OK tatizo lilianzia bustan ya Eden wakati zambi ilipoingia kwenye kizazi cha binadamu kupitia hawa na adam (Hope you know the story) baada ya pale Mungu alikosana na mwanadamu lakini akaweka utaratibu wa kujipatanisha na wanadamu kupitia kafara ya damu na nyama,aliweka pia list na aina ya wanyama ambao wanafaa kutolewa kafara mbele zake ikiwemo ngombe na kondoo,mnyama wa kafara asiwe mwenye shape mbaya,asiwe mlemavu,asiwe na madoa madoa awe msafi then kabla ya kuchinywa kwa yule mnyama watu ambao walikuwa wanashida ya kujitakasa walikuwa wanaweka mikono yao kwa yule mnyama na kuzitaja dhambi zao (confess) then yule mnyama anachinjwa na kuhani ile damu ya yule mnyama ndio inaenda kufanya upatanisho kati ya hao watu na Mungu kufanya huu upatanisho maana yake wale watu wanafutiwa dhambi zao wanakuwa wametakasika
Sasa huu utaratibu ulikuwa just a formality tu ambayo Mungu aliwawekea wanadamu sababu woote walikuwa chini ya ile laana ya pale bustani ya eden,ila kwa miaka mingi kwenye agano la kale kupitia manabii Mungu mwenyewe alianza kusema kuwa kuna kitu kipya atakuja kukifanya Duniani miongoni mwao ni hawa.
1.MUSA
(Kumbukumbu la torati 18:15-22)
Alitabiri ujio wa Yesu kama Nabii kama yeye musa na mbaye kupitia yeye tutajifunza kila kituna atatoa unabii wake kwa kutumia jina la Mungu mwenyewe!! Rejea thread zangu kuhusu jina Yesu
2.ISAYA
(
Isaiah 7:14,Isaiah 9:6-7)
Isaya ndio alitoa unabii mkubwa kuhusu ujio wa huyu Yesu tunayemzungumzia hapa,kwanza alitabiri kuzaliwa kwa mtoto pilia akatabiri Kutolewa kafara kwa mtoto halafu akatoa mwanga zaidi kwa kutaja sasa Human nature yake akasema huyu mtoto mamlaka zoote za dunia zitakuwa chini yake!,Mwana mfalme wa Amani,Mshauri wa Ajabu, then akataja pia na Devine Nature zake kama MIGHTY GOD! na Eternal Father nk..
Sasa kwanini Mungu alihitaji mpatanishi??? sababu inajulikana tangia mwanzo Mungu alihitaji uhai wa mnyama kuweza kufuta dhambi za wanadamu,this time Mungu alihitaji kupata kafara ya Mtu safi kuweza kuwafutia wanadamu dhambi zao anamtoa wapi?? Mungu hana damu >soote tunajua kuwa Mungu ni Roho kama Mungu ni roho maana yake hana Damu na Nyama kama tulivyo sisi wanadamu na it takes blood to redem us
Ufunio wa Yohana imeandikwa wazi kuwa Mungu alitafuta kila mahali nani wa kufungua kile kitabu maana yake wakwenda kuyatimiza maandiko yake duniani biblia inasema alitafuta Mbinguni hakuona ,akatafuta duniani kwa wanadamu hakuona akaenda hadi chini aldhini maana yake hadi kwa wanadamu waliokufa hakuona wakumtuma imeandikwa hapa ufunuo 5:1-10 ! sasa kama hakuona alikuja nani? ndio pale lile jina Emmanuel linachukua taswira yake maana yake Mungu pamoja nasi yaani Mungu alikuwa nasi katika ule mwili wa Yesu kristo!!!
Mungu kutimiza unabiii alikwenda kwenye kabila la Yuda akamtafuta mwanamke katika ukoo wa daudi akatengeneza MWILI halafu akaingia ndani ya ule mwili halafu ule mwili ukazaliwa na bikira maria ukarithi jina lake ambalo ni Yesu,nguvu,mamlaka,hekima,uweza,maarifa nk..Mungu akiwa ndani ya ule mwili akaanza kuwafundisha wanadamu namna ya kuishi maisha matakatifu,maisha ya kumpendeza Mungu mwenyewe,akaanza kuwafundisha jinsi ya kusali,jinsi ya kufunga,jinsi ya kuomba,jinsi ya kuhubiri injili,jinsi ya kuponya watu,kufufua wafu,kutoa mapepo,jinsi ya kushinda majaribu ya shetani jinsi ya kufunga na mambo mengi sana ule mwili ulikuwa wa kuwaonyeshea binadamu MFANO! na baada ya mifano yoote kutimia
Mungu akaruhusu ule mwili uteswe,upigwe ili maandiko yake yatimie ule mwili ukapelekwa pale msalabani kwaajili ya kutolewa kafara ndio hii maana ya Yesu wakati Mungu aliyekuwa ndani yake sasa natoka Yesu alipiga kelele akalia akisema "MUNGU WANGU MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA" Mungu pale alitoke ndani ya Yesu sasa na Kwenda kuhubiri injili kwa zile roho zingine zilizokuwa zimekufa kabla ya Yesu umesahau kuna sehemu imeandikwa hadi wafu walihubiriwa injili huko huko walikokuwa??? na siku ile ya tatu wale wafu walio amini walifufuka pamoja na yesu na wakawatokea watu wengi pale yerusalemu?? ok turudi kwenye maada yetu hilo ni somo jigine,Ndio sababu Yesu kutokuvunjwa hata mfupa mmoja wa mwili wake sababu kama angevunjika kafara yake pale msalabani mungu angekuwa kajitolea kafara ya mnyama ambaye ni mlemavu ndio maana iliandikwa hawatavunja hata mfupa mmoja wa mwili wake na hapo juu nimekuandikia masharti ya mnyama wa kafara alivyotakiwa awe (ZABURI 34:20,YOHANA 19:36) na hata ule muda wale askari walipokuja kuwakagua wale watu wawili waliosulubiwa pamoja na Yesu wale wawili waliwavunja vidole vyao ila Yesu hawakumvunja kitu isipokuwa walimchoma Mkuki ubavuni halafu DAMU NA MAJI VIKATOKA!!!!!!!! hapa ndipo wanadamu tulipokombolewa
Mungu allijifanyia kafara ya mnyama pale msalabani kusudi damu na Maji yamwagike tupate ondolea la dhambi ONCE AND FOR ALL
Summary ya swali lako
1.Who sanctioned him to be ameaditor-Mungu mwenyewe alijipatanisha na wanadamu kupitia Man Jesus
2.Did God need a meaditor-Mungu ana njia nyingi za kufanya jambo na hili la Yesu alihitaji damu ya mwanaye (binadamu aliyemuumba yeye kujipatanisha na yeye mwenyewe!)
3.is ameaditor the same as a messanger?-Mpatanishi Kristo Yesu ana TITLES mbali mbali ikiwamo hiyo ya Messanger,sababu alikuwa katumwa na Mungu,title Zingine ni PRINCE OF PEACE,Njia,MWANA WA MUNGU,MWALIMU,KUHANI,MWANA KONDOO,MPATANISHI