Huyu Kamanda wa Jeshi anatukera sana wakazi wa Mbezi

Habari wana jamvi,

Kwa wale wakazi wenzangu wa Mbezi Beach, Kunduchi, Goba na watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kwa ujumla
bila shaka Mtakuwa mmekutana na huyu Kamanda wa Jeshi (Chief of Staff) ambaye kuanzia majira ya kila siku Asubuhi 12:30- 1:00 hutugandisha kwenye foleni kwa muda mrefu kila siku akisubiriwa kupita yeye na ma MPs wake wanaoning'inia kwenye milango bila sababu ya Msingi na wakati mwingine waki ning'inia na Bunduki na mavazi kama tuko Afghanistan...wakifokea watu barabarani kukaa pembeni tena wakiwa kwenye wrong Lane!

Binafsi ananikera sana, kama anahitajika kufika ofisini mapema si atoke mapema kama wengine...:mad: au ndio Madaraka ya Kulevya?
Kuna siku niliwahi kuongozana na gari ya Waziri wa Ulinzi toka Uwanja wa ndege wa Dsm hadi hadi nilipofika Mwenge nao wakiwa kwenye foleni bila hamaki wala papara.

Hebu mfikishieni salamu huyu Kamanda, awaambie walinzi wake kuwa wastaarabu na kutotukera wananchi.
Chief of staff ni mnazimu Mkuu wa JWTZ ni kiongozi wa ngazi za juu Kabisa katika usalama wa Nchi hii, ndio mtu wa kwanza kujua idadi ya dhana za kivita. Ninachokuona ww unachokereka zaidi ni namna MPs wanavyomlinda, ndugu utaumia roho yako bure, na ww kama unajua Kabisa kuwa muda furani lazima mkuu apite Kwa nini usiwe unawahi mapema? Ili huo msafara usiwe unakukuta
 
Hahahahahaha....aise nimecheka kwa nguvu mno, kidogo nidondoke kwenye kiti, hahahahaha..
Laana za kunyanyasa raia hizo...
Hahahahahha...ni shida kwa kweli...ungerekodi mkuu tucheke zaidi...:D:D:D
Wewe ningerekodi wangeniambia sukuma kwa pua

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Niliwahi kukutana na davis mwamunyange kwenye foleni tena akiwa hana ata gari yenye 4 stars plate number nilimgundua alivyofungua kioo ndio nkampungia mkono CDF huyu makini kabisa kupata kutokea ktk nchi hii
Nilimuonaga msibani moro,jamaa mpole hata kuongea,anasalimiana na watu kwa unyenyekevu, nikajiuliza hivi huyu ni mkuu wa majeshi kweli? Aiseee..!
 
Sijasema hana msafara, ila sio huo wa kukuta watu eti wananing'inia na mi bunduki, mfano mzuri enzi zile za mwamunyange, waulize watu wa mbezi beach, walikuwa wanashangaa kama ni yeye ndio anapita hakuna mishemishe kabisa!! Hayo mambo ni hulka ya mtu, tu ndio maana akistafu anapata shida sana, mwisho wa siku lazima awahi kufa!! Tungepata na kabila lake huyo tungeweza kwenda mbele zaidi inawezekana analaumiwa bure tu
Jamaa anatoka zake Kilongawima wala hata hana Mbwembwe ...jioni akiwa nyumbani baada ya kazi anaingia kwenye kigari chake fulani hivi anasogea Jangwani Sea breeze meeting point na kidemu fulani cha bahari beach alichozaa nacho yupo Uk muda tu

Story mbili tatu anamuachia dolari huyoo anasepa zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana jamvi,

Kwa wale wakazi wenzangu wa Mbezi Beach, Kunduchi, Goba na watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kwa ujumla
bila shaka Mtakuwa mmekutana na huyu Kamanda wa Jeshi (Chief of Staff) ambaye kuanzia majira ya kila siku Asubuhi 12:30- 1:00 hutugandisha kwenye foleni kwa muda mrefu kila siku akisubiriwa kupita yeye na ma MPs wake wanaoning'inia kwenye milango bila sababu ya Msingi na wakati mwingine waki ning'inia na Bunduki na mavazi kama tuko Afghanistan...wakifokea watu barabarani kukaa pembeni tena wakiwa kwenye wrong Lane!

Binafsi ananikera sana, kama anahitajika kufika ofisini mapema si atoke mapema kama wengine...:mad: au ndio Madaraka ya Kulevya?
Kuna siku niliwahi kuongozana na gari ya Waziri wa Ulinzi toka Uwanja wa ndege wa Dsm hadi hadi nilipofika Mwenge nao wakiwa kwenye foleni bila hamaki wala papara.

Hebu mfikishieni salamu huyu Kamanda, awaambie walinzi wake kuwa wastaarabu na kutotukera wananchi.
Chunga sana. Narudia chunga sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom