Yesu hajasema mahala popote kwenye Biblia kuwa, yeye (mimi) sio Mungu kwa sababu; HAJAWAHI kusema mahala popote kwenye Biblia kuwa yeye (mimi) ni Mungu. Unamtaka akanushe kitu ambacho hajawahi kusema?
Bwana Yesu Kristo alipokuja hapa duniani kwa mara ya kwanza hakuficha kitu kuhusu Uungu wake. Alifanya hivyo kwa kuwa Yeye alikuwa ni Emmanuel, yaani Mungu akiwa pamoja na wanadamu katika hali kibinadamu.
Ni kama vile manabii walivyotabiri kuhusu ujio wake. Nukuu kutoka katika chuo cha Isaya na Mika vinatuambia;
ISAYA 7
13 Ndipo Isaya akasema, “Sikia sasa, ewe nyumba ya Daudi! Je, haitoshi kujaribu uvumilivu wa wanadamu? Je, mtaujaribu uvumilivu wa Mungu wangu pia?
14Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara: Bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, na ataitwa Imanueli.
ISAYA 9
6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto wa kiume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu,
Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.
7 Mamlaka ya enzi yake yatakuzwa daima,
Na kutakuwa na amani isiyo na mwisho,
Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake;
Kuuthibitisha na kuutegemeza
Kwa hukumu na kwa haki,
Tangu sasa na hata milele.
Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.
Hukumu kwa ujeuri na udhalimu
MIKA 5
2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atatokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye asili yake imekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
Yesu Kristo ili alizaliwa kama mwanadamu ili apate kuutimiza unabii huu. Na tunaweza kupata ukweli kuhusu Uungu wake kupitia kauli za kinywa chake yeye mwenyewe kupitia nukuu zifuatazo;
YOHANA 10
30 Mimi na Baba yangu tu mmoja.”
31 Kwa mara nyingine wale Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo.
32 Yesu akawauliza, “Nimewaonyesha mambo mengi mazuri kutoka kwa Baba yangu. Kati ya hayo ni lipi linalosababisha mtake kunipiga mawe?”
33 Wao wakamjibu, “Tunataka kukupiga mawe si kwa sababu ya mambo mema uliyotenda bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.”
YOHANA 14
8 Filipo akamwambia Yesu, “Bwana, tuonyeshe Baba yako nasi tutaridhika.”
9 Yesu akamjibu, “Filipo, imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu? Mtu ye yote ambaye ameniona mimi, amemwona Baba. Sasa inakuwaje unasema, ‘Tuonyeshe Baba’?
10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu? Mambo ninayowaambia siyasemi kwa mamlaka yangu mwenyewe, bali yanatoka kwa Baba yangu ambaye anaishi ndani yangu, na ndiye anayetenda haya yote.
Sent from my Nokia 2.3 using
JamiiForums mobile app