Idara ya Usalama wa Taifa yakanusha tuhuma

Idara ya Usalama wa Taifa yakanusha tuhuma

Status
Not open for further replies.
Imeongeza kusema kwamba itaendelea kufanya kazi zake kwa weledi na kuwa tukio la kutekwa Dr. Ulimboka linachunguzwa na jeshi la polisi chombo pekee chenye kazi ya kufanya hivyo.

Pia taarifa hizo zinachafua sifa ya IUWT

Eti mnasimamia maslahi ya taifa? Maslahi yapi hayo? kutorosha madini na wanyama pori wangali hai ndio maslahi ya taifa?
Kuchakachua matokeo ya chaguzi mbalimbali kwa lengo la kuwapendelea waume zenu kwenu ndio maslahi ya taifa? Kuteka na kuua viongozi wa taasisi na vyama vyenye msimamo unaotishia maslahi yenu na waume zenu kwenu ndio maslahi ya taifa? Usinitie kichefuchefu Nchi hii haina taasisi yoyote yenye sifa za kuitwa usalama wa taifa. Ni bora mkakaa kimya tu.
 
bado wana mbinu za kizamani mno kusaka taarifa "intarogasheni bai tocharingi",wengi waje huku kitaa tuwape mbinu
 
Eti maslahi ya taifa. Nanyi pia mnaelewa maana ya maslahi ya taifa? Maslahi ya taifa lipi mnayoyasimamia nyie? Madini na wanyama pori wanatoroshwa kupitia uwanja wa ndege mkiwa wapi?

Mnashiriki kuchakachua matokeo ya chaguzi mbalimbali kwa maslahi ya waume zenu alafu mnabana pua eti ooooh maslahi ya taifa, ni maslahi ya taifa gani yanapatikana kwa kuchakachua matokeo ya chaguzi za viongozi? Kuteka na kuua viongozi wa taasisi na vyama vyenye misimamo inayokinzana na maslahi ya waume zenu nayo ni maslahi ya taifa?

Nchi hii haina taasisi yoyote yenye sifa za kuitwa usalama wa taifa. Ni bora mkanyamaza kimya kwani naona mnatuzidishia tu hasira.
 
Tangu lini hawa wamekuwa wakifanya kazi kwa weledi? Wangekuwa wanafanya kazi kwa weledi basi wangemshukia Pinda pale alipotoa kauli kwamba "Wezi wa EPA ni matajiri wakubwa nchini kama wakikamatwa basi nchi itawaka moto." pia wangekuwa makini kuhakikisha ndege ya kigeni haingii nchini usiku usiku kuiba wanyama katika mbuga za Taifa tena bila ya kibali cha kutua nchini...Hawana hata sifa moja ya kustahili kuitwa usalama wa Taifa.

Imeongeza kusema kwamba itaendelea kufanya kazi zake kwa weledi na kuwa tukio la kutekwa Dr. Ulimboka linachunguzwa na jeshi la polisi chombo pekee chenye kazi ya kufanya hivyo.

Pia taarifa hizo zinachafua sifa ya IUWT
 
Aibu sana,idara inayofanya uharamia dhidi ya raia wake,hamuwezi kukanusha kuhusika kwenu na wakati info imetolewa na wana-TISS wenye mapenzi mema na raia wao,mbona hamjasema waliotajwa kama si wafanyakazi wenu,hivi kuna watu waliosoma kwenye hiyo idara?
 
Hata mimi nilitegemea wangekuja na taarifa za kina zenyekujieleza.

Kama wakitaka kukanusha tukawaelewa waanze kubainisha kuanzia yule Abeid/David/Rama, halafu ije Kova na yule Mkenya wa Mchungaji Gwajima,

Then ndiyo waje hizi series za simu zinazoshahabiana na tukio zima la Dr.Ulimboka. Kutuambia tupuuze tu wakati tupo njia panda haitakuwa kitu rahisi hivyo.

Mkuu wanafikiri watanzania wote ni vilaza wa kuaminishwa ujinga kirahisi rahisi. Walitakiwa wakane taarifa kwa kuongelea maudhui ya tarifa husika pamoja na wahusika (characters) waliotajwa. Na sio kutuambia tu TUPUUZE BILA DETAILS zozote kama wanavosemaga Magamba na Kurugenzi ya habari Ikulu wanapobanwa kisawasawa.

Kwa kanusho hili, tayari na wao (TISS) wametumbukia vizuri kwenye hisia zetu (kuwa wanahusika pasi na shaka).
 

Zoka, naibu mkurugenzi wa Tiss anayeshughulikia siasa, ambaye amajiapiza kuwa'ulimboka wote wanaoikosoa serikali.....! Uwiiiiiii.........................!

Tiss; Tunawapenda wadanganyika kwa kuwaficha mafisadi wa EPA na fedha zao zilizopo mabenki ya majuu.....Tisiiiiiiiii......!

Kibanga Msese
 
Kwa kuona tu hiyo taarifa, sasa naelewa kwa nini hiyo idara inafanya haya inayoyafanya, ya kutesa na kuua raia. Katika nchi za wenzetu, ukisikia mtu ni afisa wa intelligence unajua kuwa ni lazima atakuwa ni mtu ambaye akili yake, uwezo wa kuchambua na kuchunguza, upeo na elimu siyo vitu vya kutiliwa mashaka hata kidogo. Sasa huyu aliyeandika hii taarifa, uwezo wake wa kuandika kiswahili, natamka wazi ni pungufu maradufu ya uwezo wangu nilipokuwa darasa la tano. Ni katika madarasa hayo ya msingi ndipo tulikuwa tunafundishwa umuhimu wa kutenganisha maneno, kutambua viunganishi, vihisishi, visifa, n.k.

Hii taarifa imekaa kienyeji ikiwa na maneno zaidi ya moja, yakiwa yamefanywa kuwa neno moja, viunganishi vimechanganywa na maneno, inatia kinyaa hata kusoma, halafu tunasema tuna idara ya intelligence.
 
kila kitu kina mwisho hata sirya walikuwa na usalama wa taifa ila majuzi mkuu wao wa usalama kilichomkuta kila mtu anajua, na TISS, inabid mjifunze kwa hili.
 
badala ya kutuambia nani alimtesa dokta uli wao wanatuambia sio wao... lol
 
Kama hawakushiriki basi wapishe chombo huru cha uchunguzi kichunguze na kutambua nani alishiriki.. Hamuwezi kujichunguza wenyewe... Huyo rama yuko wapi na kwa nini namba zake ndo zilikua za mwisho kumpigia ulimboka? Sisi ni wadanganyika lakini safari hii hatudanganyiki..nyie sio usalama wa taifa bali ni janga la taifa
 
kuna ile video walioikamata madaktari wakati wakimuadhibu mmoja wa wahusika wa utekaji ambae alinyanganywa kamera,simu nk
itawaumbua vizuri.hata mtoto wa chekechea anajua wahusika ni nani.
ni kawaida kwa mtu yoyote duniani anaepinga serikali huadhibiwa kwa njia dhalimu kama alivofanyiwa Ulimboka.
 
tz ya saivi sio kama ile ya zamani' 2meona usalama wa taifa walivyo jipotezea hadhi, wameshndwa kudil na v2 muhmu venye tija kwa taifa..wao wamekuwa usalama wa chama cha mapinduzi, imefkia 2meshndwa kuwatofautisha na wana siasa.
 
Who will even belive them...Kwanza wamekanusha kienyeji kama sio usalama wa Taifa vile... Utadhan ni chama flani cha siasa kinakanusha ubea wa kisiasa.Yani not proffessional kabisa
 
"unaweza kuwadanganya watu wote lakini sio kwa muda mmoja"
 
ni taarifa fupi lakini yenye content iliyojitosheleza.hawa mwanahalisi kwa kweli wanakotupeleka ipo siku nchi itaingia vitani hivi hivi.wanapaswa kudhibitiwa mapema sana,maana chuki wanayopandikiza kwa wananchi sio ndogo

walewale wa mawazo mgando tumewachoka
 
Hivi huko IUWT hakuna makatibu makhsusi? Haiwezekani taarifa fupi ya aya nne tu iwe na printing errors zaidi ia 12!
Fake.
 
kuna taarifa baadhi ya watu wanaowafahamu watu hawa, tayari wamjibu mapigo kwa kuwauwa vija wawili wa idara hiyo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom