Huyu Jerry Muro ana matatizo gani jamani?

Huyu Jerry Muro ana matatizo gani jamani?

Mkuu wala usiumize kichwa. Kwani ulikuwa hufahamu kuwa huyo bwana ana matatizo ya inferiority complex tokea siku nyingi?
 
duh kweli huu mwaka wa mabadiliko yaan hadi popoma anakemea waropokaji ama kweli kuna kubadilika. Huyo jerry mshamba tu nae
 
Manara naomba uchukue hatua stahiki, this is too much kwa Muro yaani jana nilivyokuwa nasikiliza sikuamini masikio yangu daah ni aibu kwa kweri mpira unakuwa kama taarabu!
 
" Kwanza Huyo Manara Ni MPUUZI Kabisa Na Wa HOVYO "
" Mtu Anakaa USWAHILINI Ataweza Kushindana Na Mimi Niishie Mbezi Beach? "
" Mimi Namiliki GARI La Kifahari Ambalo Yeye Hana Na Hatoweza Kuwa Nalo "
" Isitoshe Nina Elimu Kubwa Ya MASTERS DEGREE Ambapo Yeye Hata Diploma Tu TATIZO "
" Nina Uwezo Sasa Hata Wa KUOA Mwanamke Wa Kizungu Kwakuwa Mimi Ni Wa KIMATAIFA Zaidi "
" Hawa Watu Wenye Hizi NGOZI Ni Matatizo Makubwa Ndiyo Maana Tunawasaidia Kuwalinda "
" Afisa Habari Gani Kutwa Anashinidia MIHOGO Pale MAGOMENI Kagera? "

Manara alikuwa amesema nini hata kikasababisha huyo Jery kuongea hayo maneno? Lakini hata kama angesema nini huwezi kumtuhumu mtu ambaye hahusiki na maumbile yake. Hayo maneno hayapaswi kuzungumzwa na ye yote aliyewahi kuingia darasani. Watu kama Muro ni wale wanaokuwa na kisomo lakini hawajaelimika. Manara amesamahe bure kwani huyu jamaa ni zuzu na limbukeni.
 
Mchaga wa wapi huyu anakuwa mshamba kiasi hiki???
 
Weka video tusikie hayo maneno..
 
Mchaga wa wapi huyu anakuwa mshamba kiasi hiki???

Ni kweli ameonyesha ushamba, ni gari zuri ninaishi mbezi bichi, sasa mbona bado anaajiliwa. Ukimsikia mtu anajisifia kwa anavyomiliki ni mshamba tena kupindukia, anaposema Haji hawazi miliki, yeye ndiye Mungu wake. Nani alijua Magufuri atakua rais wa nchi mwaka mmoja kabla ya uchaguzi, huyu jamaa hajamshinda haji tu kwa alivyonavyo hata hata mimi mbaya zaidi amenizidi hadi ushamba.
 
Anajiita kama siyo kujinasibu kuwa yeye ni msomi sana kwa kuwa ana master's degree ya Public Administration na kwamba ana mafanikio lukuki tu ya kimaisha.

Jana ktk press conference pale Jangwani msemaji wa klabu ya yanga jerry muro hakika alitufanya watu wenye akili zetu tena zilizotukuka tuwe na mashaka nae ya kitaaluma na kiuweledi kutokana na kile alichokifanya ambacho nashukuru hakikumfurahisha kila mtu aliyekuwepo pale na hasa hasa wana Yanga wenzake wale wenye uwezo wa kuchambua masuala.

Hivi ni kweli Jerry Muro anajua majukumu hasa ya afisa habari au afisa uhusiano au meneja mahusiano au kurugenzi ya habari, uhusiano na mawasiliano?


Yaliyonifanya hadi nikaamua kuanzisha huu uzi ni kitendo chake ambacho binafsi naweza kukiita ni kama vile ameibaka taaluma na ikiwezekana upesi na haraka sana atuombe radhi wana taaluma na hapa ndipo tutapima uimara wa uongozi wa klabu ya Yanga kama utamwajibisha au na wenyewe utaungana nae Jerry Muro.

Jana pale mkutanoni Jerry Muro wakati akijibu maswali ya wanahabari, ghafla akapotoka ktk hoja ya msingi na kuanza kumjibu hovyo msemaji wa klabu ya Simba, Hajji Manara.


Na ili muyaamini haya niyasemayo naomba kama una mwandishi yoyote wa habari ambaye jana alikuwepo pale ukumbini, muulize maneno machafu, ya kejeli, kudhalilisha, ya kishamba na sifa ambayo Muro alikuwa akiyasema pale.

Hapa nitayasema kisha nitawaombeni nanyi humu mnisaidie kuniambia, je msemaji wa timu au taasisi hivi ndivyo anavyotakiwa kutekeleza wajibu wake?

Maneno yenyewe ni kama haya yafuatayo:

" Kwanza huyo Manara ni mpuuzi kabisa na wa hovyo "
" Mtu anakaa uswahilini ataweza kushindana na mimi niishie Mbezi beach? "
" Mimi namiliki gari la kifahari ambalo yeye hana na hatoweza kuwa nalo "
" Isitoshe nina elimu kubwa ya masters degree ambapo yeye hata diploma tu tatizo "
" Nina uwezo sasa hata wa kuoa mwanamke wa kizungu kwa kuwa mimi ni wa kimataifa zaidi "
" Hawa watu wenye hizi ngozi ni matatizo makubwa ndiyo maana tunawasaidia kuwalinda "
" Afisa habari gani kutwa anashinidia mihogo pale Magomeni Kagera? "

Hayo hapo juu ndiyo maneno ya msemaji wa Yanga aliyoyasema jana ktk press conference, ila kutokana na pengine hao waandishi kumwogopa au kumpotezea hakuna aliyeyasema au hata kuyazungumzia isipokuwa chombo kimoja tu cha Magic Fm kipindi cha jana usiku. Na nimeamka leo asubuhi hii nikijua kuwa wale waandishi niliowaona jana pale wangeandika hii kitu na kukemea kwa maslahi na maendeleo ya mpira wetu. Cha kushangaza, hakuna print media yoyote iliyoandika hivyo!


Kidume nimeamua kujilipua kama kawaida yangu. Na kwa wale mtakaodhani hizo kauli nilizoziweka hapo juu Jerry Muro hakuzisema, nawaombeni watafuteni waandishi wa habari za michezo wawapeni uthibitisho kamili.

Na cha kuchekesha zaidi, hizo kauli chafu zote alizitoa baada tu ya kuulizwa kuwa je, anasemaje kuhusu malalamiko ya timu za Simba na Azam kuwa Yanga inapendelewa na TFF, baada ya TFF kuyafanyia haraka sana marekebisho ya wachezaji wa kigeni, yaliyowaruhusu wachezaji wote wageni waliokuwa na matatizo na taratibu za vibali vya kucheza ligi kuu kuanzia leo, wakati kabla ya mechi ya Simba na Azam klabu ya Simba ilihangaika huko huko TFF ili wachezaji wake Paul Kiongera na Brian Majwega wacheze lakini TFF ikaikatalia Simba tena hadi kwa vitisho?

Nimetema nyongo rasmi na nawaachieni intellectuals na academicians mliopo humu muweze kujadili zaidi, ila naiomba klabu ya Yanga iliangalie suala hili kwa umakini mkubwa mno hasa kwa huyu msemaji wao kwani akiachwa aendelee kuwa na hizi lugha zisizo na staha kuna siku mpira wetu utachafuka na hata kusababisha machafuko makubwa na hadi vifo.


Binafsi nimesikitika mno!​

Hawa jamaa huwa ni watani wa jadi kwa hiyo kupigana madongo ni kawaida,ila hapo kwenye walemavu ameteleza,na muungwana anapoteleza huamba radhi,ni matumaini yangu ataomba radhi kwa kukwaza huku.
 
Tena Naomba Mwenye Contacts Za Rais Wa TFF Jamal Malinzi, Katibu Mkuu Wa Klabu Ya Yanga Jonas Tiborowa, Rais Wa Klabu Ya Simba Evans Aveva Na Mawasiliano Ya MSEMAJI WA SIMBA Haji Manara Awafowadie Wote Hii Kitu TAFADHALI Na Ikiwezekana Hata Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dr. MAGUFULI Na Yeye Afikishiwe Hili Huku Bila Kumsahau Waziri Husika Wa Michezo Na Mkuu Wa Baraza La Michezo La Taifa Nao WAFIKISHIWE Lakini Kubwa Kuliko Yote Nitoe WITO Kwa MEDIA Zote Nchini Tanzania Hasa Wale WANAOHUSIKA MOJA KWA MOJA Na Michezo WALIVALIE NJUGA Hili Jambo au Suala Na WAKILIKALIA Kimya Nitajua Kuna Tatizo La KIUELEDI Ktk Tasnia Nzima Ya Habari Nchini Tanzania.
 
Mkuu Huwa Kabla Sijaanzisha UZI Humu Huwa NAJIRIDHISHA Kwa Kila Pande Na Sikurupuki. Nilipoandika Kuwa Ana Masters Degree Ya Public Administration Sijakosea Kwani Ni Kweli Huyo Msemaji Wa Yanga Alihitimu Mwaka Juzi Na Hiyo Kozi. Na Kwakuwa Umenichokoza Labda Pia Nikuambie Tu Kuwa Jerry Muro Hajasomea UANDISHI Wa HABARI Popote Bali Alisomea Hayo Hayo Masuala Yake Ya Utawala. Kwa Uthibitisho Zaidi Mtafute Mwenyewe AKUTHIBITISHIE. Na Siku Nyingine Muwe Kwanza Mnasoma CONTENT Nzima Ya UZI Na Pia Kujua CONTEXT Yake Ili Unaponihoji Nijue Kuwa Nahojiwa Na MTAALUMA Na Siyo Just A POPOMA.

Tofauti yako na Jerry Muro ni kuwa wewe unajua kumix kidogo na maneno mengine, ila kwenye suala la KUJISIFIA na KUJIKWEZA, uko juu.
 
Mkuu Huwa Kabla Sijaanzisha UZI Humu Huwa NAJIRIDHISHA Kwa Kila Pande Na Sikurupuki. Nilipoandika Kuwa Ana Masters Degree Ya Public Administration Sijakosea Kwani Ni Kweli Huyo Msemaji Wa Yanga Alihitimu Mwaka Juzi Na Hiyo Kozi. Na Kwakuwa Umenichokoza Labda Pia Nikuambie Tu Kuwa Jerry Muro Hajasomea UANDISHI Wa HABARI Popote Bali Alisomea Hayo Hayo Masuala Yake Ya Utawala. Kwa Uthibitisho Zaidi Mtafute Mwenyewe AKUTHIBITISHIE. Na Siku Nyingine Muwe Kwanza Mnasoma CONTENT Nzima Ya UZI Na Pia Kujua CONTEXT Yake Ili Unaponihoji Nijue Kuwa Nahojiwa Na MTAALUMA Na Siyo Just A POPOMA.

sijapingana nawe...Point yangu taaluma yake haiendani na taaluma ya afisa habari.Yawezekana mi ni popoma kweli ila nina haki pia ya kuchangia.Thanks
 
Mimi skusikia chombo cha habari kikiongelea hilo lkn kama ndiyo maneno ys msemaji wa yanga hayo.....basi yanga wajipime kama ndio mwongozo wa kazi waliompa basi kazi ipo.
 
Jeri amefirisika kiasi hiki?!
Nimemdharau sana!
 
Back
Top Bottom