kuihusisha Idara.

Idarainataka kuwahakikishia wananchi kwamba taarifa hizo ni za
UZUSHI NA UONGO ambazo zina nia ya kuharibu jina na sifa ya Idara. Taarifa hizo zimekuwa zikiunganishaunganisha vipande vya taarifa mbalimbali ili kukidhi malengo yaliyokusudiwa na wanaolitumia gazeti hilo. Idara haikuhusika wala haihusiki na matukio yoyote yaliyotajwa katika tuhuma hizo. Hivyo tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo.

Matukio yaliyotajwa katika tuhuma hizo yanachunguzwa na Jeshi la Polisi ambacho ndicho Chombo Chenye Dhamana, na kwa Maslahi ya Taifa si vizuri kuachia upotoshaji huo uendelee.

Aidha, tunapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa uzushi na tuhuma zinazotolewa dhidi ya Idara hazitatuvunja moyo bali zitatuunganisha na hivyo kutuimarisha katika azma yetu ya kuhakikisha nchi yetu inaendelea kubaki salama kwa kushirikiana nawanachi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.

Imetolewa na Idara ya Usalama wa Taifa,

Makao Makuu,

DAR ES SALAAM

26 Julai, 2012.
 
Imeongeza kusema kwamba itaendelea kufanya kazi zake kwa weledi na kuwa tukio la kutekwa Dr. Ulimboka linachunguzwa na jeshi la polisi chombo pekee chenye kazi ya kufanya hivyo.

Pia taarifa hizo zinachafua sifa ya IUWT
 
wamekana taarifa iliyoandikwa na mwanahalisi juu ya ushiriki wa TISS ktk kumteka na hatimaye kumtesa DR. Ulimboka

source;chanel 10
 
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamaba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visvyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze. (source channel ten)

Hawakupanga kumuua bali kumtesa ili awatajie aliye nyuma ya mgomo!
 
Nasi tunawapuuza ninyi Usalama wa Taifa, kwani ndio mliohusika . kama mnakanusha nani sasa anahusika mngetuambia basi tungepuuza vyombo vya habari lakini kamwe hatuwezi kuupuuza ukweli.
 
Nasi tunawapuuza ninyi Usalama wa Taifa, kwani ndio mliohusika . kama mnakanusha nani sasa anahusika mngetuambia basi tungepuuza vyombo vya habari lakini kamwe hatuwezi kuupuuza ukweli.
 
Hata Magogoni wamekanusha ijekuwa hawa maslai ya mafisadi? tulitegemea watakuja hivyo. Hakuna cha kushangaa zaidi ya kusubiri 2015 tuifumue hii TISS. TISS imekuwa janga la Taifa kama alivyo Mr. Vasco Da Gama Matonya
 
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamaba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visvyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze. (source channel ten)

Tumeshawapuuza TISS na tunajua kuwa Usalama wa Mafisadi ni waongo pamoja na Director wao Kova
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom