Huu ndio Utapeli wa "Prophet Bushiri" Anayemtishia Lowassa

Huu ndio Utapeli wa "Prophet Bushiri" Anayemtishia Lowassa

Kitabu cha Yeremia 28:16-17 kuna habari ya Nabii Yeremia kumtabiria kifo Nabii Hanania, na ikawa...

"Kwa hiyo Yehova amesema hivi, ‘Tazama! Ninakuondolea mbali kutoka katika uso wa nchi. Mwaka huu utakufa hakika,+ kwa maana umesema maasi ya waziwazi juu ya Yehova.’”+17 Basi Hanania nabii akafa mwaka huo, katika mwezi wa saba"

Wafalme wa Pili, 1: 16-17 kuna habari ya Nabii Elia kumtabiria kifo Mfalme Ahazia na ikawa...

"16 Akamwambia, Bwana asema hivi, Kwa kuwa umetuma wajumbe waulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, uulize neno lake? Kwa hiyo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.
17 Basi akafa, sawasawa na neno la Bwana alilolinena Eliya."

Hivyo usigeneralize huo mtazamo wako.Nabii wa kweli pia anaweza kutabiri kifo.
Hawa manabii uliowaweka hapa wote wa zamani, walikuwa kwenye Biblia. Mimi naongea Mapastor/Manabii hawa wa sasahivi wote matapeli nitajie mmoja alietabiri kifo cha mtu na kikawa miaka mia(100) iliopita mpaka sasa. Unakumbuka mwaka juzi kuna Nabii mmoja muogo aliesema kuwa kutatokea mauti ya rais mzee barani afrika. Alikusudia Mugabe lakini bado yupo namalizia hakuna ajuwae kifo cha mweziwe lini kinakuja labda wapiga ramli kwasababu huona giza kwenye nyota yako na ndio husema mauti yatakufika mwaka huu.
 
Soma biblia upate maarifa ya kumjua mungu, inahuzinisha sana wanadam wanashindwa kuchuja yupi mtumishi WA mungu na yupi anajifanya mtumishi WA mungu kumbe ni mateka na shetan jaman wapendwa achen kukimbilia miujiza na maombi ya msisimko wengi wao ni wakala WA shetani mtumishi WA mungu hawezi jisifu na kujitukuza Bali atamtukuza mungu alie juu,pita magoti funga na kuomba mungu wetu sio kiziwi hata asiweze sikia maombi yetu kuliko kudanganywa na manabii WA uongo,mwenye sikio na asikie
 
Nakumbuka yule transformer alitabiri waandishi wa habar kufa hadi ifikapo mda Fulani! Baada ya kumuandika anakunywa viroba..sijui unabii wake ulitimia? MUNGU aturehemu sana na hawa manabii wa uongo ni ngumu kuwatambua
Km ni msomaji mzuri WA biblia ni rahisi sana kuwatambua tatizo hatusomi tunataka kusomewa hii ni mbaya sana ndiyo maana wengi wamejikuta wakiwatukuza hao manabii kana kwamba ni mungu wao
 
Mnaorukaruka kwenye makanisa ya kuombewa mtahangaika sana tulieni ndani ya kanisa takatifu KATOLIKI la mitume
Haha ni kweli watu wanahangaika ila nalo hilo kanisa lako halina tofauti na hao wanaohangaika,soma biblia utajua mungu anataka nn na kanisa lenu linafanya yapii
 
Kwenye harakati za kutafuta uso wa Mungu watu wanaingia kirahisi kwenye mitego ya watenda miujiza feki na wengine wakitumia nguvu za giza. Ni vyema kujua historia ya mchungaji unayeabudu kwake ili walau ujue amepatia wapi daraja hilo then ndio uhamie kupima kama anahubiri injili ya kweli? ....Paulo hakuwa sehemu ya mitume lakini alipokutana na Yesu hakuanza tu kufungua Kanisa na kuhubiri bali alienda kwa mitume ambao ndio waliomuwekea mikono akafanye kazi ya Bwana. Siku hizi mtu anasema amekutana na Yesu ndotoni then anafungua Kanisa! Paulo aliyekutana nae live pengine ndio asingewasikiliza kabisa mitume ......huduma za Kanisa ni madaraja ambayo yanautaratibu wake toka enzi za Kanisa la kwanza na si mtu kuibuka tu kama mzimu .....

Na Usimfuate Mtu Kiblind Kuna watu hata Wakimkuta mtu anakula nyama ya Mtu watamfuata Bado. Kuna Wakati nakumbuka Wakati Askofu Gwajima akianza GCTC tulikuwa kama Brothers, Sijawahi kuwa na Tatizo hata moja na Gwajima. Na hata sasa namheshimu Nasema hivi Pamoja na Controversy nyingi Gwajima anasali sana, hakati Tamaa, alikuwa akifunga hata siku ishirini akinywa maji tu. Nimekuwa naye na nimemwona kwa Macho na namjua Nguvu na Ubinadamu wake Pia! Ila siku za Mwazo akaja Rafiki yake Mkorea, akawa anatufundisha Viongozi, sasa Mimi na Mwenzangu tukatatizwa na Baadhi ya Misimamo yake huyu Mkorea! Katika kumuuliza Maswali ati akawa anatutishia na Fimbo kwa Kupiga Meza! Abeee! Nikamuuliza hivi wewe ulikuja hapa TZ ukidhani Watanzania ni watu wa aina Gani hata ututishie Fimbo?
Basi Nikainuka nikamwambia Brother Gwajima, Nakuheshimu sana, Naondoka, ila asinitafute mtu, Nitakuwa nikiwaona! Gwajima hakusema Kitu alijiinamia tu na Kulia. Alikuwa katika wakati Mgumu kwani Mwanzoni huyu Mkorea alimpa Toyota Hilux, Vyombo vipya vichache na hela kidogo ya Kununulia Kiwanja cha Kanisa really ilikuwa ni Down payment Ndogo sana. Sasa Unaona Njngeweza Kumwabudu kwa Kumwogopa Yule Mkorea you know! Mind you hakuwa ni Mtu mbaya lakini kunishikia Fimbo Mtu mzima Ni Ukoloni na. Ilimkemea! It was 1996 Hatuna haja ya Kufuata watu blindly!
 
Always Christians are bunch of fools !
Dont say that, Wako wanaabudu Ngombe ambaye alizaliwa akawakuta lakini Ni Medical Prophesionals, Ni Computer scientists, Astrologers etc. Imani ni Fumbo acha Kutukana watu. Wewe si Unaamini ipo Oxygen ulishaiona au Kuishika? Nani anayemwelekeza Mtoto kula akizaliwa?
 
Bushiri ni raia wa nchi gani ?
Kwanza, tuanzie hapo!
 
Sawa natafuta, lkn size za kusema Adam na Eva walikuwa weupe ni kutokufikiri vizuri....hakuna mahali imeandikwa hivyo...

Biblia Haisemi Watu wote walitokea kwa Adamu hapo Ndipo watu wanakosea. Jiulize Adamu na Hawa Walikuwa na Watoto wawili tu Abel na cain. Cain akamuua Abel. Akalaaniwa na Mungu akakimbilia Nchi ya watu wengine huko akaoa, Walikuwa ni Kina nani hao aliokimbilia kwao na Kuoa kwao?

Biblia inasema hapo Mwanzo Maji yalitulia juu ya Uso wa Nchi, Je ni Dunia nzima au ilikuwa ni Jangwa la. Ashariki ya kati. Kisayansi Arabian Desert ilikuwa ni Sehemu ya Bahari, kama kulitokea tetemeko likasababisha mwinuko kutoka majini sijui but hiyo ni fact.
Mimi Naamini Wazungu, Wachina Wahindi wekundu na Wahindi wa Asia etc na Pengine Waafrika walikuwepo Kabla ya Adamu! Kwani Mungu aliloleta gharika la Nuhu sababu ilikuwa nini? Sio wana wa Mungu au Uzao wa Adamu waliwaoa binti za watu? Kuna Mambo mengi Biblia haituambii lakini hainamaana Mungu hakuyaumba wala hayamhusu. Je kukiwa na sayari nyingine yenye watu? Ni Adamu aliwazaa?
Wayahudi walimkataa Yesu Kwa kupitia Mtume Paulo akaamua awaokoe Mataifa! Biblia Iko wazi Mataifa sio Uzao wa Adamu.
Huo ni Utafiti wangu Binafsi na Imani yangu lakini hata ningekaribishwa Katika Kanisa kutoa Mahubiri. Naongea ya Kawaida tu hayo nayaacha Moyoni!

ADAM and EVE are not the Origins of all Man, though I believe all man were established by God how when, I dont know! Dunia imekuwepo miaka mingi kabla ya Adamu na Watu na Viumbe vingine wamekuwepo miaka mingi kabla ya Adam!
 
You might be correct!!
 
You might be correct!!
Take time ufuatilie hizi vitu ukitumia Bible, Geography, Science, culture etc utashangaa watu tunavyo settle for simple and false assumptions! Na usidhani mimi simwamini Mungu, Mimi ni mlokole anayesali na kufunga! Naweza kufunga na kukaa mahali kwa siku tatu usiku na Mchana bila kusema lolote, Kisha nikisha kutafakari naomba kwa lisaa limoja na navunja Kufunga. Nimeona mengi ya ajabu ila siweze kusema mengine. Do you know even some humans are born directly by the will of the devil and with his Spirit! Anazaliwa Shetani, anaishi shetani na mpaka anaondoka duniani ni shetani. Why do you think God in the Bible rejected Essaw? And He made sure the father Issac will be blind cause God knew being human, Issac would insist on blessing Essau instead of Jacob! God found it hard to let Issac know that your his born Essau was the seed of the devil. Je umeshawahi kukutana na watu wa aina hii?
 
Huu ukiristo ni laana tupu!!!! Viongozi wao matapeli hasa huku Africa ni utapeli mtupu. Tazama akina gwajima na matapeli wengi na ukianzisha kanisa tu umeshakuwa milionea. Wale wa uzunguni nao wana bariki ushoga yaani ni laana tupi
Acha povu ww, sio ukristo. Be specific. Haya yote yametabiliwa ndani ya biblia na kwa ambao tunaamini biblia hatushangai kwani unabii ni shart utimie.
 
Back
Top Bottom