Huyu Jerry Muro ana matatizo gani jamani?

Huyu Jerry Muro ana matatizo gani jamani?

Mkuu Huwa Kabla Sijaanzisha UZI Humu Huwa NAJIRIDHISHA Kwa Kila Pande Na Sikurupuki. Nilipoandika Kuwa Ana Masters Degree Ya Public Administration Sijakosea Kwani Ni Kweli Huyo Msemaji Wa Yanga Alihitimu Mwaka Juzi Na Hiyo Kozi. Na Kwakuwa Umenichokoza Labda Pia Nikuambie Tu Kuwa Jerry Muro Hajasomea UANDISHI Wa HABARI Popote Bali Alisomea Hayo Hayo Masuala Yake Ya Utawala. Kwa Uthibitisho Zaidi Mtafute Mwenyewe AKUTHIBITISHIE. Na Siku Nyingine Muwe Kwanza Mnasoma CONTENT Nzima Ya UZI Na Pia Kujua CONTEXT Yake Ili Unaponihoji Nijue Kuwa Nahojiwa Na MTAALUMA Na Siyo Just A POPOMA.
Usipoangalia vizuri utakuwa kama huyo huyo Jerry Muro. Maana kwa mbali mnafanana jinsi mnavyoongea KWA KUJIAMINI!
 
Kwa kweli hata Mimi nilisikitika sana kwa jinsi alovyoongea kwakweli hajawa mstaarabu,katika hili achukuliwe hatua ili ajilinde na ulimi wake.
 
Mm ni Yanga damu lkn kwa hili napingana nalo kwa nguvu zote,kuna kitu kitakuwa hakiko sawa katika ubongo wake.
Mimi napingana na hilo la kuwagusa walemavu wa ngozi tu...

Hayo mengine ya kula mihogo na kuoa wazungu au wachina ni arrogance ambayo hata mtu kama Profesa Muhongo anayo!
 
Jamani msiliamini popoma lililotukuka tupate chanzo kingine cha habari ili tujiridhishe kabla ya kuhukumu.
 
Jamani msiliamini popoma lililotukuka tupate chanzo kingine cha habari ili tujiridhishe kabla ya kuhukumu.
uploadfromtaptalk1450571563801.png
 
Tena Naomba Mwenye Contacts Za Rais Wa TFF Jamal Malinzi, Katibu Mkuu Wa Klabu Ya Yanga Jonas Tiborowa, Rais Wa Klabu Ya Simba Evans Aveva Na Mawasiliano Ya MSEMAJI WA SIMBA Haji Manara Awafowadie Wote Hii Kitu TAFADHALI Na Ikiwezekana Hata Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dr. MAGUFULI Na Yeye Afikishiwe Hili Huku Bila Kumsahau Waziri Husika Wa Michezo Na Mkuu Wa Baraza La Michezo La Taifa Nao WAFIKISHIWE Lakini Kubwa Kuliko Yote Nitoe WITO Kwa MEDIA Zote Nchini Tanzania Hasa Wale WANAOHUSIKA MOJA KWA MOJA Na Michezo WALIVALIE NJUGA Hili Jambo au Suala Na WAKILIKALIA Kimya Nitajua Kuna Tatizo La KIUELEDI Ktk Tasnia Nzima Ya Habari Nchini Tanzania.
Usiwe na shaka, naamini TFF wameshachukua hatua...
TFF YAAMUA KUMFIKISHA JERRY MURO KAMATI YA MAADILI, KISA NI KILE MANENO YAKE KWA HAJI MANARA - SALEH JEMBE
 
Jamani msiliamini popoma lililotukuka tupate chanzo kingine cha habari ili tujiridhishe kabla ya kuhukumu.

Na Hata SIKU MOJA USIJIFANANISHE Wewe Na Mimi Na FAHAMU Kuwa IMPACT Yangu Ktk Jamii Ni Kubwa Mno Na Ya KUTUKUKA Na Ili ULIAMINI Hilo Tayari TFF WAMESHACHUKUA Hatua Baada Ya Kusoma Nilichokiandika Humu Leo Kupitia Huu Huu UZI Wangu Na Huyo Ndiyo GENTAMYCINE, Nimemaliza.
 
Itabidi ajiuzulu tu.vinginevyo anamfanya mpumbavu magufuli alieteua albino kuwa waziri
 
Itabidi ajiuzulu tu.vinginevyo anamfanya mpumbavu magufuli alieteua albino kuwa waziri

Na Hata Ktk Hizo Clips Zake Ninazoziona Na Kuzisikiliza Sasa Mitandaoni Nadhani Kimaadili ao Uwoga Hao Walioziweka Wameondoa Tu Yale Maneno Yake Makali Mengine Aliyoyasema Pale UKUMBINI Jana ILA Akatae Akubali Jerry Muro Jana Kayasema Yote Hayo Niliyoyasema Hapo Mwanzoni Kabisa Mwa UZI Wangu Na Ktk Hili WAANDISHI Wa HABARI Za MICHEZO Wote Nchini TANZANIA Wakilificha au Kulifumbia Macho Hili SUALA Nitawadharau KUNAKOTUKUKA Na Hata KUHOJI UELEDI Wao. Ameidhalilisha Mno Hiyo Profession Na Atuombe Radhi Na AWAJIBISHWE Pia Upesi Na Haraka Na Nimesifu Response Ya MSEMAJI Wa Simba Haji Manara Aliyoitoa Hivi Punde Kuwa " HATOMJIBU CHOCHOTE Jerry Muro ILA Anamwachia Mwenyezi Mungu ".
 
Anajiita kama siyo kujinasibu kuwa yeye ni msomi sana kwa kuwa ana master's degree ya Public Administration na kwamba ana mafanikio lukuki tu ya kimaisha.

Jana ktk press conference pale Jangwani msemaji wa klabu ya yanga jerry muro hakika alitufanya watu wenye akili zetu tena zilizotukuka tuwe na mashaka nae ya kitaaluma na kiuweledi kutokana na kile alichokifanya ambacho nashukuru hakikumfurahisha kila mtu aliyekuwepo pale na hasa hasa wana Yanga wenzake wale wenye uwezo wa kuchambua masuala.

Hivi ni kweli Jerry Muro anajua majukumu hasa ya afisa habari au afisa uhusiano au meneja mahusiano au kurugenzi ya habari, uhusiano na mawasiliano?


Yaliyonifanya hadi nikaamua kuanzisha huu uzi ni kitendo chake ambacho binafsi naweza kukiita ni kama vile ameibaka taaluma na ikiwezekana upesi na haraka sana atuombe radhi wana taaluma na hapa ndipo tutapima uimara wa uongozi wa klabu ya Yanga kama utamwajibisha au na wenyewe utaungana nae Jerry Muro.

Jana pale mkutanoni Jerry Muro wakati akijibu maswali ya wanahabari, ghafla akapotoka ktk hoja ya msingi na kuanza kumjibu hovyo msemaji wa klabu ya Simba, Hajji Manara.


Na ili muyaamini haya niyasemayo naomba kama una mwandishi yoyote wa habari ambaye jana alikuwepo pale ukumbini, muulize maneno machafu, ya kejeli, kudhalilisha, ya kishamba na sifa ambayo Muro alikuwa akiyasema pale.

Hapa nitayasema kisha nitawaombeni nanyi humu mnisaidie kuniambia, je msemaji wa timu au taasisi hivi ndivyo anavyotakiwa kutekeleza wajibu wake?

Maneno yenyewe ni kama haya yafuatayo:

" Kwanza huyo Manara ni mpuuzi kabisa na wa hovyo "
" Mtu anakaa uswahilini ataweza kushindana na mimi niishie Mbezi beach? "
" Mimi namiliki gari la kifahari ambalo yeye hana na hatoweza kuwa nalo "
" Isitoshe nina elimu kubwa ya masters degree ambapo yeye hata diploma tu tatizo "
" Nina uwezo sasa hata wa kuoa mwanamke wa kizungu kwa kuwa mimi ni wa kimataifa zaidi "
" Hawa watu wenye hizi ngozi ni matatizo makubwa ndiyo maana tunawasaidia kuwalinda "
" Afisa habari gani kutwa anashinidia mihogo pale Magomeni Kagera? "

Hayo hapo juu ndiyo maneno ya msemaji wa Yanga aliyoyasema jana ktk press conference, ila kutokana na pengine hao waandishi kumwogopa au kumpotezea hakuna aliyeyasema au hata kuyazungumzia isipokuwa chombo kimoja tu cha Magic Fm kipindi cha jana usiku. Na nimeamka leo asubuhi hii nikijua kuwa wale waandishi niliowaona jana pale wangeandika hii kitu na kukemea kwa maslahi na maendeleo ya mpira wetu. Cha kushangaza, hakuna print media yoyote iliyoandika hivyo!


Kidume nimeamua kujilipua kama kawaida yangu. Na kwa wale mtakaodhani hizo kauli nilizoziweka hapo juu Jerry Muro hakuzisema, nawaombeni watafuteni waandishi wa habari za michezo wawapeni uthibitisho kamili.

Na cha kuchekesha zaidi, hizo kauli chafu zote alizitoa baada tu ya kuulizwa kuwa je, anasemaje kuhusu malalamiko ya timu za Simba na Azam kuwa Yanga inapendelewa na TFF, baada ya TFF kuyafanyia haraka sana marekebisho ya wachezaji wa kigeni, yaliyowaruhusu wachezaji wote wageni waliokuwa na matatizo na taratibu za vibali vya kucheza ligi kuu kuanzia leo, wakati kabla ya mechi ya Simba na Azam klabu ya Simba ilihangaika huko huko TFF ili wachezaji wake Paul Kiongera na Brian Majwega wacheze lakini TFF ikaikatalia Simba tena hadi kwa vitisho?

Nimetema nyongo rasmi na nawaachieni intellectuals na academicians mliopo humu muweze kujadili zaidi, ila naiomba klabu ya Yanga iliangalie suala hili kwa umakini mkubwa mno hasa kwa huyu msemaji wao kwani akiachwa aendelee kuwa na hizi lugha zisizo na staha kuna siku mpira wetu utachafuka na hata kusababisha machafuko makubwa na hadi vifo.


Binafsi nimesikitika mno!​

Haya mikia mkakojoe mlale mmeambulia point moja Kiumba Kiongera mliye kuwa mnampamba alikuwepo pia!
 
Nimemsikia akiongea,ni maneno mabaya,watanzania hawapo hivyo:Anaringia elimu,gari,kuishi masaki?ujinga.
 
Jamani tusimshambulie yeye kama yeye bali tujikite katika hoja hizi zilizo mbele yetu kama ni za kweli ama la. Tukifanya hivyo tutaingia upuzi ule ule wa Jerry wa kumshambulia mwenzie bila kushughulikia agenda iliyokuwa mbele yake. Huo ni uvivu wa kufikiri
 
mh.......Maskini akipata Tutakoma waswahili....pole zake kwa ujinga wa kiwango cha Masters anachojivunia...sie bekitatu wetu kagraduate mastar yake juzi tu Mzumbe so what so special abt mastar or phd nowdayz??????
 
Atakula Ban Soon Tu!! Ndio Maana Alitengenezewa Kesi Ya Kuomba Rushwa!!! Mi Nilikuwa Mnatetea Ktk Hoja Zake, Ila Jana Too Much!!
 
Back
Top Bottom