Huyu Kamanda wa Jeshi anatukera sana wakazi wa Mbezi

Mkuu mimi ni mzoefu Wa hiyo barabara tangu enzi za mkwere kila asubuhi na jioni lazima kunakuwa na ving'ora vya hawa wajomba na tulishazoea huo utaratibu, mkuu all in all heshimu mamlaka husika hasa hawa mabaka mabaka ukileta ujuaji mwingi hawakawii kukufundisha adabu mpaka uhame mji na kuwachukia milele, mbona misafara ya rais mnapigishwa foleni mpaka Masaa mawili hulalamiki?
Mbona unamtaja rais kimzaha mzaha hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kumbuka hali ya barabara zetu mwaka 2003 hakukuwa na msongamano kama uliopo sasa, mama Maria nyerere hakuwaga na mshahara ila now mama majaliwa anamsafara
sio uongo
mimi binafsi wakati nasoma Tambaza high school 2003 tulikuwa tunamuona CDF General george waitara na gari yake 4 star akiingia ngome kila siku hakuwa ma vingora wala mbwembe kama za siku hizi, tuliwahi kumpungia mkono na yeye akarudisha salamu.
mwaka huu nilikutanana chief of staff YH Mohamed dodoma anamsafara kama wa magari 5 na MP wa kutosha,tena barabarani kila kona ya dodoma Millitary police wanafanya kazi za trafiki polisi, nilibaki na duwaa ni kajisemea zama zimebadilika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa jamaa kweli wanapaswa kuwa na walinzi lakini wakati mwingine wana exaggerate zaidi
Kuna siku natoka hotel moja kubwa nipo nje wakatoka mp wawili mmoja anaangalia kushoto mwingine kulia yaani utafikiri tunavamiwa yaani kama wana act movie kabisa na mimi nikajisemea sijui nilale chini ku take cover maana na mimi sio wa spotispoti
Basi katoka bosi na mbembwe zote zile gari likakataa kuwaka
Mimi bado naangalia movie tu

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
nimecheka sana
 
Nilishawahi kukaa foleni Mbagala tukitokea Mtwara, enzi ile Kibiti imekuwa kibiti, CDF Mabeyo naye alikuwa akitoka huko kusini akawa nyuma yetu na ilikuwa mida ya saa 2 usiku. Alikuwa na MPs lakini kwenye magari sio kuning´inia. Tulikaa pale foleni imeshona haivuti masaa mawili.

Walichofanya, MPs walishuka wakasimama kuzunguka gari yake, wengine wachache wakakimbia huko mbele kutafiti tatizo ni nini. Mmoja akiwa dirishani kwetu akampigia mkuu wa trafiki kumwambia CDF amekwama barabarani.
Gafla palimwagika askari, wakamchepulia njia wakauondoa msafara wake. Kuhoji trafiki akasema kiusalama na hali ya Kibiti, ni hatari CDF kuwa pale muda mrefu vile na lile giza. Na sie mdogo mdogo tukavutwa tukatoka.
Kulikuwa hakuna ajali wala nini, ukorofi tu wa madereva kuzibiana na kukomoana.
 
66 Reactions
Reply
Back
Top Bottom