what do you have you to say on this incidence?
One story about Jesus in the bible that is confusing and incoherent is the story of the fig tree. Matthew 21:18-19 states, "Early in the morning, as Jesus was on his way back to the city, he was hungry. Seeing a fig tree by the road, he went up to it but found nothing on it except leaves. Then he said to it, “May you never bear fruit again!” Immediately the tree withered."
1. Jesus was hungry (God hungry?)
2. He cursed the fig tree because it wasn't bearing fruit.
A).God didn't know the tree didn't have fruit
B). He cursed a perfectly good tree that was only conforming to its nature to bear fruit in the season God designed it to.
3. The Human nature of Jesus overrode his divine nature and cursed the tree.
For me 3 is an incredibly huge problem. His "divine" nature did not stop his human nature from curse.
Nb
Plz avoid your emotions while answering and reasoning this out. plz.
Umeuliza kwa usahihi zaidi kwamba je Yesu ni asilimia 100 MTU au asilimia 100 Mungu!,Jibu ni NDIO na HAPANA!!! sasa swali lako halitaki uwe biased na msimamo wa dini au dhehebu lako au ubishani wa kichwa chako wewe soma kwa makini ninachokwenda kukujibu halafu chunguza maandiko pia yanasemaje maana sitakujibu kwa maneno yangu mwenyewe nitakupa na vifungu vya biblia vya kuunga mkono Jibu langu!
1.ASILI YA MUNGU (GOD'S NATURE)
Kwanza kwa kuanzia kabla hatujaenda kwa huyo YESU uliyemuuliza hapo tunatakiwa tujue ASILI YA MUNGU (GOD'S NATURE),Mungu ni nani,yupoje ana sifa zipi,ana tabia zipi?.Mungu hana BABA wala hana MAMA,Hana mwazo wa siku zake wala hana mwisho wa siku zake ,Mungu ni wa milele wala hana wazazi (Waebrania 7:1-3),Mungu ni Roho (Yohana 4:24),Mungu ni wa milele maana yake hafi (Kumbu 33:27),Mungu anajua kila kitu (1Yohana 3:20,),Mungu anaweza kila kitu,Mungu yupo kila mahali kwa wakati mmoja na MUNGU SIO MWANADAMU HADI ASEME UONGO (Hesabu 23:19) naweza weka sifa za Mungu hapa nikajaza hii thread yoote wacha niishie hapo
2.KUNA MIUNGU WANGAPI??
Ndani ya biblia yoote hakuna mahali pamesema kuna miungu zaidi ya mmoja hakuna ! Mungu ni mmoja tu! hana msaidizi wala Mungu mwingine pembeni yake,kaumba vitu vyoote ulimwenguni na Mbinguni pekeyake!!!!!! maandiko ni mengi haya hapa (Kumbukumbu 6:4,marko 12:29,marko 12:33,wagalatia 3:20) na hapa pia kuna mistari mingi sana nimechagua kuweka hiyo hapo baadhi tu
Sasa nikirudi kwenye swali lako kinachokuchanganya na kinacho wachanganya watu wengi ni jina YESU!!!!!,na watu wengi wakilisikia jina Yesu kinachokuja kichwani mwao ni Yule mwana wa mariam aliyezaliwa kwa uweza wa roho mtakatifu akaitwa Yesu je Ndio MUNGU?????!!!!,Nimeweka hapo asili ya Mungu ukisoma hizo sifa za asili ya Mungu Yule mwana wa adamu au mwana wa mariam aliyezaliwa akaitwa Yesu hakidhi sifa hizo Yule alikuwa ni mwanadamu tu sasa kwanini tunasema Yesu ni Mungu? tukisema Yesu ni Mungu hatumaanishi yule mtoto wa mariam kama Mungu bali tunamaanisha Yehova,Mungu yule aliyeumba vitu vyoote ndio MUNGU! inamaana jina Yesu limekuja kugundulika ndio jina la Mungu mwenyewe kwenye agano jipya
😀😀😀!!!!
Agano loote la kale Mungu alikuwa na Majina mengine kama YEHOVA,yehova jire,jehova shama,nk.... ila agano Jipya Mungu alilifunua jina lake lingine alilowapa wanadamu chini ya Jua kupitia kwa mwanaye wa pekeee mwana wa mariam YESU!!!! Unabisha??
1.Yesu Mwana wa adamu alisema anakuja kwa jina la baba yangu na hamkumuamini YOHANA 5:43 unadhani jina la baba yake alilosema amekuja nalo ni lipi????
😀😀
2.Yesu aliitwa mwana wa Mungu maana yake Baba yake ni Mungu unajua kwasababu gani? kwasababu kuja kwake hapa duniani hakukuwa kwa njia ya kibinadamu yaani mwanamke kutunga mimba mara baada ya kukutana kimwili na mwanaume bali ni Mungu mwenyewe alimfanya ndiomaana akaitwa mwana wa Mungu unajua hata Adamu aliitwa mwana wa Mungu maana kuja kwake duniani pia aliumbwa na Mungu Moja kwa moja (Luka 3:38) ndiomaana kuna Adamu wa kwanza ambaye yule alileta dhambi pale bustani ya eden na mkewe hawa na Yesu anaitwa Adam wa pili ambaye kupitia yeye dhambi zilifutwa pale msalabani (1 wakorinto 15:45) adamu wa kwanza alileta dhambi,adamu wa pili alifuta dhambi mara baada ya ile damu kumwagika pale msalabani
3.Unajua jina Yesu ni Jina la Urithi???(waebrania 1:4) sasa kama yule mwanadamu aliyezaliwa na bikira mariam aliitwa Yesu alipata hili jina Yesu kwa kurithi je alirithi kutoka kwa nani??? Jibu ni kwamba alirithi kutoka kwa baba yake ambaye ndio Mungu mwenyewe!!!!!
Yesu kristo mwana wa daudi alikuwa mwanadamu kamili 100% kwa maana ya kuwa na Damu na nyama,kuzaliwa na mwanamke,kuwa na mapungufu mengine ya kibinadamu,na wakati huo huo Mungu mwenyewe alikuwa ndani ya Yesu akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake kwahiyo Yule yesu alivyokuwa akifundisha,akiponya,akitembea juu ya maji,akisali akihubiri MUNGU ALIKUWA NDANI YAKE!!!!! imeandikwa hapa (2 Wakolinto 5:19) hata yesu mwenyewe alikiri kuwa hayo yoote anayofanya sio yeye anafanya bali Baba aliye ndani yake maana yake ni hivi MUNGU ALI NDANI YAKE NDIO ANAFANYA imeandikwa hapa (YOHANA 5:30)
Kwahiyo ukiona Yesu ndani ya biblia kasamehe dhambi basi jua ni Mungu ndio kasamehe maana alikuwa ndani yake
😀😀,ukiona Yesu kaponya,katembea juu ya maji,kafufua basi jua ni Mungu ndio kayafanya yoote hayo!
Na Ukiona kwenye biblia Yesu mwana wa daudi kalala,anaumwa njaa,kakua kimo na maarifa basi jua ni yule mwanadamu Yesu ,kwahiyo ndani ya maisha ya YESU MWANA WA MARIAM alikuwa 100%DEVINE na 100%HUMAN! ndiomaana nikakujibu YES and NO
Mwisho wa Yesu kristo mwana wa Mungu uliisha pale msalabani baada ya kufa maana yake kazi aliyoletewa duniani ilikuwa ni kufundisha wanadamu kuwaonyesha njia ya kuishi maisha matakatifu mpaka kifo na mwisho wa siku Mungu akajitolea kafara pale msalabani sasa kujipatanisha baina yake na wanadamu ndiomaana yesu alichomwa ule mkuki ubavuni DAMU NA MAJI VIKATOKA ili kutoa ondoleo la dhambi ndiomaana tunasema tumekombolewa kwa damu na maji vilivyomagika msalabani,Mungu ni Roho kwahiyo kama ni Roho hana damu wa nyama na ili kujipatanisha na wanadamu alihitaji Damu na maji ndiomaana alimuumba mtu halafu akaingia ndani yake na muda ulivyofika akajitolea kafara yule mtu pale msalabani kuleta upatanisho baina yake na wanadamu