Huu ndio Utapeli wa "Prophet Bushiri" Anayemtishia Lowassa

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Nilisikiliza Madai ya Askofu Gwajima Dhidi ya Tapeli mmoja aitwaye Prophet Bushiri. Jinsi ambavyo anatumiwa Kutabiri ati Lowassa atakufa.

Wasichojua watu wengi Ni kuwa Wengi wa wanaoitwa Watumishi wa Mungu, Kiasi kikubwa ni Mbwa mwitu Matapeli wa Kutisha.

Nitaweka Mambo Kadhaa ya Kitapeli anayofanya Bushiri. Mojawapo ni Kujifanya alitabiri kuhusu Tetemeko, hawa wanachofanya ni Kungojea Tukio kubwa linatokea, halafu wanatengeneza Video inayoweka sauti yake juu ya Video nyingine ya zamani kabla ya Tukio na Wanasuparimpose maneno mapya (lipsing) juu ya hiyo video ya zamani ili isikike kana kwamba alikuwa akitabiri Tukio hilo, ilihali katika video ya awali, alikuwa akiongelea mengine kabisa!

Mengine ni Kutengeneza Mazingaumbwe ya Michezo ya Kitoto mfano kama huu. Bushiri akijifanya anashusha moto toka mbinguni Kuchoma hirizi. Ukweli ni kuwa ameweka kemikali yenye kutoa moto na akaongezea kiberiti juu yake ili kikipata joto la kemikali kilipoke moto!


Angalia kwa makini.

Na hii Video nyingine anachukua Video ya Zamani ambayo watu walikuwa wakiomba, anaiedit na kusema wanaona Malaika halafu ukisikiliza jibu analopewa ni la mtu wa studio maana halaiki ya watu wale haikuwa naye wakati akiongeza hiyo sauti mpya na ukungu wa malaika.





Sasa Ukiona Mtu anaweza Kudanganya Maelfu ya Watu Kiasi hiki, Hata kuua mtu hatasita! Nimemsikia Katika Video Fulani akisema alimwombea Mchungaji mmoja afe, na akafa sasa, ni wazi Tapeli wa Aina hii anaweza hata kumtumia mtu Majambazi ili wamuue kisha ajidai Utabiri wake umetimia.

Gwajima asidanganyike Bushiri haombei afe, Bali Bushiri anaweza hata Kumtumia Majambazi! Gwajima.
 
KMimi nakumbuka 2015 kuwa Magufuli atashinda na ikawa,kuhusu Lowasa hakutaja jina ila alisema kuwa kuna kiongozi mkubwa wa upinzani atapatwa na maradhi.Gwajima aache miemko!
 
Nakumbuka yule transformer alitabiri waandishi wa habar kufa hadi ifikapo mda Fulani! Baada ya kumuandika anakunywa viroba..sijui unabii wake ulitimia? MUNGU aturehemu sana na hawa manabii wa uongo ni ngumu kuwatambua
 
Wakati mwingine huwa nikitizama movies za hollywood nashindwa kujizuia kuamini kwamba ni maigizo....yaan vitu ni kama kweli kabsaaa! So is bushiri na wenzake miracles....
 
Back
Top Bottom