Huyu Jerry Muro ana matatizo gani jamani?

Huyu Jerry Muro ana matatizo gani jamani?

jerry murro hakika ana mfadhaiko wa akili. yafaa yanga wamteme kabla hajawaletea na wao mfadhaiko. ni mtu mwenye majigambo ya kijinga na dharau kwa watu wema wasiokua na hatia yoyote. ni wale watu wanaojidai eti wanajitambua huku ni nyumbu wa kusaka malisho tu. ukisikia alivyohorojoka kwa maneno ya ovyo hakika utamuonea huruma.
 
huyu anahitaji kuadhibiwa, na pia kama kuna kifungu cha sheria ya makosa ya jinai amekiuka ni bora aburuzwe mahakammani, polisi waangalie kama amekiuka sheria ili wamfikishe tena kisutu mara moja. kadili siku zinavoenda ndivyo muro anavyozidi kudidimia. sasa kwa kauli kama hiyo, akiondolewa yanga, na vipindi vyake vile ya TRA vya kudandia, atakuwa wapi? halafu mwezi uliopita nilikutana naye barabarani, anaendesha gari zile mark II za zamaniii, ile gari ambayo mtu akiichoka anaipeleka kimara mwisho ipeleke watu kwa komba au sweken ndani ndani huko, gari imechokaaa, ndiyo anayomringishia mwenzie hadi anamtukania ngozi yake ambayo Watanzania tunapiga vita unyanyasaji wa albino, tumedharaulika kama nchi kutokana na manyanyaso dhidi ya albino, na jerry muro anakuja leo kuongea utumbo kama huo anazidi kuidhalilisha nchi. mtu anayewachukia albino hadi kuongea kitu kama hicho hadharani kwenye vyombo vya habari atashindwaje akiwa sirini kuwaua? hana maana.
 
Tatizo liko Yanga
Manji anaiendesha anavyotaka
uchaguzi hakuna...yeye mwenyewe hata klabuni hafiki
anaiendesha club kwa simu tu
sasa ndo maana hakuna kudhibitiana wala kuwekana sawa
 
mh.......Maskini akipata Tutakoma waswahili....pole zake kwa ujinga wa kiwango cha Masters anachojivunia...sie bekitatu wetu kagraduate mastar yake juzi tu Mzumbe so what so special abt mastar or phd nowdayz??????
baada ya ku graduate anaendelea na kazi yake au kaacha??
 
Siku ile tu wabongo watajua elimu ni nini hapo ndio tutaelimika. Inasikitisha sana wakati huu elimu ya bongo imepanuka vyuo vingi wahitimu hao wasomi wengi ndio kwanza ujinga unakithiri.

We're a doomed helpless and hopeless nation

Elimu Elimu Elimu

Maniner zetu!
 
Siku ile tu wabongo watajua elimu ni nini hapo ndio tutaelimika. Inasikitisha sana wakati huu elimu ya bongo imepanuka vyuo vingi wahitimu hao wasomi wengi ndio kwanza ujinga unakithiri.

We're a doomed helpless and hopeless nation

Elimu Elimu Elimu

Maniner zetu!



Na still wengine hawatakuelewa
 
Masuala ya Manara na Muro yasiwaumize vichwa, labda hili suala la kuongelea ulemavu wa Manala lakini haya mengine ni kawaida yao.
 
[QUOTEx=GENTAMYCINE;14903487]Anajiita kama siyo kujinasibu kuwa yeye ni msomi sana kwa kuwa ana master's degree ya Public Administration na kwamba ana mafanikio lukuki tu ya kimaisha.

Jana ktk press conference pale Jangwani msemaji wa klabu ya yanga jerry muro hakika alitufanya watu wenye akili zetu tena zilizotukuka tuwe na mashaka nae ya kitaaluma na kiuweledi kutokana na kile alichokifanya ambacho nashukuru hakikumfurahisha kila mtu aliyekuwepo pale na hasa hasa wana Yanga wenzake wale wenye uwezo wa kuchambua masuala.

Hivi ni kweli Jerry Muro anajua majukumu hasa ya afisa habari au afisa uhusiano au meneja mahusiano au kurugenzi ya habari, uhusiano na mawasiliano?


Yaliyonifanya hadi nikaamua kuanzisha huu uzi ni kitendo chake ambacho binafsi naweza kukiita ni kama vile ameibaka taaluma na ikiwezekana upesi na haraka sana atuombe radhi wana taaluma na hapa ndipo tutapima uimara wa uongozi wa klabu ya Yanga kama utamwajibisha au na wenyewe utaungana nae Jerry Muro.

Jana pale mkutanoni Jerry Muro wakati akijibu maswali ya wanahabari, ghafla akapotoka ktk hoja ya msingi na kuanza kumjibu hovyo msemaji wa klabu ya Simba, Hajji Manara.


Na ili muyaamini haya niyasemayo naomba kama una mwandishi yoyote wa habari ambaye jana alikuwepo pale ukumbini, muulize maneno machafu, ya kejeli, kudhalilisha, ya kishamba na sifa ambayo Muro alikuwa akiyasema pale.

Hapa nitayasema kisha nitawaombeni nanyi humu mnisaidie kuniambia, je msemaji wa timu au taasisi hivi ndivyo anavyotakiwa kutekeleza wajibu wake?

Maneno yenyewe ni kama haya yafuatayo:

" Kwanza huyo Manara ni mpuuzi kabisa na wa hovyo "
" Mtu anakaa uswahilini ataweza kushindana na mimi niishie Mbezi beach? "
" Mimi namiliki gari la kifahari ambalo yeye hana na hatoweza kuwa nalo "
" Isitoshe nina elimu kubwa ya masters degree ambapo yeye hata diploma tu tatizo "
" Nina uwezo sasa hata wa kuoa mwanamke wa kizungu kwa kuwa mimi ni wa kimataifa zaidi "
" Hawa watu wenye hizi ngozi ni matatizo makubwa ndiyo maana tunawasaidia kuwalinda "
" Afisa habari gani kutwa anashinidia mihogo pale Magomeni Kagera? "

Hayo hapo juu ndiyo maneno ya msemaji wa Yanga aliyoyasema jana ktk press conference, ila kutokana na pengine hao waandishi kumwogopa au kumpotezea hakuna aliyeyasema au hata kuyazungumzia isipokuwa chombo kimoja tu cha Magic Fm kipindi cha jana usiku. Na nimeamka leo asubuhi hii nikijua kuwa wale waandishi niliowaona jana pale wangeandika hii kitu na kukemea kwa maslahi na maendeleo ya mpira wetu. Cha kushangaza, hakuna print media yoyote iliyoandika hivyo!


Kidume nimeamua kujilipua kama kawaida yangu. Na kwa wale mtakaodhani hizo kauli nilizoziweka hapo juu Jerry Muro hakuzisema, nawaombeni watafuteni waandishi wa habari za michezo wawapeni uthibitisho kamili.

Na cha kuchekesha zaidi, hizo kauli chafu zote alizitoa baada tu ya kuulizwa kuwa je, anasemaje kuhusu malalamiko ya timu za Simba na Azam kuwa Yanga inapendelewa na TFF, baada ya TFF kuyafanyia haraka sana marekebisho ya wachezaji wa kigeni, yaliyowaruhusu wachezaji wote wageni waliokuwa na matatizo na taratibu za vibali vya kucheza ligi kuu kuanzia leo, wakati kabla ya mechi ya Simba na Azam klabu ya Simba ilihangaika huko huko TFF ili wachezaji wake Paul Kiongera na Brian Majwega wacheze lakini TFF ikaikatalia Simba tena hadi kwa vitisho?

Nimetema nyongo rasmi na nawaachieni intellectuals na academicians mliopo humu muweze kujadili zaidi, ila naiomba klabu ya Yanga iliangalie suala hili kwa umakini mkubwa mno hasa kwa huyu msemaji wao kwani akiachwa aendelee kuwa na hizi lugha zisizo na staha kuna siku mpira wetu utachafuka na hata kusababisha machafuko makubwa na hadi vifo.


Binafsi nimesikitika mno!​
[/QUOTE]KWANZA.NAOMBA RADHI YALE MANENO SITUYEYE NIMEFANYAKAZI NAKINA.MURO WAKO KTK HALIZILE SIKUZOTE..SO UKIFWATILIA SANA N KAMA CANSER YA UKOO UNAJUA CANCER ILIVYO..TUNAJUA NA FB TUMEMSIKIA TUNAOMBA RADHI NAAMINI TFF WAMEMWITA JANUARY BAADA YA SIKUKUU..IKUMBUKWE ALISHAADHIBIWA MIL 5KWA MANENO MACHAFU NA NAFIKIRI MANARA ANA AKILI UKITAKA KU WIN JUA WEAKNESS YA ADUI YAKO NA.MANARA AKUKOSEA..HAYO TUWAACHIE TFF JAN...YANGA 4..TAMBWE MABAO KAONDOKA NA MPORA MENGINE MWANAHISA ITD VANGAAL WANAMTANGAZIA KICHINJO KESHOO SAKUMI YA TANZANIA NAMUWISH KILA LA KHERI..
 
hapana kama ni kweli yanga wenyewe ki uungwana kabisa wamwombe radhi manara na waranzania ki ujumla huu ni ubaguzi ambao dunia ya watu wastarabu hatupendi
 
Huo ndio utani wa jadi. Ningeshangaa sana kama angemmwagia sifa mpinzani wake lakini kwa hili yuko sawa tu.
 
Kilichobaki ni Yanga kumwajibisha Jerry au Jerry kujiwajibisha mwenyewe. Vinginevyo ni kususa kutazama mechi za Yanga labda ziwe za 'fungulia mbwa'
 
Na Hata SIKU MOJA USIJIFANANISHE Wewe Na Mimi Na FAHAMU Kuwa IMPACT Yangu Ktk Jamii Ni Kubwa Mno Na Ya KUTUKUKA Na Ili ULIAMINI Hilo Tayari TFF WAMESHACHUKUA Hatua Baada Ya Kusoma Nilichokiandika Humu Leo Kupitia Huu Huu UZI Wangu Na Huyo Ndiyo GENTAMYCINE, Nimemaliza.

We boya tu...huna lolote
 
Lakini hata msemaji wa Simba nae huwa anamaneno ya "Shombo" ila kwa vile wao wa mchangani huwa watu hawawasikilizi lakini yakisemwa na Jerry wa Kimataifa watu wanayashadadia.Ila kuhusu la ulemavu wake hapo ameteleza tu lakini kwa vile swala lake limefika Tff bas atapewa nafasi ya kujitetea.
Pia mtoa mada inaonekana ulikuwepo kwenye huo mkutano wa muro bas ulishindwa kurekod hata sauti utuwekee humu hadi utakae kuomba msaada kwa waandishi wengine nawe tukisema unamuogopa Muro tutakua tumekosea?
Asante.
 
Ingekuwa vyema kama ungemhoji on the spot, kitendo cha kukimbilia jf na id yako fake ni kuendelea kuonesha uoga na kuto kujiamini kitaaluma mbele ya jerry muro, pia ni kiherehere na umbea ndio umeweka mbele . Kifupi ni kwamba wasomi hatuto zingatia andiko lako
Usomi wako hauna tofauti na mwendesha gari la taka.
Mtu kaleta hoja nzito mlemavu kadhalilishwa wewe unamtaka akamuhoji?
Ingekuwa nchi za wenzetu,muro hana kazi muda huu
 
Kwani hakai mbezi? hana Gari zuri? hakai mbezi? hana masters? Tuanza hapo kwanza .
 
Huo ndio utani wa jadi. Ningeshangaa sana kama angemmwagia sifa mpinzani wake lakini kwa hili yuko sawa tu.

Mkuu kuna utani wa jadi ila usivuke mipaka. Hili la kusema hawa watu wenye ngozi fulani......ndio maana tunawalinda ni lakibaguzi na si sawa. Hili hatuwezi kuacha kulikemea kwa kuamini kuwa ni utani wa jadi tu.
 
Kwani hakai mbezi? hana Gari zuri? hakai mbezi? hana masters? Tuanza hapo kwanza .

Halafu tukisema hayo ni kweli nini kitakachofuata? Na hakuna alipinga yeye kuwa na vitu vizuri ila ishu hapa ni maneno yenye viashiria vikubwa vya UBAGUZI
 
Back
Top Bottom