Wewe ulishawahi kumuona huyo mungu ? Au hukumtafuta bado..
mungu sijawahi kutamani kumtafuta ila Mungu kwa kweli nimeshuhudia uwepo wake kwangu na ninazidi kuuona. Amenibadilisha sana na hata watu wanaonifahamu wanamtukuza Mungu na wanakiri kuwa hakika mimi kuwa hivi nilivyo ni Mungu kanionekania.
Ndio maana Natamani wengine pia wapate neema ya kumjua Mungu wa kweli na wamtumikie kwa kuwa kusudi la sisi kuwepo hapa Duniani ni kutiisha, kumiliki na kutawala, na kuzidisha vitu vyote alivyoumba Mungu na uwezo huo ameuweka ndani yetu.
Ukishapata maarifa juu ya makusudi ya Mungu kukuweka hapa Duniani unafunguliwa macho then unaanza kuona yale ambayo sio kila mtu anaona na hapo ndio utamtukuza Mungu na kumtegemea yeye siku zote. Na huo ndio utaratibu wa Mungu kwamba ukishaelewa yeye anaachilia nguvu yake juu yako na unaona nuru na anakuletea udaidizi ws Roho wa Mungu.
Ukikosa maarifa haya ya Mungu ni rahisi sana shetani kukuchezea na kukutesa. Utafanya kazi kwa bidii, utapata fedha lakini unaweza usione zikikusaidia zaidi ya kuleta uharibifu na masumbufu na kukuondolea amani uliyo nayo.
Unaweza ukawa na kipato kizuri tu lakini usiweze kuwa hata na kitu cha kuhamisha kwenda kwa watoto wako au wajukuu na vitukuu kwa sababu huna usaidizi na huoni. Au ukawa na fedha ya kutosha ikaishia kwenye mambo yasiyo ya msingi lakini kwa mtazamo wako utaona ni ya maana, na hii inakuwa hivyo kwa kuwa fedha yako haina ulinzi na inakuzidi nguvu kwa kuwa huna mamlaka ya kuitiisha na kuimiliki.
Tusiishi kwa kupapasa na kubahatisha. Tumtafute Mungu kwa bidii katika Roho na kweli na kwa kumaamisha na tutaona uwepo wake na usaidizi. Pia tuwe na tabia ya kusoma neno la Mungu na tumsihi Roho Mtakatifu atufundishe kwa kuwa yeye ndiye mwalimu, kiongozi, msaidizi, na mkumbushaji, na anatuombea pia. Tumpe nafasi.
Mfalme Sulemani mwana wa Daudi alisema "Mpumbavu husema moyoni mwake hakuna Mungu".