Huu ndio Utapeli wa "Prophet Bushiri" Anayemtishia Lowassa

Huu ndio Utapeli wa "Prophet Bushiri" Anayemtishia Lowassa

Kwenye harakati za kutafuta uso wa Mungu watu wanaingia kirahisi kwenye mitego ya watenda miujiza feki na wengine wakitumia nguvu za giza. Ni vyema kujua historia ya mchungaji unayeabudu kwake ili walau ujue amepatia wapi daraja hilo then ndio uhamie kupima kama anahubiri injili ya kweli? ....Paulo hakuwa sehemu ya mitume lakini alipokutana na Yesu hakuanza tu kufungua Kanisa na kuhubiri bali alienda kwa mitume ambao ndio waliomuwekea mikono akafanye kazi ya Bwana. Siku hizi mtu anasema amekutana na Yesu ndotoni then anafungua Kanisa! Paulo aliyekutana nae live pengine ndio asingewasikiliza kabisa mitume ......huduma za Kanisa ni madaraja ambayo yanautaratibu wake toka enzi za Kanisa la kwanza na si mtu kuibuka tu kama mzimu .....
Mkuu asante sana kwa comment hii.Hakuna hata mtume mmoja aliomba apewe kazi ya Utume Bali Yesu ndio aliona kama mtu Fulani anafaa au sivyo.Leo watu wanajipachika tu madaraka iwe mchana au asubuhi.
 
Hakuna manabii ni matapeli watupu. Na wewe unaleta maandiko ya laaana hapa kutetea majitu laaana nyinyi ndio hata mkiambiwa vua nguo uliwe tigo nikutie baraka unafanya. Amkeni sio mnatapeliwa na mpo mpo tu. Lakini siwalaumu ikiwa maviongozi wenye dhamana ya nchi wanakwenda eti kuombewa na mijitu laaana kabisa
Vip kwani Nabii Yeremia na Nabii Eliya kwako ni matapeli kwa kuwa walitabiria watu vifo?hekima ya Mungu ni kubwa kuliko ufahamu wetu.
 
Hivi yule aliyetabiri waandishi wa habari mwezi wa tatu watakufa bado tu wazima au walikufa???? Je kama hawajafa ,kaanza kuuza gongo au bado????

Mimi nadhani hata vyombo vyetu vya habari bado havina uweledi Wa kutosha.Walipaswa muda huu watoke na makala nzito kueleza kwamba wale waliotabiriwa naye kifo wako hai tena wakiwa hard as nails.Kwamba pengine wamefanikiwa wengine kupandishwa vyeo na wengine wamejenga nyumba au wamezidi kumudu ada za watoto wao licha ya maombi ya uchuro ya huyo jamaa.
 
KMimi nakumbuka 2015 kuwa Magufuli atashinda na ikawa,kuhusu Lowasa hakutaja jina ila alisema kuwa kuna kiongozi mkubwa wa upinzani atapatwa na maradhi.Gwajima aache miemko!
Jina alitaja wewe ndiye hukusikia na ametabiri more than one
 
waliopotea ni wale wanaosema mungu ana mwana ! wewe uwe na watoto na mungu awe na katoto kamoja tu, kisha kaishie msalabani .....damn !

Inaelekea unafikiria kinyume nyume.Kama wewe unaweza kuwa na mtoto Mungu anashindwaje kuwa naye? Kama wewe unaweza kujenga Nyumba nzuri hadi watu wakaigwaya Mungu anashindwaje kuwa nayo nzuri kupita yako? Tumia Mantiki.
 
Hata Gwajima ana tabia ya kutishia watu kufa kama alivyokuwa akimtishia Makonda. Kwa hiyo Bushili na pwagu na gwajima na pwaguzi. Wote matapeli tu na asilimia kubwa ya wachungaji wa kisasa ndo dili zao hizi za upwaguzi.

Ndo maana ninaendelea kuabudu katika kanisa moja takatifu katoliki la mitume hakunaga watu kujifanya wanatenda hii miujizaujiza ya kijuha

Katoliki isn't best either. Mambo ya kuomba wafu wawaombee kwa Mungu why msiombe wenyewe kama Kristo alivyoagiza? Soon mtapata sala like Mtakatifu nyerere utuombee??? Mmh no don't dis others na kubrag vyako wkt vyako navyo wingu tupu.
 
Hamna nabii wa ukweli miaka hii, watu wanapiga hela za kununua ma private jets tu
 
Inaelekea unafikiria kinyume nyume.Kama wewe unaweza kuwa na mtoto Mungu anashindwaje kuwa naye? Kama wewe unaweza kujenga Nyumba nzuri hadi watu wakaigwaya Mungu anashindwaje kuwa nayo nzuri kupita yako? Tumia Mantiki.
Mantiki ni Mungu anaumba na hazai mtoto ! ...Mwenyezi Mungu hutamka kuwa na ikawa. Ametakasika na huo upuuzi mnao mbandikiza nao !
 
Hamna nabii wa ukweli miaka hii, watu wanapiga hela za kununua ma private jets tu
Kwa Waislaam ukisema wewe ni Nabii, wamekuheshimu sana basi kila mtu atashika njia endezake, vinginevyo utapigwa tu maana hamna namna !
 
Mantiki ni Mungu anaumba na hazai mtoto ! ...Mwenyezi Mungu hutamka kuwa na ikawa. Ametakasika na huo upuuzi mnao mbandikiza nao !

Kwa hiyo kuzaa siyo sehemu ya uumbaji? Kama uumbaji unatokana tu kutamka unajuaje kuwa Mungu huwa hatamki tu na kisha ndio mbegu ya kiume ikaungana na ya kiume? Kwani Mungu akiwa na mtoto wewe itakuzuia kufika Mbinguni? Kama Mungu asingekuwa na mtoto angewezaje kuwa na uchungu na wewe kama mwanaye? Je, na wewe sio mtoto Wa Mungu?
 
Nilisikiliza Madai ya Askofu Gwajima Dhidi ya Tapeli mmoja aitwaye Prophet Bushiri. Jinsi ambavyo anatumiwa Kutabiri ati Lowassa atakufa.

Wasichojua watu wengi Ni kuwa Wengi wa wanaoitwa Watumishi wa Mungu, Kiasi kikubwa ni Mbwa mwitu Matapeli wa Kutisha.

Nitaweka Mambo Kadhaa ya Kitapeli anayofanya Bushiri. Mojawapo ni Kujifanya alitabiri kuhusu Tetemeko, hawa wanachofanya ni Kungojea Tukio kubwa linatokea, halafu wanatengeneza Video inayoweka sauti yake juu ya Video nyingine ya zamani kabla ya Tukio na Wanasuparimpose maneno mapya (lipsing) juu ya hiyo video ya zamani ili isikike kana kwamba alikuwa akitabiri Tukio hilo, ilihali katika video ya awali, alikuwa akiongelea mengine kabisa!

Mengine ni Kutengeneza Mazingaumbwe ya Michezo ya Kitoto mfano kama huu. Bushiri akijifanya anashusha moto toka mbinguni Kuchoma hirizi. Ukweli ni kuwa ameweka kemikali yenye kutoa moto na akaongezea kiberiti juu yake ili kikipata joto la kemikali kilipoke moto!


Angalia kwa makini.

Na hii Video nyingine anachukua Video ya Zamani ambayo watu walikuwa wakiomba, anaiedit na kusema wanaona Malaika halafu ukisikiliza jibu analopewa ni la mtu wa studio maana halaiki ya watu wale haikuwa naye wakati akiongeza hiyo sauti mpya na ukungu wa malaika.





Sasa Ukiona Mtu anaweza Kudanganya Maelfu ya Watu Kiasi hiki, Hata kuua mtu hatasita! Nimemsikia Katika Video Fulani akisema alimwombea Mchungaji mmoja afe, na akafa sasa, ni wazi Tapeli wa Aina hii anaweza hata kumtumia mtu Majambazi ili wamuue kisha ajidai Utabiri wake umetimia.

Gwajima asidanganyike Bushiri haombei afe, Bali Bushiri anaweza hata Kumtumia Majambazi! Gwajima.

Hata wewe mtoa post ni ndondocha tu na wewe.km bado unaweza kuamini maneno ya manabii wa shetani una nn kuchwani mwako.bushiri na gwajima woote ni matapeli wakubwa.ni mbwa mwiitu.NAKUOMBA USIJARIBU HATA KUWATOLEA MFANO WOOTE. GWAJIMA BONGE LA TAPELI BUSHIRI BONGE LA TAPELI .
 
Huyu jamaa anatumia fedha au shetani ,sidhani kama anamtumikia Mungu, sema Mungu wa Mbinguni ni mvumilivu sana, angekua kama mwanadamu kuna watu kama bushiri wangekua wamechomwa moto.
 
Kwa hiyo kuzaa siyo sehemu ya uumbaji? Kama uumbaji unatokana tu kutamka unajuaje kuwa Mungu huwa hatamki tu na kisha ndio mbegu ya kiume ikaungana na ya kiume? Kwani Mungu akiwa na mtoto wewe itakuzuia kufika Mbinguni? Kama Mungu asingekuwa na mtoto angewezaje kuwa na uchungu na wewe kama mwanaye? Je, na wewe sio mtoto Wa Mungu?
Kwahiyo Mariam alitiwa mbegu za kiume ili Yesu azaliwe !.? .....damn ! mimi ni mwana wa Adam, kwa kiarabu ni Bin Adam
 
Wameshawageuza waumini wao mambumbumbu ndio wanadhani watadanganya kila mtu!

Sadaka zangu nitapelekea maskini na watu wasiojiweza sio hawa wafanyabiashara wa dini!
ni kweli kabisa, ni heri ukusanye sadaka yako mwenyewe na kila mwisho wa mwezi upeleke kuroba cha sembe kwenye nyumba za yatima.
 
Una uhakika wa ulichokiandika? Una amini katika MUNGU wa Yesu Kristo kuwa nabii Bushir ni tapeli na Askofu Gwajima ni mwaminifu mbele za MUNGU? MUNGU wetu hadhihakiwi,atajithibitisha uwezo wake.Hategemei wanadamu bali sisi wanadamu humtegemea yeye.Tunaomba athibitishe sawasawa na neno lake nani ni mtumishi wake.

Kama Elia na manabii wa Baali walivyojidhihirisha na hawa wawili wajidhihirishe.

Wewe ni mfia Dini jiangalie sana
 
Hakuna lolote hao wasaka pesa tu ,wanejaa unafiki na upumbavu , binadamu toka lini akatabili kifo cha binadamu mwenzake?? Nabii walikuwepo enzi hizo si sasa
 
Back
Top Bottom