Mahusiano ya mwanaume na mwanamke ni natural pattern. Hakuna alternative. Unachokisema hapa tutarudi kwenye mabishano mengine ya kati ya mwanaume na mwanamke nani anamuhitaji zaidi mwenzake. Kumbuka tukifika uko kwenye ligi hakuna jinsia itakayoibuka mshindi kiujumla. Victims watakuwepo kila upande. Kwahiyo namna bora zaidi ni kuangalia tunatokaje hapa.
Mimi nina familia(mke na mtoto), na suala la maadili na family structure(yaani baba, mama, mtoto kila mmoja akae kwenye nafasi na wajibu wake) nalizingatia sana. Lakini haimaanishi kwamba sioni kama hii pattern tunayoenda nayo kama jamii inapeleka shimoni ustawi wetu. Hata familia yangu nikiilea kwenye uelekeo mzuri mwisho wa siku watoto watakua na kujitegemea watakutana na ulimwengu uliovulugika. Kwahiyo tukisema haimaanishi tunataka huruma,isipokua tunaonyesha ambapo hatupo sahihi. Personally am fine in almost all aspects of my life, relationship, financial, family e.t.c kwahiyo sitafuti huruma ya yoyote