Huu muujiza na ushuhuda niliosikia kwa Mwamposa umenistua

mkumbwa junior

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
814
1,545
Huwa sipendi sana kuingilia imani ya mtu ila kwa jana nimeona kabisa MTUME na NABII Mwamposa kuna dalili za upigaji

Kuna mahali nilikuwepo wameweka ile chanel yake watu wanatoa ushuhuda jamaa mmoja akasema alienda kuomba apate hela akala na keki siku hiyo yupo nyumbani akashangaa sms kucheki amepokea milioni 10 hajui ilipotoka kwa hofu akamshirikisha jirani, jirani akamwambia katoe labda Mungu kakuona akaenda kwa wakala kutoa ilivyotoka ikaingia tano ingine akatoa

Najiuliza mtandao gani wa simu laini inaweza pokea milioni 15 na ikatoka ndani ya lisaa limojatena bora angekuwa mtu wa kutumia miamala jamaa anadai hakuwahi weka kwenye simu hata laki.

Jamaa akaendelea baada ya kutoa ile tano ikaingia mbili akatoa tena jumla akawa na milioni 17(sijui roho mtakatifu alilipia makato) jamaa anadai hakuwahi miliki milioni moja yake ila kwa mara ya kwanza akawa amepata milioni 17 akarudi home akaanza harakati za Ujenzi, mpaka sasa amefanikiwa kujenga, kununua pikipiki na kafungua biashara, anadai kuwa ule mtindo wa kupokea hela uliendelea hadi akakamilisha ujenzi wa nyumba ya Milioni 30 biashara na usafiri(pikipiki)sasa hivi ana mpango wa kununua gari.

Hela zote hajui zinatoka wapi.

Daah MUNGU anisamehe tu ila huu ni utapeli wa hadharani
 
huwa sipendi sana kuingilia imani ya mtu ila kwa jana nimeona kabisa MTUME na NABII Mwaposa kuna dalili za upigaj...
Unategemea nini toka kwa watu waliokubali kuitwa wanakondoo? Kondoo hawana akili unawaswaga tu wanaenda unakotaka. Ndivyo hawa wanaojiita mitume wengi wanavyofanya.

Ni kama vile uwa wanashindana kuonyesha ni nani ambaye ana kondoo wajinga kuliko mwenzake. Utakuta huyu anawavua kondoo wake wa kike chupi madhabahuni nao wanakubali, huyu anakula ugali madhabahuni anaita kondoo wake wa kiume waje wamlambe mikono.
Huyu anawanywesha dawa ya kuulia wadudu.

Ukikubali kuwa kondoo kwisha kazi.
 
Huwa sipendi sana kuingilia imani ya mtu ila kwa jana nimeona kabisa MTUME na NABII Mwamposa kuna dalili za upigaji

Kuna mahali nilikuwepo wameweka ile chanel yake watu wanatoa ushuhuda jamaa mmoja akasema alienda kuomba apate hela akala na keki siku

Utapeli huo
 
😂😂😂😂halafu kuna mbwiga zikiona hivyo zinaenda kupanga foleni kusubiri mtonyo wa dezo. Katika hali kama hii si ajabu ukamtumia mtu msg ya salamu akakujibu na tusi. Maana mwenyewe amekaa anasubiri muamala toka kwa 'roho mtakatifu' wewe unamrrusha roho na ka ujumbe kako ka salamu.

Ila hawa watumishi wa dini watakuwa na mengi ya kujieleza kwa Muumba huko. Maana siku hizi wala hawaoni aibu kutapeli kwa kutumia jina la Mungu.
 
Ushuhuda una chembe chembe za miujiza

Kihalisia kiwango cha mwisho kuhifadhi kwenye simu ni chini ya milion 4

Ila kwa mwamposa lolote linawezekana, yale maji yana power ya kupumbaza servers za mitandao na kufanya milion 10 iwe detected kama milion 1

Halafu kingine ambacho shuhuda hakukisimulia ni pesa ya makato, unajua ukishapata upako wa mwamposa hakuna muamala wowote ambao utakuwa na tozo wala makato?

Ni muda tu haukuwa rafiki ila shuhuda alikuwa na mengi ya kusimulia na yakushangaza na kuonesha ukuu wa Mungu kupitia nabii wake mnyakyusa mwamposa

Shalom
 
Back
Top Bottom