cocochanel
Platinum Member
- Oct 6, 2007
- 28,999
- 79,190
Ipo YouTube.. mmmmmh.. mali jina mali!!!
Nilisha nunua vail ninakusubiri kumbe huna mpango huo!Sina mpango wa kuoa kabisa,
Sasa mkuu hapo unamlaumuje mwanamke kwa kutokutunza siri ya mumewe wakati hata mumewe hakutunza siri alimwambia mzee wake, anajuaje kuwa mzee wake hatokuja kuitumia against him siku moja? Kama umeshindwa kutunza siri yako mwenyewe utawalaumuje wengine kutokukutunzia siri? Kila choice ina consequence yake, one must own it!Umenikumbusha Story Moja hivi mtu na mkewe walikuwa home sasa pale maeneo ya kwao walisikia kama kitu kinapekecha ukuta wao wa michongoma,sasa baba mwenye nyumba akajua ni nguruwe pori sasa ikabidi achukue mkuki na kuurusha lahaula kumbe alikuwa mtu mpita njia baada ya kwenda kuangalia mtu chali akawa amefariki,daa ikabidi kuficha siri wamchukue kimya kimya wakaenda pembeni ya mwembe wakachimba shimo wakamfukia kupoteza ushahidi ikawa imeisha hiyo.
Sasa Kuna siku Jamaa alienda kumtembelea Mzee wake ndio akampa story kwamba alipata janga la kuua mtu kibahati mbaya ila alimfukia hakuna mtu aliyejua,akamuuliza wakati unamzika mkeo alijua? Akamwambia ndio anajua hadi sehemu tulimpomzika,Mzee wake akamwambia hapo umefanya bonge la kosa ,nenda kamfukue ile maiti ya mtu uzike mbwa halafu ile mifupa ya mtu kaifukie sehemu nyingine ,kweli jamaa alivyorudi akafnya kama alivyoelekezwa na mzee wake.
Kuna siku ulitokea mzozo kati yake na mkewe,basi mkewe akaanza kupayuka kwamba aliua kwa kumpiga mtu mkuki na kumzika chini ya mwembe akaanza kutangaza na kwenda kwa mtendaji mara polisi,wakaja kweli wakamuhoji akasema mkewe anamsingizia tu kisa wamegombana yeye alikuwa na mbwa tu bahati mbaya mbwa akafa ndio akamzika hapo chini ya mwembe,mkewe akasema hapana muongo ikabidi polisi na madktari wafukue wakaangalia kwenye lile shimo wakakuta mifupa ya mbwa na hapo ndio ikawa salama ya jamaa.
Kweli wanawake kwenye siri mkigombana tu anakiwasha.
Japokuwa umeongea kwa hasira mpaka umepoteza maana ya watu kuoana lakini una hoja kubwa hapa, huyo dada angeridhika na alichopewa sababu sio walichochuma wakiwa pamoja. Kumharibia huyo mwanaume hakumsaidii kitu.Wanawake wengi wanakuja kipindi cha mavuno lkn ukiwakuta mishipa ya shingo imewatoka eti tumetafuta wote. Yaani mtu asomeshwe na wazazi wake mpaka amalize chuo, apambane aingie Tra, anakuja kukuoa kipindi cha mavuno (payback period) halafu unasema mlitafuta wote, na hao wazazi wake waliohangaika nae nao wasemeje? Hivi kwa mfano akipelekwa ndani kwa kula rushwa utasema pia rushwa mlikula wote? Acheni hizo bana, ridhikeni na kidogo mtakachopewa, kama jamaa kaamu kutoa nyumba ya Tuangoma pokea sio ung'ang'anie ya Mbezi. Hata asingekuoa wewe hizo mali angepata tu, labda kama huko Tra ulimuingiza wewe
Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Nikiona hivi visanga, vinanipa nguvu kila mali yangu kuiandika kwa jina lala mama yangu na baba yangu.. maana wana mama hawatabiriki
Kabisa mkuu.Wanawake kutunza siri ni jambo gumu sana..
Nikiona hivi visanga, vinanipa nguvu kila mali yangu kuiandika kwa jina lala mama yangu na baba yangu.. maana wana mama hawatabiriki
Ni bora ipotelee kwenye familia yangu, kuliko familia ambayo haito kuwa na uchungu na mie. Alafu sio lazima watangulie wazazi, naweza tangulia mie piaUbaya lifespan yao sio kubwa be careful. Inapokuja swala la mali don’t trust anyone
Akaona isiwe shida wao wamemwaga mboga yeye kamwaga ugaliUgomvi wao mpaka mama mkwe wake yumo ndg wa mme wamo wote walikuwa hawamtaki
Hyo mwanamke ashachezea hadi mkongoto toka kwa ndg wa mme walikuwa wanamfukuza hawamtaki
Ova
Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Wanawake hajaubwa kutunza siri,Leo nilikua natizama kipindi kinaitwa “Darajani” cha Clouds Plus TV. Kuna mama anaitwa Celvina Damas anadai mumewe kamfukuza kwenye nyumba waliojenga Mbezi Beach. Hii habari nimeona tena TBC na nyumba imeoneshwaView attachment 1690156
Kitakachompomza huyu mumewe kwa majina ya Nsaji Raphael Mwanjali ni huyu mkewe kudai kwamba wana nyumba Tabata, Twangoma na maeneo mengine. Ameenda mbali na kudai kwamba hizi nyumba ameandika majina ya ndugu zake. Alikua akidai hataki ofisini (TRA) wamfuatilie.
Nina mshauri baharia mwenzetu haya mambo aachane nayo. Akubali tu kumuachia mkewe hiyo nyumba ya Mbezi Beach.
SHERIA ya Takukuru inasema kumiliki mali inayozidi kipato chako creates rebuttable presumption of public swindling. Ni juu yako kuthibitisha mali hizo hujazipata kwa rushwa, ukwapuzi, ulanguzi, magendo na magumashi ya kazini.Inawezekana dogo kanunua Ile nyumba kwa pesa halali kabisa, lkn sasa hivi wengi wanajua Ni pesa ya rushwa
Uko sahihi kabisa.Laana za kuidhulumu hela za watu. Maafisa wa TRA wengi wanaishia kwa kudhulumu hela za watu kwa kisingizo cha kukusanya kodi
Jamaa boya, unaanza maisha na mke halafu wataka kubwaga na watoto wenu bila kumuachia chochote?! Wanaume hatuachi hivyo aise, huyu mama lazima apewe haki zake, huyo kigogo kazinguwa sana sana...msimlaumu huyo mwanamke, jamaa ndio kazingua sio vizuri kumfukuza mwanamke uliyepambana nae kutafuta maisha
na sasa hivi jiwe ana hasira sana atapita na kichwa hiko cha jamaa
Kabisa kabisa...SHERIA ya Takukuru inasema kumiliki mali inayozidi kipato chako creates rebuttable presumption of public swindling. Ni juu yako kuthibitisha mali hizo hujazipata kwa rushwa, ukwapuzi, ulanguzi, magendo na magumashi ya kazini.
Taratibu tutarudi tulipoanzia miaka ya mwanzo ya nchi hii, ilipoeleweka wazi kwamba kazi ya umma ni wito na ukafara, sio mahala pa kutajirikia. Kutajirika nenda sekta binafsi.
Mdomo uliponza kichwa.Kumbe tunajitahidi kukamuana kodi,nae jamaa anazichota tu kujenga mahekaluTunaponzwa mweee
Mungu akikuita tegemea wanao kuwa omba omba maana hao ndugu zako watatimua.Kuna mambo yasiwe Siri kwa usalama wa watoto.Baba wakubwa/wadogo,Mashangazi/Wajomba nao si salama.Mkeo asijue Siri zako
Wewe na huyo mkewe lenu moja. Umetaja na jina kabisa! Hivi unafikiri nini?Leo nilikua natizama kipindi kinaitwa “Darajani” cha Clouds Plus TV. Kuna mama anaitwa Celvina Damas anadai mumewe kamfukuza kwenye nyumba waliojenga Mbezi Beach. Hii habari nimeona tena TBC na nyumba imeoneshwaView attachment 1690156
Kitakachompomza huyu mumewe kwa majina ya Nsaji Raphael Mwanjali ni huyu mkewe kudai kwamba wana nyumba Tabata, Twangoma na maeneo mengine. Ameenda mbali na kudai kwamba hizi nyumba ameandika majina ya ndugu zake. Alikua akidai hataki ofisini (TRA) wamfuatilie.
Nina mshauri baharia mwenzetu haya mambo aachane nayo. Akubali tu kumuachia mkewe hiyo nyumba ya Mbezi Beach.