Tulimsomesha kwa tabu akang'ang'ania kuolewa, mwisho wa siku akatelekezwa na mapacha

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,150
11,197
Ndugu zangu sijui kwenu wanawake mnawachukuliaje, au ndio mafundisho yenu yale kuwa wanawake wapo wengi hivyo mnawasaidia kwa kuwaoa kwa wingi? Hivi huwa mnawasaidia au ni tamaa zanu mwisho wa siku mnawaletea maisha magumu na kuwaharibia maisha?

Twende kwenye mada

Kuna mtoto wa dada yangu (marehemu); dada alifariki mwaka 2004 akamuacha dogo kichanga kina miezi 5 tu na baba yake alileta mahitaji miezi miwili ya mwanzo tu baada ya hapo akapotea mazima na ndio kitu tunadhani kilimletea dada sonona hadi akafariki.

Hivyo mama yetu akamlea, maana mzee alikuwa kashafariki hivyo mama akachukua mizigo yote hadi mimi na dada zangu tulipokuja kuanza kazi tukampokea akiwa na miaka 5 tukawa tunajichanga tunamsomesha.

Binti tumempambania sana shule za gharama hadi akafika kidato cha nne mwaka 2021. Matokeo yalipotoka akatapa Div 4, hatukukata tamaa, tukajichanga mimi na dada zangu ili aanze chuo.

Tukachanga kama milioni mbili ya kuanzia, ada ya utangulizi ikalipwa kabisa, hapo alikuwa na miaka 17. Ile anakaribia tu kuanza chuo mara akabadilika anasema anataka kuolewa, kapata mchumba.

Tulipopata hizo taarifa kwanza tukachanganyikiwa, maana tulishachoma pesa halafu mtu anakuja kukwambia hataki shule, anadai kapata mchumba anataka kuolewa!

Tukapinga vikali kuwa hilo swala halipo akitaka aondoke akaanze maisha na huyo mchumba, ila hatulitambui hilo na lolote litakalomkuta asitushirikishe maana tulitaka asome kwanza.

Balaa likaja kuwa tayari ana mimba juu. Ile Bi mkubwa (bibi yake) kushtukia akatupigia simu kuwa ni heri aolewe yaishe, akasema kumkataza binti kuolewa hata kama ana mikaa 17 na ni mjamzito shida itamuangukia yeye.

Basi tukasema sisi hatupo kama bibi yake kaamua basi amuite huyo mchumba wake ajitambulishe aoe, amchukue, ila tukasistiza kuwa litakalomtokea huko mbeleni hatutotoa hata mia.

Mama akafanya mpango kuwasiliana na ndugu wakaitana, wakamkaribisha yule mume mtarajiwa. Sasa ile kufika tu pale wanashtukia jamaa kumbe ni Muislam na sisi ni Wakristo!

Shida ikaja atamuoa yule binti kwa ndoa gani? Yule binti akajitetea kuwa baba yake alikuwa ni Muislam hivyo hata yeye ni Muislam, anachotaka yeye ni kuolewa yaishe.

Ila huyo baba yake anaejitetea ni Muislam alimtekeleza akiwa na miezi miwili akakimbia na ile hali ikamletea dada presha akafa ila binti hakujali.

Ndugu wakanyoosha mikono juu wakasema kama umeamua kuolewa kiislam na sisi tumekulea kikristo basi sawa, ila ndoa yako haitafanyikia hapa nyumbani, bwanaharusi atakuja kukuchukulia hapo msikiti wa jirani mtamalizana hapo uende kwenye maisha uliyoyachagua.

Siku ya harusi ikafika yule bwana akachukua jiko, tena walikuja na ndugu zake kwa mbwembwe hadi marafiki zake baadhi wasanii walikuwepo.

Baada ya dogo kujifungua akajifungua mapacha, ile watoto wamefikisha miezi minne yule binti akarudi pale nyumbani kwa kushtukiza.

Bibi yake akampokea akamuuliza kulikoni, yule bwanaharusi akampigia simu bi mkubwa kuwa amepata safari ya kikazi Uganda hivyo anaenda mara moja akirudi atamfuata mkewe maana watoto ni mapacha hivyo angemuacha peke yake angepata shida.

Hapa ninavyowaambia unakaribia mwaka yule bwana hajaonekana kapotea na hajulikani alipo! Binti kamletea mama yetu mzigo mkubwa, juzi mama anatupigia simu kuwa tumtumie hela ya unga na pampers watoto wale, hali ni ngumu.

Dada zangu nao sasa ni watata sana maana ni maaskari hivyo wana misimamo migumu, wamegoma kutoa hata mia na wakirudi likizo wameapa kumtimua kabisa pale.

Hadi sasa hatujatuma hata mia ila tunajua hela tunazomhudumia mama ndio anazipenyeza kwa yule binti ila tunakereka sana na kuumia.

Ila ndugu zangu waislam acheni kufanya ndoa kama mchezo wa kuigiza, yaani Waislam mmeifanya ndoa kuchezewa. Yaani kwenu mtu kuowa leo kesho anaacha ni kawaida maana ni ruksa kuowa hata wanne akiacha anaowa tena.

Mtu anaweza kuoa leo kesho anaacha wiki ijayo anaoa tena sababu mmefanya ndoa kuwa jambo rahisi ambalo mtu akijiskia tu anacheza na binti wa mtu akishamaliza haja zale anatoa talaka anatafuta mwingine anaowa.

Wakristo wameifanya ndoa kuwa sehem ngumu ili mtu akiowa awe na adabu ndio maana ndoa za kikristo zipo kama gereza ukiowa mara moja ndio imeisha na kuvunja ndoa ya kikristo ujipange. Katoliki hadi Lutheran ukiowa mara moja huruhusiwi kufunga ndoa nyingine na ndio maana ndoa za Kikristo zina nafuu ila ndoa za kiislam watu wanaowa kesho ndoa imekufa keshokutwa mtu anaoa tena.

Muangalieni Haji Manara, ndani ya miaka 2 ana ndoa 4, yaani hawezi kuwa na adabu maana dini yake inaruhusu kutoa talaka kesho unachukua mzigo mpya unaoa tena, ukitosheka ushamchakaza mtoto wa mtu unaacha unaowa tena!
 
Ndugu zangu sijui kwenu wanawake mnawachukuliaje, au ndio mafundisho
Yenu yale kuwa wanawake wapo wengi hivyo mnawasaidia kwa kuwaowa kwa wingi?. Hivi huwa mnawasaidia au ni tamaa zanu mwisho wa siku mnawaletea maisha magumu na kuwaharibia maisha

Twende kwenye mada

Kuna mtoto wa Dada yangu(Marehem) Dada alifariki mwaka 2004 akamuacha Dogo kichanga kina miezi 5 Tu na Baba yake alikuwa analeta mahutaji miezi miwili ya mwanzo tu baada ya hapo akapotea mazima na ndio kitu tunazani kilimletea Dada sonona hadi akafariki

Hivyo Mama yetu akamlea maana mzee alikuwa kashafariki hivyo Mama akachukua mizigo yote hadi mimi na Dada zangu tulipokuja kuanza kazi tukampokea akiwa na miaka 5 tukawa tunajichanga tunamsomesha

Binti tumempambania sana shule za garama hadi akafika kidato cha nne mwaka 2021 matokeo yalipotoka akatapa Dv 4, Hatukukata tamaa tukajichanga mimi na dada zangu ili aanze chuo tukachanga kama milioni mbili ya kuanzia,Ada ya utangulizi ikalipwa kabisa hapo alikuwa na miaka 17 ,Ile anakaribia tu kuanza chuo mara akabadilika anasema anataka kuolewa kapata mchumba

Tulipopata hizo taarifa kwanza tukachanganyikiwa maana tulishachoma pesa alafu mtu anakuja kukwambia hataki shule anadai kapata mchumba anataka kuolewa, Tukapinga vikali kuwa hilo swala halipo akitaka aondoke akaanze maisha na huyo mchumba ila hatulitambui hilo na lolote litakalo mkuta asitushirikishe maana tulitaka asome kwanza

Balaa likaja kuwa Tayari ana mimba juu, Ile Bi mkubwa (bibi yake) kushtukia akatupigia sim kuwa ni heri aolewe yaishe akasema kumkataza binti kuolewa hata kama ana mikaa 17 na ni mjamzito shida itamuangukia yeye. Basi tukasema sisi hatupo kama Bibi yake kaamua basi amuite huyo mchumba wake ajitambulishe aoe amchukue ila tukasistiza kuwa litakalomtokea huko mbeleni hatutotoa hata mia.

Mama akafanya mpango kuwasiliana na ndugu wakaitana wakamkaribisha yule Mume mtarajiwa sasa ile kufika tu pale wanashtukia jamaa kumbe ni Muislam na sisi ni Wakristo, Shida ikaja atamuowa yule Binti kwa Ndoa gani? Yule Binti akajitetea kuwa Baba yake alikuwa ni Muislam hivyo hata yeye ni Muislam anachotaka yeye ni kuolewa yaishe

Ila huyo baba yake anaejitetea ni Muislam alimtekeleza akiwa na miezi miwili akakimbia na ile hali ikamletea Dada presha akafa ila Binti hakujali, Ndugu wakanyoosha mikono juu wakasema kama umeamua kuolewa kiislam na sisi tumekuleq kikristo,basi sawa ila ndoa yako haitafanyikia hapa nyumbani bwanaharusi atakuja kukuchukulia hapo msikiti wa jirani mtamalizana hapo uende kwenye maisha uliyoyachagua

Siku ya Harusi ikafika yule bwana akachukua jiko tena walikuja na ndugu zake kwa mbwembwe hadi marafiki zake baadhi wasanii walikuwepo

Baada ya Dogo kujifungua akajifungua mapacha, ile watoto wamefikisha miezi minne yule binti akarudi pale nyumbani kwa kushtukiza Bibi yake akampokea akamuuliza kulikoni, Yule Bwanaharusi akampigia sim Bi mkubwa kuwa amepata safari ya kikazi Uganda hivyo anaenda mara moja akirudi atamfuata mkewe maana watoto ni mapacha hivyo angemuacha peke yake angepata shida

Hapa navyowaambia unakaribia mwaka yule bwana hajaonekana kapotea na hajulikani alipo kuna tetesi kutoka kwa ndugu zake kuwa amekimbilia karagwe huko na ameowa tena mke mwingine

Binti kamletea Mama yetu mzigo mkubwa juzi mama anatupigia sim kuwa tumtumie hela Ya unga na Pampers watoto wale hali ni ngumu nao dada zangu sasa ni watata sana maana ni Maaskari hivyo wana misimamo migumu wamegoma kutoa hata mia na wakirudi likizo wameapa kumtimua kabisa pale

Hadi sasa hatujatuma hata mia ila tunajua hela tunazomhudumia mama ndio anazipenyeza kwa yule binti ila tunakereka sana na kuumia

Ila ndugu zangu waislam Acheni kufanya ndoa kama mchezo wa kuigiza yaani Waislam mmeifanya ndoa kuchezewa, Yaani kwenu mtu kuowa leo kesho anaacha ni kawaida maana ni ruksa kuowa hata wanne akiacha anaowa tena

Mtu anaweza kuowa leo kesho anaacha wiki ijayo anaowa tena sababu mmefanya ndoa kuwa jambo rahisi ambalo mtu akijiskia tu anacheza na binti wa mtu akishamaliza haja zale anatoa talaka anatafuta mwingine anaowa

wakristo wameifanya Ndoa kuwa sehem ngumu ili mtu akiowa awe na adabu ndio maana ndoa za kikristo zipo kama Gereza ukiowa mara moja ndio imeisha na kuvunja ndoa ya kikristo ujipange, Katoliki hadi Lutheran ukiowa mara moja huruhusiwi kufunga ndoa nyingine na ndio maana Ndoa za Kikristo zna nafuu ila ndoa za kiislam watu wanaowa kesho ndoa imekufa keshokutwa mtu anaowa tena

muangalieni Haji manara ndani ya miaka 2 ana ndoa 4 yaani hawezi kuwa nq adabu maana Dini yake inaruhusu kutoa talaka kesho unachukua mzigo mpya unaowa tena ukitosheka ushamchakaza mtoto wa mtu unaacha unaowa tena
POle sana.
Fukuza takataka lifie huko, alichagua mwenyewe.

ngoja waje wenyewe , maagizo ya Mtume
 
Tumeni tu hela, mapacha hawana hatia
 
Bibi yake ndio analea ujinga sisi tushamfungia vioo mda apambane na hali yake
Ndugu yangu na hiyo siyo ya kwanza, watoto wa kike wanafanya ujinga huo. Janatu, some two weeks binti amejifungua mtoto baada ya kupata mimba akiwa form2. Wanandugu walimchapa sana akiwa darasa la saba, form one kuacha uzinzi, hakusikia. Juzi kimekosa damu, watu wanahangaika kuokoa maisha yake, wale aliokataa kuwasikiliza...... sasa kimezaa, shida tupu aliyekpa mimba katopotea
 
Hatari
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom