Huu muujiza na ushuhuda niliosikia kwa Mwamposa umenistua

Wivu tu..wewe uliwasaidia nini hao wazee.?

#MaendeleoHayanaChama
Wivu tena.. akili zenu nyie ng'ombe wa mwamposa mnazijua wenyewe yani mjinga hata kujenga orphanage adanganye wenye akili zao Napo ameshindwa.

Anyway naomba niishie hapa..

Namkubali Sana Mwakasege.. Mwamposa Hana tofauti na waganga wanaofanya ramli
 
Weee mimi nina ndugu yangu kaokoka yani kila mtu kwake mwanga, kila jirani yake mwanga, anaua mijusi kuwa inatumwaga na wachawi, paka yeyote akikatiza anasema ni mwanga, yani yeye kila kitu hivyo

Nimeona hata jirani yangu
Alikuta paka amekufa.. nikamwambia labda alikula kitu chenye sumu
Akakataa akadai alimwaga maji ya upako toka kwa Mwamposa..
Akasema mtaa una wanga wengi mno.. yaani unakuta wanajenga chuki kwa mambo ya kufikirika
 
We acha yani kuna muda watu wakifa eti utasikia walikuwa wanga hao maombi yao yamewapa kipgo mpaka wamekufa.
😂😂😂
Sijui hata kama wana raha maana naona wanaishi kwa mashaka juu ya kila kitu.
 
Huwa sipendi sana kuingilia imani ya mtu ila kwa jana nimeona kabisa MTUME na NABII Mwamposa kuna dalili za upigaji

Kuna mahali nilikuwepo wameweka ile chanel yake watu wanatoa ushuhuda jamaa mmoja akasema alienda kuomba apate hela akala na keki siku hiyo yupo nyumbani akashangaa sms kucheki amepokea milioni 10 hajui ilipotoka kwa hofu akamshirikisha jirani, jirani akamwambia katoe labda Mungu kakuona akaenda kwa wakala kutoa ilivyotoka ikaingia tano ingine akatoa

Najiuliza mtandao gani wa simu laini inaweza pokea milioni 15 na ikatoka ndani ya lisaa limojatena bora angekuwa mtu wa kutumia miamala jamaa anadai hakuwahi weka kwenye simu hata laki.

Jamaa akaendelea baada ya kutoa ile tano ikaingia mbili akatoa tena jumla akawa na milioni 17(sijui roho mtakatifu alilipia makato) jamaa anadai hakuwahi miliki milioni moja yake ila kwa mara ya kwanza akawa amepata milioni 17 akarudi home akaanza harakati za Ujenzi, mpaka sasa amefanikiwa kujenga, kununua pikipiki na kafungua biashara, anadai kuwa ule mtindo wa kupokea hela uliendelea hadi akakamilisha ujenzi wa nyumba ya Milioni 30 biashara na usafiri(pikipiki)sasa hivi ana mpango wa kununua gari.

Hela zote hajui zinatoka wapi.

Daah MUNGU anisamehe tu ila huu ni utapeli wa hadharani
Ukimsikia Mtu anasali / anaabudu hapo Kwanza jua ana Ubongo dhaifu sana halafu anza Kumdharau Maisha yako yote kwani amekubali Kutekwa na Muhuni, Mchawi na Tapeli wa Kiimani apatikanae Tanganyika Packers Kawe.
 
Mwamposa , Musa richard , kakobe,mwingira, lusekelo na wahuni wengine ni televangelists ambao kazi yao ni kuhubiri kuhusu prosperity gospel kuhusiana na pesa na mafanikio tu then wanasubiri cash ziingie katika mfumo wa sadaka na fungu la ten.
 
Mimi labda muujiza wa mtu KUTAPIKA tandu na mwingine kujisaidia tandu naweza kuuamini,maana Kuna ndugu yangu naye alitapishwa vitu Kama hivyo japo siyo kwa Mwamposa ni Jamaa tuu alishusha maombi baada ya kupata maono.Kuna watu wanapata maono japo hawajiiti wachungaji au mapadri.
 
Weee mimi nina ndugu yangu kaokoka yani kila mtu kwake mwanga, kila jirani yake mwanga, anaua mijusi kuwa inatumwaga na wachawi, paka yeyote akikatiza anasema ni mwanga, yani yeye kila kitu hivyo
Nilisikia nabii anasema mijusi ni darubini za wachawi,,wanatumia kuona ndani kwako kuna nini
 
Huwa sipendi sana kuingilia imani ya mtu ila kwa jana nimeona kabisa MTUME na NABII Mwamposa kuna dalili za upigaji

Kuna mahali nilikuwepo wameweka ile chanel yake watu wanatoa ushuhuda jamaa mmoja akasema alienda kuomba apate hela akala na keki siku hiyo yupo nyumbani akashangaa sms kucheki amepokea milioni 10 hajui ilipotoka kwa hofu akamshirikisha jirani, jirani akamwambia katoe labda Mungu kakuona akaenda kwa wakala kutoa ilivyotoka ikaingia tano ingine akatoa

Najiuliza mtandao gani wa simu laini inaweza pokea milioni 15 na ikatoka ndani ya lisaa limojatena bora angekuwa mtu wa kutumia miamala jamaa anadai hakuwahi weka kwenye simu hata laki.

Jamaa akaendelea baada ya kutoa ile tano ikaingia mbili akatoa tena jumla akawa na milioni 17(sijui roho mtakatifu alilipia makato) jamaa anadai hakuwahi miliki milioni moja yake ila kwa mara ya kwanza akawa amepata milioni 17 akarudi home akaanza harakati za Ujenzi, mpaka sasa amefanikiwa kujenga, kununua pikipiki na kafungua biashara, anadai kuwa ule mtindo wa kupokea hela uliendelea hadi akakamilisha ujenzi wa nyumba ya Milioni 30 biashara na usafiri(pikipiki)sasa hivi ana mpango wa kununua gari.

Hela zote hajui zinatoka wapi.

Daah MUNGU anisamehe tu ila huu ni utapeli wa hadharani
Kibaya zaidi utatukanwa Ukristo na siyo Mwamposa.
 
Back
Top Bottom