Umenikumbusha Story Moja hivi mtu na mkewe walikuwa home sasa pale maeneo ya kwao walisikia kama kitu kinapekecha ukuta wao wa michongoma,sasa baba mwenye nyumba akajua ni nguruwe pori sasa ikabidi achukue mkuki na kuurusha lahaula kumbe alikuwa mtu mpita njia baada ya kwenda kuangalia mtu chali akawa amefariki,daa ikabidi kuficha siri wamchukue kimya kimya wakaenda pembeni ya mwembe wakachimba shimo wakamfukia kupoteza ushahidi ikawa imeisha hiyo.
Sasa Kuna siku Jamaa alienda kumtembelea Mzee wake ndio akampa story kwamba alipata janga la kuua mtu kibahati mbaya ila alimfukia hakuna mtu aliyejua,akamuuliza wakati unamzika mkeo alijua? Akamwambia ndio anajua hadi sehemu tulimpomzika,Mzee wake akamwambia hapo umefanya bonge la kosa ,nenda kamfukue ile maiti ya mtu uzike mbwa halafu ile mifupa ya mtu kaifukie sehemu nyingine ,kweli jamaa alivyorudi akafnya kama alivyoelekezwa na mzee wake.
Kuna siku ulitokea mzozo kati yake na mkewe,basi mkewe akaanza kupayuka kwamba aliua kwa kumpiga mtu mkuki na kumzika chini ya mwembe akaanza kutangaza na kwenda kwa mtendaji mara polisi,wakaja kweli wakamuhoji akasema mkewe anamsingizia tu kisa wamegombana yeye alikuwa na mbwa tu bahati mbaya mbwa akafa ndio akamzika hapo chini ya mwembe,mkewe akasema hapana muongo ikabidi polisi na madktari wafukue wakaangalia kwenye lile shimo wakakuta mifupa ya mbwa na hapo ndio ikawa salama ya jamaa.
Kweli wanawake kwenye siri mkigombana tu anakiwasha.