Idara ya Usalama wa Taifa yakanusha tuhuma

Idara ya Usalama wa Taifa yakanusha tuhuma

Status
Not open for further replies.
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visivyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze.
sifa ya kuwa usalama wa taifa ni kuwa na shule ndogo nina jamaa kibao walifeli na ndo usalama wa taifa la tanganyika.hamna jipya ninyi ni mbwa tu wa kamata kamata
 
ni afadhali nisikilize upuuuuzi wa mwigulu machemba kuliko huu wa usalama wa taifa
 
Nasi tunawapuuza ninyi Usalama wa Taifa, kwani ndio mliohusika . kama mnakanusha nani sasa anahusika mngetuambia basi tungepuuza vyombo vya habari lakini kamwe hatuwezi kuupuuza ukweli.

Sijakuelewa hapa mkuu, ina maana TISS wanatuhumiwa kwa vile hawajasema nani kahusika? Kwa uelewa wangu najua mwenye Mamlaka ya kutoa tamko nani kahusika ni Jeshi la Polisi.
 
Sijakuelewa hapa mkuu, ina maana TISS wanatuhumiwa kwa vile hawajasema nani kahusika? Kwa uelewa wangu najua mwenye Mamlaka ya kutoa tamko nani kahusika ni Jeshi la Polisi.

TISS wanatuhumiwa kwa sababu Ramadhani Ighondu (34) mzaliwa wa Matoke-Dodoma, aliyekuwa akifanya mawasiliano ya mara kwa mara na Dr. Ulimboka, ni mfanya kazi wa Ikulu. Ramadhani Ighondu (Rama) ni afisa wa TISS akiwa chini ya Naibu Mkurugenzi Jack Zoka na ndiye aliyewasiliana na Dr. Ulimboka kwa mara ya mwisho kabla ya kutekwa.
 
Kwani hao usalama wa taifa wana watoto? Najua kwa umli wa zoka anao, kwani kulikuwa hamna mbinu mbadala kupata taarifa?

Hao vijana wahusika wanaweza wakawa hawana watoto, hivi hawana akiri kiasi hicho, suala liko hot wanamteka mtu?

nilishawahi chat na hao TISS, wengiwao ni vilaaaza! Hawana vichwa hao, they think wako supperior sana! Hawajui kazi yao

Zoka analo tu, kama sio leo hatakesho! How can u supervise uharamia wa kizamani kama huo? Mambo ya 1800

Kwanza niwafundishe hawa vilaza TISS, kutesa kunatoa taarifa 23%, nusukaputi 98% kwa nn hawakutumia plan b wawe na 98%?

Au lengo lao lilikuwa kueliminate? Bado timing ni ya mwehu tuu ndio anaweza kufanya katika muda ule! Kweli ni vilaza!

Sio kuwa wanaharaka, ni vilaza! Hata panctuation hovyo, kama huyo ndio bosi kaandika je wa chini yake yukoje?
 
Ukanushaji wa habari niliutegemea kwani hawawezi kwenda tofauti na mwajiri wao JeyKey....kukanusha kichwa cha habari na kuacha content ya habari kama ilivyo kwangu mimi inadhihirisha ni wao, wangesema hata waliotajwa kuwa ni watumishi wao ni uongo basi....ipo siku watakuja kusema TULIKUWA TUNAFANYA KWA MASLAHI YA CHAMA
 
Mhh...hii habari hata sielewi nani anasema ukweli au uongo kati ya TISS na Dr. Uli. Mungu na alifungue fumbo hili.
 
Du!Kizunguzungu!!Sasa Mukoba wachama cha walimu akae mkao wakula!
 
Wanapokanusha, wanatakiwa waje na data za kutosha ili Wananchi waelewe na kuamini kile wanachokisema. Kukanusha bila vielelezo, haingii akilini. Waliotoa taarifa hizi walitoa na vielelezo na Wananchi ikawingia akilini. Tunataka "PROOF" ya hayo wanayoyasema. Tunahitaji Wanachi wote tujenga nchi yetu kwa kushirikiana na sio kulinda makundi fulani.
 
Naona giza mbele.
natakiwa nikimwona polisi nijisikie salama lakini kwa sasa nikimwona polisi inabidi nikimbie maana usalama wangu unakuwa mashakani.

Kuwepo usalama wa Taifa ni faraja,lakini kwa hali hii hakuna faraja tena.

Tukimbilie wapi sasa?
 
Labda watuformat vichwa Kama computer tusahau kila kitu

Kubenea anatupatia sana watanzania na gazeti lake. Ila ni ukweli usiyopingika kuwa hana uwezo wa kupangilia uongo wake. Mara anakuja na habari ya uhakika kuhusu afisa wa Polisi kuwa ndiye aliyemteka Ulimboka mara aje na jina Rama. Angalia hata kwenye taarifa yake anasema Rama alikuwa anasisitiza kuwa Ulimboka atamke kama alitumwa na CDM wakati huo huo anasema taarifa toka ndani ya TISS ni kwamba chombo hicho kinaamini Ulimboka alitumwa na CDM. Unaona Kubenea anavyojaribu kuupotosha Umma wa Watanzania kuwa TISS wanaamini kuwa Ulimboka alitumiwa na CDM katika sakata la Mgomo kwa kumtaka Rama kuwa alikuwa akisisitiza hilo. Kwa akili ya haraka haraka najiuliza swali hili, "TAMKA KAMA CDM WALIKUTUMA" hiyo sentensi Mwanalalisi waiipata kutoka kwa nani? Ulimboka mwenyewe au mtumishi kutoka dara hiyo ya Usalama wa Taifa?
 
Huyo mwandishi wa hiyo taarifa alikuwa na haraka sana
 
Vichwa vya watanzania vinajazwa ujinga sana.Sasa hivi tumechoka kujazwa ujinga. Tupe facts, gazeti limetoa facts, wewe unataka tuwapuuze, umekanusha zile facts?
 
TISS wangeshirikiana na Jeshi la Polisi kuwakamata washukiwa wote ikiwemo Rama ambaye alikuwepo wakati Dk anatekwa wao wamemficha rama na kubaki kukanusha kila jambo.

Kukanusha kwao kunaonekana ni kama wamejitokeza kukubali maana hata Rama mwenyewe hajakanusha ajitokeze hadharani kama kweli hakuhusika.

MWANAHALISI limetufungua macho kwa habari za uhakika na simu zao ukipiga hao watu wapo. TISS imekula kwenu hamuwezi kujisafisha kwa hili hata mkiogea sabuni tokea AHERA.
 
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visivyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze.
Basi hata kama ni kukanusha angalau taarifa yenu mngeipitia mara mbili au tatu kwani maneno yameungana na space sio uniform.Kulikuwa na haraka gani kiasi hicho?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom