Huu ni Ushuhuda wangu wa Kweli kuhusu pesa

Mwafrika mmoja

Senior Member
Joined
Mar 15, 2019
Posts
104
Reaction score
234
Katika Dunia hii ambayo wote tumezaliwa tumekuja hatuna hata soksi, kila kitu tumekikuta basi tambua kuwa hakuna kitu HAKIWEZEKANI.

Mitandao hii hii ambayo tunatumia kila siku.

Kuna watu ndiyo inawaendeshea maisha. Kuna watu wamejenga, wamenunua magari, kuna ambao hawataki kuajiriwa.

Iko Hivi !!!

Mimi nilikuwa kama wewe,

Nilikuwa naona tu watu wanasema mitandao inalipa, ila sijui wanafanyaje. Lakini siku moja nikasema nataka kujua inakuwaje ndipo nilipoamua kuchukua hatua.

Nikajifunza skills na nikafungua akaunti nikasema siachi mpaka namimi nipate pesa kama wao.

2022 nilifungua akaunti yangu ya kwanza, hapo katikati nilikata tamaa nikarudi tena mpaka nilipoanza kuingiza kipato. Sijapata kingi kama hao wakubwa lakini ninayo stori ya kushare jinsi nilivyopata $6100 ili uone kwamba inawezekana.

Kitu ninachoweza kukwambia leo ni kwamba usikate tamaa, usiogope na huu siyo utapeli. Anza sasa, jifunze na uingie kwenye mchezo na mimi niko tayari kukusaidia.

Karibu !
 
Ikiwa kweli unalengo na njia njema ya kuelimisha vijana wenzio kwa nini usitueleze ni skills zipi hizo na pia unafanya kazi katika platform zipi na mchakato mzima ukoje bila kusahau ushahidi wa picha.
 
Hivi Gwajima anaweza kukufundisha kutengeneza mafuta ya upako?.
 
Yaani nyuzi kama hizi zilitakiwa kua Facebook si Jamii Forum.. kweli JF imeshuka hadhi
Sipo hapa kumsupport mleta mada ila point yake ina mashiko. Mitandao ukijua kuitumia utatoka kimaisha.

Mfano hai mimi mwenyewe kuna jamaa nimemsahau jina lakini zamani alikuwa anaongelea mambo ya Forex na cryptocurrency. Mimi Forex siijui na wala sitaki kuigusa manake ina mambo mengi. Ila kwenye crypto nilipata hela. Pia kuna mwana hapa alitoa ideas flani ya biashara simkumbuki jamaa ila na wish nimjue nimpe asante kwa maono yake aliyo share siku ile.
 
20260625_052541.png
 
Ikiwa kweli unalengo na njia njema ya kuelimisha vijana wenzio kwa nini usitueleze ni skills zipi hizo na pia unafanya kazi katika platform zipi na mchakato mzima ukoje bila kusahau ushahidi wa picha.
Hiyo ni makusudi. Hapo anataka watu waingine DM awalize.
 
Serikali ya Samia yatenga Tzs trillion 1 kwa ajili ya safari za viongozi
Sasa wewe ulitaka watenge kiasi gani bwashee?

Maana fungu la safari linavyokuwa kubwa na sisi machawa tunaponea humo humo.

We fikiria wakati wa zile heka heka za ule uchaguzi feki wa 2025 nilipewa 300m kwa ajili ya kazi maalum.

Na baada ya kumaliza hiyo kazi "maalumu" kwa ufanisi mkubwa nikapewa 500m kama kifuta jasho.

Sasa wewe hebu fikiria mwalimu au daktari akistaafu baada ya kuitumikia serikali kwa miaka 49 analipwa 50-60m kama kiinua mgongo.

Mimi nimevuta 800m ndani ya miezi 2 tu.

Mimi nitawashauri waongeze pesa ya safari iwe angalau 4trn.
 
Sipo hapa kumsupport mleta mada ila point yake ina mashiko. Mitandao ukijua kuitumia utatoka kimaisha.

Mfano hai mimi mwenyewe kuna jamaa nimemsahau jina lakini zamani alikuwa anaongelea mambo ya Forex na cryptocurrency. Mimi Forex siijui na wala sitaki kuigusa manake ina mambo mengi. Ila kwenye crypto nilipata hela. Pia kuna mwana hapa alitoa ideas flani ya biashara simkumbuki jamaa ila na wish nimjue nimpe asante kwa maono yake aliyo share siku ile.
Asante Mkuu, wengi hawataki kuchosha akili wanataka niwaambie tu fungua hapa ukibonyeza utapata hela kwenye simu yako
 
Hiyo ni makusudi. Hapo anataka watu waingine DM awalize.
Ingia kwenye profile yangu nina nyuzi nyingi kuhusu Fiverr nimeeleza ..... ushahidi wa picha niliweka Jamiiforums wameshusha
 
Katika Dunia hii ambayo wote tumezaliwa tumekuja hatuna hata soksi, kila kitu tumekikuta basi tambua kuwa hakuna kitu HAKIWEZEKANI.

Mitandao hii hii ambayo tunatumia kila siku.

Kuna watu ndiyo inawaendeshea maisha. Kuna watu wamejenga, wamenunua magari, kuna ambao hawataki kuajiriwa.

Iko Hivi !!!

Mimi nilikuwa kama wewe,

Nilikuwa naona tu watu wanasema mitandao inalipa, ila sijui wanafanyaje. Lakini siku moja nikasema nataka kujua inakuwaje ndipo nilipoamua kuchukua hatua.

Nikajifunza skills na nikafungua akaunti nikasema siachi mpaka namimi nipate pesa kama wao.

2022 nilifungua akaunti yangu ya kwanza, hapo katikati nilikata tamaa nikarudi tena mpaka nilipoanza kuingiza kipato. Sijapata kingi kama hao wakubwa lakini ninayo stori ya kushare jinsi nilivyopata $6100 ili uone kwamba inawezekana.

Kitu ninachoweza kukwambia leo ni kwamba usikate tamaa, usiogope na huu siyo utapeli. Anza sasa, jifunze na uingie kwenye mchezo na mimi niko tayari kukusaidia.

Karibu !
Lipia tangazo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom