Huyu Jerry Muro ana matatizo gani jamani?

Huyu Jerry Muro ana matatizo gani jamani?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,602
Reaction score
127,975

Anajiita kama siyo kujinasibu kuwa yeye ni msomi sana kwa kuwa ana master's degree ya Public Administration na kwamba ana mafanikio lukuki tu ya kimaisha.

Jana ktk press conference pale Jangwani msemaji wa klabu ya yanga jerry muro hakika alitufanya watu wenye akili zetu tena zilizotukuka tuwe na mashaka nae ya kitaaluma na kiuweledi kutokana na kile alichokifanya ambacho nashukuru hakikumfurahisha kila mtu aliyekuwepo pale na hasa hasa wana Yanga wenzake wale wenye uwezo wa kuchambua masuala.

Hivi ni kweli Jerry Muro anajua majukumu hasa ya afisa habari au afisa uhusiano au meneja mahusiano au kurugenzi ya habari, uhusiano na mawasiliano?


Yaliyonifanya hadi nikaamua kuanzisha huu uzi ni kitendo chake ambacho binafsi naweza kukiita ni kama vile ameibaka taaluma na ikiwezekana upesi na haraka sana atuombe radhi wana taaluma na hapa ndipo tutapima uimara wa uongozi wa klabu ya Yanga kama utamwajibisha au na wenyewe utaungana nae Jerry Muro.

Jana pale mkutanoni Jerry Muro wakati akijibu maswali ya wanahabari, ghafla akapotoka ktk hoja ya msingi na kuanza kumjibu hovyo msemaji wa klabu ya Simba, Hajji Manara.


Na ili muyaamini haya niyasemayo naomba kama una mwandishi yoyote wa habari ambaye jana alikuwepo pale ukumbini, muulize maneno machafu, ya kejeli, kudhalilisha, ya kishamba na sifa ambayo Muro alikuwa akiyasema pale.

Hapa nitayasema kisha nitawaombeni nanyi humu mnisaidie kuniambia, je msemaji wa timu au taasisi hivi ndivyo anavyotakiwa kutekeleza wajibu wake?

Maneno yenyewe ni kama haya yafuatayo:

" Kwanza huyo Manara ni mpuuzi kabisa na wa hovyo "
" Mtu anakaa uswahilini ataweza kushindana na mimi niishie Mbezi beach? "
" Mimi namiliki gari la kifahari ambalo yeye hana na hatoweza kuwa nalo "
" Isitoshe nina elimu kubwa ya masters degree ambapo yeye hata diploma tu tatizo "
" Nina uwezo sasa hata wa kuoa mwanamke wa kizungu kwa kuwa mimi ni wa kimataifa zaidi "
" Hawa watu wenye hizi ngozi ni matatizo makubwa ndiyo maana tunawasaidia kuwalinda "
" Afisa habari gani kutwa anashinidia mihogo pale Magomeni Kagera? "

Hayo hapo juu ndiyo maneno ya msemaji wa Yanga aliyoyasema jana ktk press conference, ila kutokana na pengine hao waandishi kumwogopa au kumpotezea hakuna aliyeyasema au hata kuyazungumzia isipokuwa chombo kimoja tu cha Magic Fm kipindi cha jana usiku. Na nimeamka leo asubuhi hii nikijua kuwa wale waandishi niliowaona jana pale wangeandika hii kitu na kukemea kwa maslahi na maendeleo ya mpira wetu. Cha kushangaza, hakuna print media yoyote iliyoandika hivyo!


Kidume nimeamua kujilipua kama kawaida yangu. Na kwa wale mtakaodhani hizo kauli nilizoziweka hapo juu Jerry Muro hakuzisema, nawaombeni watafuteni waandishi wa habari za michezo wawapeni uthibitisho kamili.

Na cha kuchekesha zaidi, hizo kauli chafu zote alizitoa baada tu ya kuulizwa kuwa je, anasemaje kuhusu malalamiko ya timu za Simba na Azam kuwa Yanga inapendelewa na TFF, baada ya TFF kuyafanyia haraka sana marekebisho ya wachezaji wa kigeni, yaliyowaruhusu wachezaji wote wageni waliokuwa na matatizo na taratibu za vibali vya kucheza ligi kuu kuanzia leo, wakati kabla ya mechi ya Simba na Azam klabu ya Simba ilihangaika huko huko TFF ili wachezaji wake Paul Kiongera na Brian Majwega wacheze lakini TFF ikaikatalia Simba tena hadi kwa vitisho?

Nimetema nyongo rasmi na nawaachieni intellectuals na academicians mliopo humu muweze kujadili zaidi, ila naiomba klabu ya Yanga iliangalie suala hili kwa umakini mkubwa mno hasa kwa huyu msemaji wao kwani akiachwa aendelee kuwa na hizi lugha zisizo na staha kuna siku mpira wetu utachafuka na hata kusababisha machafuko makubwa na hadi vifo.


Binafsi nimesikitika mno!

=============================

Update

JERRY MURO KUFIKISHWA KWENYE KAMATI YA MAADILI YA TFF


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litamfikisha kwenye Kamati ya Maadlili mapema Mwakani baada ya sikukuu ya mwaka Mpya 2016, Mkuu wa Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Jerry Muro kutokana na kauli zake za kibaguzi dhidi ya Mkuu wa Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara.

Muro alimshambulia kwa maneno ya kibaguzi Manara wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika jana makao makuu ya klabu ya Yanga jijini Dar es Salaam.

Kauli ya Muro dhidi ya Manara ni kinyume na Katiba ya TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambao zinapiga vita vitendo vya ubaguzi wa aina yoyote katika mpira wa miguu.

Mapema mwaka huu, Muro alifikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kutokana na kumshambulia na kumdhalilisha kupitia vyombo vya habari aliyekuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Fatma Abdallah. Kamati ya Nidhamu ilimwadhibu kwa kumpiga faini ya sh. milioni 5.

Chanzo:Shaffih Dauda
​
 
Last edited by a moderator:
Yanga na simba haihitaji uje utumie elimu inahitaji ujue kuongea maneno ya hovyo kama hayo hongera jery muro kutokana na utawala wa hizi timu utaendelea kuwa msemaji wa yanga

Ila mm siumgi mkono maneno yake kiukweli machafu
 
Kama kweli alifika ngambo ya pili hasa kwa kundi hili la watu maalum.....
 
" Kwanza Huyo Manara Ni MPUUZI Kabisa Na Wa HOVYO "
" Mtu Anakaa USWAHILINI Ataweza Kushindana Na Mimi Niishie Mbezi Beach? "
" Mimi Namiliki GARI La Kifahari Ambalo Yeye Hana Na Hatoweza Kuwa Nalo "
" Isitoshe Nina Elimu Kubwa Ya MASTERS DEGREE Ambapo Yeye Hata Diploma Tu TATIZO "
" Nina Uwezo Sasa Hata Wa KUOA Mwanamke Wa Kizungu Kwakuwa Mimi Ni Wa KIMATAIFA Zaidi "
" Hawa Watu Wenye Hizi NGOZI Ni Matatizo Makubwa Ndiyo Maana Tunawasaidia Kuwalinda "
" Afisa Habari Gani Kutwa Anashinidia MIHOGO Pale MAGOMENI Kagera? "
 
Kama ni kweli Yanga inabidi ichukue hata Mara moja, Yanga ni taasisi kubwa. Maneno ya ubaguzi wa hali na kijamii hauwezi kuvumiliwa na taasisi kama yanga.
 
excuse mtoa post...kuna Public administration na Public relation.Ya mwanzo haiusiani na utoaji wa habari au usemaji ila ya pili ndiyo inahusika.
 
Hayo maneno yanasikitisha sana na kinachomponza jerry ni kutaka kumiga masau bwire ili naye apewe sifa lakini hana kitu kichwani na sina shaka atafukuzwa hivi karibuni
 
Kama ni kweli Yanga inabidi ichukue hata Mara moja, Yanga ni taasisi kubwa. Maneno ya ubaguzi wa hali na kijamii hauwezi kuvumiliwa na taasisi kama yanga.

Mkuu SILAHA Yangu Kubwa Ni KUWA MKWELI Na KUJIAMINI Kwa Kile Ninachokisema Na Tena Kuna Mengine Makubwa Tu ( MATUSI ) Aliyasema Pale Kama Kawaida Yake Na Kwa Mshangao Wale WAANDISHI Badala Ya KUHOJI Wao Nao Wao Wakawa WANACHEKA. Ninachokiomba Hapa Ni Kwamba Tusijadili KIITIKADI Bali Tujadili KIMANTIKI Ili Itusaidie Zaidi Kama Watu Tunaojitambua. Najua Kuwa Simba Na Yanga Ni WATANI Na Huwa TUNATANIANA Mno Tu Lakini Jerry Muro AMEZIDISHA Na Ni Kama Vile Kuna JEURI FULANI Anaipata Kutoka Sehemu Fulani au Ktk MAMLAKA Fulani. Yanga Kama KLABU Na TFF Iliangalie Na Kulichunguza Kwa UMAKINI Mkubwa Hili Suala Na Hatua KALI Zichukuliwe Na Naomba Pia Kama Kuna Sehemu Pia MSEMAJI WA SIMBA Hajji Manara Na Yeye ALISHASEMA MANENO Yasiyo Na TIJA au Ya KITAALUMA Basi Na Yeye Pia Vile Vile SIMBA Na TFF Ichunguze Na Achukuliwe Hatua Stahiki Za Kinidhamu. ILA Kitaaluma Kwa ALICHOKIFANYA Jerry Muro Jana HAKITAKIWI Na HAKIKUBALIKI Kwani Atatufanya Wenye Hiyo TASNIA Na TULIOTUKUKA Nayo TUDHARAULIKE Mbele Ya Jamii.
 
excuse mtoa post...kuna Public administration na Public relation.Ya mwanzo haiusiani na utoaji wa habari au usemaji ila ya pili ndiyo inahusika.

Mkuu Huwa Kabla Sijaanzisha UZI Humu Huwa NAJIRIDHISHA Kwa Kila Pande Na Sikurupuki. Nilipoandika Kuwa Ana Masters Degree Ya Public Administration Sijakosea Kwani Ni Kweli Huyo Msemaji Wa Yanga Alihitimu Mwaka Juzi Na Hiyo Kozi. Na Kwakuwa Umenichokoza Labda Pia Nikuambie Tu Kuwa Jerry Muro Hajasomea UANDISHI Wa HABARI Popote Bali Alisomea Hayo Hayo Masuala Yake Ya Utawala. Kwa Uthibitisho Zaidi Mtafute Mwenyewe AKUTHIBITISHIE. Na Siku Nyingine Muwe Kwanza Mnasoma CONTENT Nzima Ya UZI Na Pia Kujua CONTEXT Yake Ili Unaponihoji Nijue Kuwa Nahojiwa Na MTAALUMA Na Siyo Just A POPOMA.
 
Kama kweli alifika ngambo ya pili hasa kwa kundi hili la watu maalum.....

Mkuu Huyu Jamaa Kwa Tunaomjua Ana Mengi Makubwa Hata Zaidi Ya Haya Na Huwezi Amini Kuwa Ni Mtoto Wa Mwalimu Mama Muro Pale Ubungo. Nahisi Kuna Kitu Anatumia Si Bure!
 
Ebu muulize kama kashaacha uwizi.... Kuna kipindi alikuwa anatoka na Mkuu wa Wilaya wa Nanyunbu wakati huo akamwibia zaidi ya millioni 3...

Jerry Muro anaishi kwa ujanja ujanja tu na wala hana Masterz. Ni sidhani kama ana hata Diploma..
 
Ninadhani alisema hivyo kwa sababu alikuwa amekaa na kuhojiwa na mapopoma wenzie. PERIOD.
 
Duuuh!
Amefanya ubaguzi wa hali ya juu,
Swala zito hili sio la kuchekewa hata kidogo,
Jerry anapaswa aadabishwe,
Iwe fundisho kwake na wengineo.
 
Mkuu Huyu Jamaa Kwa Tunaomjua Ana Mengi Makubwa Hata Zaidi Ya Haya Na Huwezi Amini Kuwa Ni Mtoto Wa Mwalimu Mama Muro Pale Ubungo. Nahisi Kuna Kitu Anatumia Si Bure!

Mkuu mimi niliyasikia hayo matusi jana magic fm sikuamini nikaona ngoja nijaribu sources nyingine nikagundua kumbe alitukana zaidi ya yale niliyoyasikia magic fm.Jerry moro hafai kuendelea kuwepo kwenye ile nafasi kwa club kubwa kama yanga yenye mamilioni ya fans wa kariba mbalimbali.Hivi kuwa na masters ni ishu nowdays?kukuaa mbezi au kuoa mzungu nayo ishu ya kututangazia wanaume?kwani mzungu ana nini special kuliko dada zetu.Nitashangaa Yanga au TFF wakinyamaza kimya.
 
Hao wazungu anaowaona wa maana sisi enzi za ujana tulikua tunawanunua tuna kula mzigo na tunawaacha na mwisho tumeoa weusi wenzetu.
 
Maneno kama hayo nikawaida kwa Simba na yanga, lkn kama aligusia kwa hawa watu wa waremavu alikosea sn...
 
Mkuu Huwa Kabla Sijaanzisha UZI Humu Huwa NAJIRIDHISHA Kwa Kila Pande Na Sikurupuki. Nilipoandika Kuwa Ana Masters Degree Ya Public Administration Sijakosea Kwani Ni Kweli Huyo Msemaji Wa Yanga Alihitimu Mwaka Juzi Na Hiyo Kozi. Na Kwakuwa Umenichokoza Labda Pia Nikuambie Tu Kuwa Jerry Muro Hajasomea UANDISHI Wa HABARI Popote Bali Alisomea Hayo Hayo Masuala Yake Ya Utawala. Kwa Uthibitisho Zaidi Mtafute Mwenyewe AKUTHIBITISHIE. Na Siku Nyingine Muwe Kwanza Mnasoma CONTENT Nzima Ya UZI Na Pia Kujua CONTEXT Yake Ili Unaponihoji Nijue Kuwa Nahojiwa Na MTAALUMA Na Siyo Just A POPOMA.

Asante mkuu wasamee hawa watoto wa juzi wao kukurupuka ni jadi.tatizo wakiwa form six au first year basi wanadhani hakuna wengine wamewahi kupita hiyo level.
 
Mbona na wewe unatumia lugha isiyofaa sasa? Neno POPOMA ni la kistaarabu?
 
Back
Top Bottom