Huu muujiza na ushuhuda niliosikia kwa Mwamposa umenistua

Kwa uelewa wangu wa kibangibangi,wenye HIV wakimeza manjugu ukipima virusi havionekani.Sasa mama anatafuta wajinga walete manjugu yao ayaombee wameze wakapime test ionyeshe negative awapige pesa kuwa amewaponya.Simple like that.
Na wengi wakishatoka kupima huko, wanakuja kutoa ushuhuda kuwa wameponywa HIV then wanaacha kula dozi; kinachofuata sasa...
 
Huwa sipendi sana kuingilia imani ya mtu ila kwa jana nimeona kabisa MTUME na NABII Mwamposa kuna dalili za upigaji

Kuna mahali nilikuwepo wameweka ile chanel yake watu wanatoa ushuhuda jamaa mmoja akasema alienda kuomba apate hela akala na keki siku hiyo yupo nyumbani akashangaa sms kucheki amepokea milioni 10 hajui ilipotoka kwa hofu akamshirikisha jirani, jirani akamwambia katoe labda Mungu kakuona akaenda kwa wakala kutoa ilivyotoka ikaingia tano ingine akatoa

Najiuliza mtandao gani wa simu laini inaweza pokea milioni 15 na ikatoka ndani ya lisaa limojatena bora angekuwa mtu wa kutumia miamala jamaa anadai hakuwahi weka kwenye simu hata laki.

Jamaa akaendelea baada ya kutoa ile tano ikaingia mbili akatoa tena jumla akawa na milioni 17(sijui roho mtakatifu alilipia makato) jamaa anadai hakuwahi miliki milioni moja yake ila kwa mara ya kwanza akawa amepata milioni 17 akarudi home akaanza harakati za Ujenzi, mpaka sasa amefanikiwa kujenga, kununua pikipiki na kafungua biashara, anadai kuwa ule mtindo wa kupokea hela uliendelea hadi akakamilisha ujenzi wa nyumba ya Milioni 30 biashara na usafiri(pikipiki)sasa hivi ana mpango wa kununua gari.

Hela zote hajui zinatoka wapi.

Daah MUNGU anisamehe tu ila huu ni utapeli wa hadharani
Mbona huyo Mwamposa mwenyewe hajawahi kupata muujiza kama huo? Yeye pesa anapata kwa hao hao mazuzu maana anajua za miujiza hazipo.
 
Mbona huyo Mwamposa mwenyewe hajawahi kupata muujiza kama huo? Yeye pesa anapata kwa hao hao mazuzu maana anajua za miujiza hazipo.
Muujiza sio wa pesa tu hivyo pengine huwezi kujua yeye Mwamposa ameshakutana na miujiza gani kwenye maisha yake.
 
Hawa manabiii walishaona Watanzania ni vipofu acha wajipigie hela kutokana na ujinga wetu
NB; maisha haya kina mama na watoto ndio wanaopata shida duniani
 
Unategemea nini toka kwa watu waliokubali kuitwa wanakondoo? Kondoo hawana akili unawaswaga tu wanaenda unakotaka. Ndivyo hawa wanaojiita mitume wengi wanavyofanya.

Ni kama vile uwa wanashindana kuonyesha ni nani ambaye ana kondoo wajinga kuliko mwenzake. Utakuta huyu anawavua kondoo wake wa kike chupi madhabahuni nao wanakubali, huyu anakula ugali madhabahuni anaita kondoo wake wa kiume waje wamlambe mikono.
Huyu anawanywesha dawa ya kuulia wadudu.

Ukikubali kuwa kondoo kwisha kazi.
Sure
 
Hii inaonyesha Ni kiasi gani Mwamposa Hana elimu.
Amesahau kila mtandao una limit ya kupokea pesa.
Amesahau TOZO ?the guy must be very forgetful. Tozo si kitu Cha juzi tu??
Amesahau makato ya mtandao.
15 M unaitoa yote.
 
Huwa sipendi sana kuingilia imani ya mtu ila kwa jana nimeona kabisa MTUME na NABII Mwamposa kuna dalili za upigaji

Kuna mahali nilikuwepo wameweka ile chanel yake watu wanatoa ushuhuda jamaa mmoja akasema alienda kuomba apate hela akala na keki siku hiyo yupo nyumbani akashangaa sms kucheki amepokea milioni 10 hajui ilipotoka kwa hofu akamshirikisha jirani, jirani akamwambia katoe labda Mungu kakuona akaenda kwa wakala kutoa ilivyotoka ikaingia tano ingine akatoa

Najiuliza mtandao gani wa simu laini inaweza pokea milioni 15 na ikatoka ndani ya lisaa limojatena bora angekuwa mtu wa kutumia miamala jamaa anadai hakuwahi weka kwenye simu hata laki.

Jamaa akaendelea baada ya kutoa ile tano ikaingia mbili akatoa tena jumla akawa na milioni 17(sijui roho mtakatifu alilipia makato) jamaa anadai hakuwahi miliki milioni moja yake ila kwa mara ya kwanza akawa amepata milioni 17 akarudi home akaanza harakati za Ujenzi, mpaka sasa amefanikiwa kujenga, kununua pikipiki na kafungua biashara, anadai kuwa ule mtindo wa kupokea hela uliendelea hadi akakamilisha ujenzi wa nyumba ya Milioni 30 biashara na usafiri(pikipiki)sasa hivi ana mpango wa kununua gari.

Hela zote hajui zinatoka wapi.

Daah MUNGU anisamehe tu ila huu ni utapeli wa hadharani
😂😂😂
 
Ushuhuda una chembe chembe za miujiza

Kihalisia kiwango cha mwisho kuhifadhi kwenye simu ni chini ya milion 4

Ila kwa mwamposa lolote linawezekana, yale maji yana power ya kupumbaza servers za mitandao na kufanya milion 10 iwe detected kama milion 1

Halafu kingine ambacho shuhuda hakukisimulia ni pesa ya makato, unajua ukishapata upako wa mwamposa hakuna muamala wowote ambao utakuwa na tozo wala makato?

Ni muda tu haukuwa rafiki ila shuhuda alikuwa na mengi ya kusimulia na yakushangaza na kuonesha ukuu wa Mungu kupitia nabii wake mnyakyusa mwamposa

Shalom

Unaweza kupokea Mpaka million 50 inategemea na line uliyonayo company ya Simu wanakuwezesha

Japo Hii story ni ya kusadikika tumepigwa na kitu kizito🤣🤣🤣
 
Mama alikuwa amejipara... Alikuwa ametengeneza ocult.
Akamalaghai hadi mama kanunba eti anaenda kumwonyesha kanumba kufika kamwonyesha eti mdada kanisani kwake akasema ndo roho ya kanumba imeingia hapo..
Yule mama alikuwa katengeneza ocult kabisa yani waumini wakimwona wanasujudu yani kuna muda unajiuliza hivi ubongo uwa unapigwa shoti au.
Kuna video niliona eti wanapigana vita ya amagadon. Yani watu wazima si wanawake si wanaume wanaviringishana kwenye mchanga halafu yeye huyo zumaridi anasema kwenye macho ya nyama unaona kawaida ila ulimwengu wa roho wanapigana hapo wanaelekea kushinda ni vita kali ila yeye alikuwa hapigan hataki chafuka
 
Nlishawahi soma ushuhuda wao kwenye gazeti lake wanauza hapo kanisani..kulikua na mpangaji kanipa ye no muumini hapo..jamani jamani
Eti mmoja anasema anashukuru mwanae kapona alikua anasumbuliwa na Kansa ya ubongo,akaenda hospital madokta wakamwambia inabidi tumfanyie operation mwano tumtoe huo ubongo atakufa.akaubalai wakamtoa. Akabakia fuvu ndani tupu.

Kuna mwingine akasema alikua na mtaji wa million kumi duka.likafilisika lote hadi akaishiwa.akaja kuombewa asahivi duka na mtaji umerudi tena
.nkajiuliza umerudije

Mwingine anadaia alikua hana jamani ana madeni makubwa na hela hana,akaja kuombewa madeni yakaisha..najiuliza yaliisha kimiujiza ama wenye pesa zao walimsamehe.
 
Kwanza mwamposa sio MTUME wala NABII,, hii ni taka taka inayocheza na akili za akina mama
Huwaambii kitu kuhusu huyo mpuuzi🤣🤣🤣
 
Nlishawahi soma ushuhuda wao kwenye gazeti lake wanauza hapo kanisani..kulikua na mpangaji kanipa ye no muumini hapo..jamani jamani
Eti mmoja anasema anashukuru mwanae kapona alikua anasumbuliwa na Kansa ya ubongo,akaenda hospital madokta wakamwambia inabidi tumfanyie operation mwano tumtoe huo ubongo atakufa.akaubalai wakamtoa. Akabakia fuvu ndani tupu.

Kuna mwingine akasema alikua na mtaji wa million kumi duka.likafilisika lote hadi akaishiwa.akaja kuombewa asahivi duka na mtaji umerudi tena
.nkajiuliza umerudije

Mwingine anadaia alikua hana jamani ana madeni makubwa na hela hana,akaja kuombewa madeni yakaisha..najiuliza yaliisha kimiujiza ama wenye pesa zao walimsamehe.
Walimtoa Ubongo halafu akabaki, hai hivi huwa wanatuchukulia sisi viande😀😅
 
Na wamewashika akili zaidi wanawake, yaani huwaambii kitu kuhusu hao manabii wao. Wanawatetea na kuwaogopa zaidi ya Mungu. Inshort ndio miungu yao hiyo.
 
Back
Top Bottom